Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Awasilisha Siasa Kuu za Elimu na Teknolojia Chapa
20/09/2014
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewasilisha siasa kuu za elimu na teknolojia baada ya kushauriana na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu kama anavyopewa haki hiyo na kifungu cha 110 cha katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Matini ya siasa hizo kuu za elimu na teknolojia ambazo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameziwasilisha kwa wakuu wa mihimili mitatu mikuu ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama) na kwa Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Siasa kuu za elimu na teknolojia (mfumo wa elimu ya juu, utafiti na teknolojia)
1 - Jihadi ya kuendelea na isiyosita ya kielimu kwa ajili ya kuifanya Iran kuwa marejeo makubwa ya kielimu na kiteknolojia duniani kwa kusisitizia mambo yafuatayo:
1 - 1 - Kuzalisha elimu na ustawi wa ubunifu na utoaji wa nadharia.
1 - 2 - Kuiunua nafasi ya nchi kimataifa katika elimu na teknolojia na kuibadilisha Iran kuwa kambi na kituo muhimu cha elimu na teknolojia katika ulimwengu wa Kiislamu.
1 - 3 - Kustawisha elimu kuu na utafiti wa kimsingi.
1 - 4 - Kuleta mabadiliko na kunyanyua masomo ya Sayansi ya Jamii hususan kutilia nguvu sana na kusoma kwa kina mafundisho ya kidini na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu kwa kusisitizia mambo yafuatayo: Kutia nguvu na kunyanyua nafasi ya elimu hizo, kuvutia watu wenye vipaji na misukumo inayotakiwa katika elimu hizo, kufanyia marekebisho na kuangalia upya matini za kufundishia, kuwa na mipangilio na njia nzuri za ufundishaji, na kuongeza kiwango na idadi ya vituo na harakati za kiutafiti zinazohusiana na elimu hizo.
1 - 5 - Kupata elimu na teknolojia za kisasa kwa kuweka siasa na mipangilio maalumu.
2 - Kustafidi vizuri na utendaji na muundo wa mfumo wa elimu na utafiti nchini kwa lengo la kufikia kwenye shabaha za hati ya malengo ya muda mrefu na ustawi wa kielimu kwa kusisitizia mambo yafuatayo:
2 - 1 - Kusimaia na kuedesha vizuri masuala ya elimu na utafiti na kuleta mfungamano wa kina katika sekta mbali mbali kwenye utungaji sera na siasa tofauti; kuweka mipango na usimamiaji wa kiistratijia katika nyanja za elimu na teknolojia na kustawisha mtawalia vielelezo mbali mbali na kuifanya ya kisasa mara kwa mara ramani kuu ya kielimu nchini kwa kuzingatia mabadiliko ya kielimu na kiteknolojia katika elimu yanayotokea kwenye eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla.
2 - 2 - Kuufanyia marekebisho mfumo wa kupokea wanachuo na kuvipa mazingatio maalumu vipaji na masomo wanayoyapenda wanachuo katika kuchagua kozi za kujifunza na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na Vyuo Vikuu ikilinganishwa na mihula iliyotangulia ya masomo ya kuhitimu.
2 - 3 - Kupangilia vizuri na kutia nguvu mifumo ya usimamiaji mambo, tathmini, kuainisha itibari na uainishaji wa itibari ya vitu mbali mbali katika masuala ya elimu na teknolojia.
2 - 4 - Kupangilia vizuri mfumo kamili na unaofaa wa taifa wa takwimu na taarifa za kielimu, kiutafiti na kiteknolojia.
2 - 5 - Kusaidia na kuunga mkono uanzishaji na ustawishaji wa bustani na vijiji vya elimu na teknolojia.
2 - 6 - Kugawa kiuadilifu fursa na suhula za elimu na utafiti katika elimu ya juu kote nchini.
2 - 7 - Kutafuta na kugundua watu wenye vipawa, kulea vipawa bora na kuhifadhi na kuvutia uwekezaji wa kibinadamu.
2 - 8 - Kuongezwa bajeti ya kazi za utafiti na uhakiki kwa uchache kwa asilimia 4 zaidi ya uzalishaji ghafi wa ndani hadi kufikia mwaka 1404 (Hijiria Shamsia swaw na mwaka 2025 Milaadia) kwa kutilia mkazo matumizi mazuri ya vyanzo vya utajiri na kustawisha matumizi mazuri ya vyanzo hivyo.
3 - Kutawala misingi, matukufu, maadili na mafundisho ya Kiislamu katika mfumo wa elimu ya juu, utafiti na teknolojia na kufanikisha malengo ya Chuo Kikuu cha Kiislamu kwa kusisitizia mambo yafuatayo:
3 - 1 - Kutilia umuhimu mfumo wa ufundishaji na malezi ya Kiislamu na asili ya malezi pambizoni mwa elimu na malezi na ustawishaji wa usalama wa kiafya, kiroho na kimaanawi wa watafiti wa masuala ya kielimu na kutia nguvu welewa na nishati zao za kisiasa.
3 - 2 - Kulea walimu na wanachuo wenye imani thabiti ya dini ya Kiislamu, waliojipamba kwa maadili yaliyo bora, wanaoheshimu na kutekeleza kivitendo sheria na mafundisho ya Kiislamu, watiifu kwa Mapinduzi ya Kiislamu na wenye uchungu na hamu kubwa ya kuistawisha nchi yao.
3 - 3 - Kulinda misingi ya Kiislamu na matukufu ya kiutamaduni na kijamii katika matumizi ya elimu na teknolojia.
4 - Kutia nguvu azma ya taifa na kuongeza welewa wa watu katika jamii kuhusu umuhimu wa ustawi wa kielimu na kiteknolojia kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
4 - 1 - Kutia nguvu na kustawisha fikra ya uzalishaji wa kielimu na harakati ya kutengeneza programu za kompyuta nchini.
4 - 2 - Kunyanyua moyo wa nishati ya matumaini, kujiamini, ubunifu wenye faida, ushujaa wa kielimu na kazi za watu wengi kwa pamoja na kufanya kazi kwa imani na kujitolea kikamilifu.
4 - 3 - Kuanzisha kozi za kubuni nadhari katika Vyuo Vikuu na kutia nguvu utamaduni wa kutafuta na kufanya kazi za elimu za kimsingi, kubadilishana na kugonganisha fikra na mawazo na kuweko uhuru wa fikra za kielimu nchini.
4 - 4 - Kunyanyua heshima ya walimu, wafanya uhakiki na watafiti wa kielimu na kuboresha maisha yao sambamba na kuwaandalia nafasi za kazi wanafunzi walioko masomoni.
4 - 5 - Kuhuisha historia ya kielimu na kiutamaduni ya Waislamu na ya Iran na kuchukua kigezo kutoka katika fakhari na shakhsia waliofanya mambo makubwa katika masuala ya kielimu na kiteknolojia.
4 - 6 - Kupanua wigo wa kuwaunga mkono kwa malengo maalumu ya kimaada na kimaanawi watu wenye vipaji na wavumbuzi na watu wanaojihusisha na masuala ya kielimu na kiteknolojia.
5 - Kuleta mabadiliko katika uhusiano baina ya mfumo wa elimu ya juu, utafiti na teknolojia na sekta nyinginezo kwa kusisitizia masuala yafuatayo:
5 - 1 - Kuongeza hisa ya elimu na teknolojia katika masuala ya uchumi na mapato ya taifa, kuzidisha uwezo wa kitaifa na kuongeza faida na manufaa yake.
5 - 2 - Kuunga mkono kimaada na kimaanawi suala la kubadilisha aidiolojia na kuifanya itekelezwe kivitendo na kuzaa matunda na kuongeza nafasi za uzalishaji wa bidhaa na huduma zinazotokana na elimu za kisasa na teknolojia za ndani ya nchi katika uzalishaji wa mali ghafi za ndani kwa lengo la kufikia hisa ya asilimia 50.
5 - 3 - Kutia nguvu na kuimarisha mfungamano wa karibu baina ya Hawza (Chuo Kikuu cha kidini) na Vyuo Vikuu (visivyo vya kidini) na kutia nguvu ushirikiano wa kudumu wa kiistratijia baina ya vyuo vikuu hivyo.
5 - 4 - Kuratibu uhusiano wa pande mbili baina yaa utafutaji elimu na kufanya kazi na kuainisha viwango na kozi za elimu na ramani kuu ya kielimu nchini na mahitaji ya uzalishaji na ufanyaji kazi.
5 - 5 - Kuainisha vipaumbele katika elimu na utafiti kwa kuzingatia sifa, uwezo na mahitaji ya nchi na mambo ya lazima ya kuweza kufikia kwenye nafasi ya kwanza ya kielimu na kiteknolojia katika eneo hili.
5 - 6 - Kuunga mkono umiliki wa kifikra na kimaanawi na kukamilisha miundombinu pamoja na sheria na kanuni zinazohusiana na suala hilo.
5 - 7 - Kuongeza nafasi na ushiriki wa sekta binafsi na zisizo za kiserikali katika masuala ya elimu na teknolojia na kunyanyua nafasi ya masuala ya wakfu na masuala ya kheri katika uga huo.
5 - 8 - Kustawisha na kutia nguvu kanali za mawasiliano ya kielimu za kitaifa na za nje ya taifa baina ya Vyuo Vikuu, vituo vya kielimu, wasomi, watafiti na taasisi za ustawi wa kiteknolojia na kiubunifu - za ndani na nje ya nchi - na kuimarisha ushirikiano katika viwango vya kiserikali na asasi za wananchi na kuzipa kipaumbele cha kwanza nchi za Kiislamu katika suala hilo.
6 - Kuzidisha ushirikiano na miamala amilifu, yenye faida na yenye kuleta ilhamu katika uga wa elimu na teknoloja baina ya Iran na nchi nyinginezo na taasisi za kielimu na kiufundi zenye itibari za kieneo na kimataifa hususan za ulimwengu wa Kiislamu sambamba na kutia nguvu uhuru wa nchi kwa kusisitizia masuala yafuatayo:
6 - 1 - Kutia nguvu viwanda na huduma zinazotokana na sayansi na teknoloja mpya na kuunga mkono uzalishaji na usafirishaji nje bidhaa za elimu za kimsingi na zinazotegemea teknolojia ya ndani ya nchi hususan katika nyuga zenye sifa na uwezo huo kwa kufanyia marekebisho mfumo wa uingizaji bidhaa kutoka nje na usafirishaji nje bidhaa.
6 - 2 - Kutilia umuhimu suala la kuhamisha teknolojia na kutafuta elimu ya ubunifu na utengenezaji wa vitu kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za ndani ya nchi na kwa kustafidi vizuri na soko la taifa katika utumiaji wa bidhaa zinazotoka nje.
6 - 3 - Kustafidi vizuri na uwezo wa kielimu na kiufundi wa Wairani waishio nje ya nchi na kuvutia wataalamu na watafiti wakubwa nchi nyinginezo hasa wa nchi za Kiislamu kulingana na mahitaji ya nchi.
6 - 4 - Kuibadilisha Iran kuwa kituo kikuu cha kuorodhesha na kuandikisha makala za kielimu na kuvutia matokeo ya utafiti mbali mbali wa watafiti pamoja na kuvutia watu wenye vipaji vya kielimu na wabunifu wa nchi nyinginezo hususan wa ulimwengu wa Kiislamu.

 
< Nyuma   Mbele >

^