Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ayatullah Amini,Viongozi, Wasanii Wamtembelea Kiongozi Muadhamu Hospitalini Chapa
14/09/2014
 Ayatullah Amini, leo jioni amekwenda hoptalini alikolazwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei kwa ajili ya kumjulia hali na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu apate afya kamili ya haraka.
Vile vile mawaziri kadhaa na Manaibu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Kiislamu ya Iran, baadhi ya wawakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) mikoani na katika taasisi za Mapinduzi ya Kiislamu, wawakilishi wa Maayatullah Safi Golpaygani, Makarim Shirazi, Mousavi Ardebili, Kabeli na Sayyid Said Hakim, baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wanachuoni Wataalamu (linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu) na wajumbe wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nao wamekwenda kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hosptalini.
Wengine waliofika hospitalini hapo kwa ajili ya kujulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni pamoja na Dk Zahra Mostafavi, mwana mkubwa wa Imam Khomeini (quddisa sirruh) mafudhalaa (wanafunzi wa kidini) na walimu kadhaa wa Hawza (Chuo Kikuu cha kidini), wakuu wa taasisi za wawakilishi wa Kiongozi Muadhamu katika Vyuo Vikuu, wawakilishi wa jumuiya za wanachuo, kundi la watoto na wake wa mashahidi wa vita vya kujihami kutakatifu na shakhsia wengine kadhaa pamoja na wakuu wa sekta tofauti nchini.
Vile vile katika kipindi cha jana na leo, malenga na wasanii kadhaa pamoja na watu wa utamaduni na fasihi, watu wa vyombo vya habari pamoja na wanamichezo, nao wamefika hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuzungumza naye kwa karibu na kwa mapenzi makubwa.
Jana pia Ayatullah Naseri Dolat Abadi, mmoja wa maulamaa wakubwa wa Isfahan alikwenda hospitalini hapo alipolazwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe afya ya haraka na amuongezee taufiki katika kazi zake za kila siku.
 
< Nyuma   Mbele >

^