Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Rais Hassan Rouhani Amtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini kwa Mara ya Pili Chapa
13/09/2014
Hujjatul Islam Walmuslimin Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo asubuhi (Jumamosi) amekwenda kumtembelea tena Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei hospitalini alikofanyiwa upasuaji wa tezi kibofu.
Rais Rouhani amekwenda hospitalini hapo mara baada ya kurejea nchini kutoka katika safari yake ya siku tano katika nchi mbili za Asia ya Kati.
Rais Rouhani ameelezea kufurahishwa kwake na hali nzuri ya afya ya kimwili na kiroho aliyomkuta nayo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuomba Mwenyezi Mungu ampe umri mrefu uliojaa baraka na afya kamili ili aendelee kulitumikia taifa la Iran, ulimwengu wa Kiislamu, Maipnduzi ya Kiislamu na utamaduni wa Kiislamu.
Amesema: Kuwepo kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kunadhamini harakati inayozidi kustawi ya kuimarika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kwa upande wake, Ayatullah Udhma Khamenei amemuombea dua Rais Rouhani ili aweze kuzidi kupata mafanikio yeye na serikali yake katika kutekeleza majukumu yao na kumwambia: Mimi wakati wote ninakuombeeni dua za kheri.
Rais Rouhani kwa upande wake amemshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mapenzi yake hayo na kusema kuwa ni kwa mapenzi na uungaji mkono huo wa Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ndiko ambako hadi hivi sasa kumeiwezesha serikali yake ifanikiwe kuvuuka katika baadhi ya changamoto na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hali itakuwa hivyo hivyo katika changamoto za usoni.
Vile vile Rais Rouhani amegusia safari yake ya siku tano katika nchi mbili za Asia ya Kati na kushiriki kwake katika kikao cha wakuu wa Shirika la Ushirikiano wa Shanghai na kusema kuwa, mazungumzo aliyofanya na viongozi mbali mbali wa ngazi za juu katika safari yake hiyo yalikuwa mazuri sana na ya maana.
Ameongeza kuwa katika mazungumzo yake na viongozi wa nchi mbali mbali, marais wote na hususan Rais wa Russia waliulizia hali ya Kiongozi Muadhamu na kumtumia salamu maalumu.
Itakumbukuwa kuwa siku ya Jumatatu iliyopita, Rais Hassan Rouhani alikwenda kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hospitalini mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu (prostate) na ndipo alipofunga safari iliyokuwa imeshapangwa tangu zamani, nje ya nchi.
Siku hiyo ya Jumatatu Rais Rouhani alisema: Hamu yangu ni kwamba nibakie Tehran, lakini Kiongozi Muadhamu mwenyewe amenieleza kuwa niendelee na safari yangu hiyo kama ilivyopangwa.
 
< Nyuma   Mbele >

^