Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe kwa Mnasaba wa Wiki ya Kujihami Kutakatifu na Siku ya Kuwaenzi Mashahidi Chapa
25/09/2014
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo (Alkhamisi) ametoa ujumbe kwa mnasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Kujihami Kutakatifu (ya kukumbuka wakati rais wa zamani wa Iraq alipoanzisha vita dhidi ya Iran) na maadhimisho ya siku ya kuwaenzi mashahidi na watu wanaojitolea katika njia ya haki na kusisitiza kuwa: Vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu taifa la Iran ni majimui na mjumuiko wa vitu vingi vinavyojenga utukufu wa taifa fulani na kwamba mashahidi na itikadi wa kufa shahidi katika njia ya haki ni kito adhimu kinachong'aa katika majimui hiyo ya kimiujiza na kito hicho kinaonekana kwa uwazi zaidi kati ya vitu vya mjumuiko huo.
Matini ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umesomwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Shahidi Mahallati, Mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) katika Taasisi ya Mashahidi na Masuala ya Watu Wanaojitolea katika Njia ya Haki. Amesoma ujumbe huo leo katika makaburi ya mashahidi kwenye eneo la Behesht Zahra mjini Tehran wakati wa kusafisha, kumwagia maua na na kutia marashi makaburi ya mashahidi. Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
 

Bismillahir Rahmanir Rahim
Vita vya miaka minane vya kujihami taifa la Iran ni majimui na mjumuiko wa vitu vingi vinavyojenga utukufu na kudhihirisha ujalili na ujamili ambao taifa fulani linaweza kuuonyesha katika maisha yake ya kihistoria. Lakini mashahidi na itikadi ya kufa shahidi katika njia ya haki ni kito kinachong'aa na chenye maajabu mengi ambacho katika mjumuiko huo wa kimiujiza kinaonekana kwa uwazi zaidi na ndicho kitu chenye thamani kubwa zaidi. Utukufu wa kito hicho unatokana na kujitolea muhanga katika njia ya haki kwa ikhlasi na utu, watu ambao wamesamehe masuala yao yote ya maisha ya kimaada na kufikiria tu radhi za Mwenyezi Mungu na kukabidhi masuala yao yote katika njia hiyo iliyojaa fakhari.
Familia za mashahidi, baba, mama, wake, watoto na jamaa wengine wa mashahidi nao kila mmoja wao ametoa mchango wake katika njia hiyo iliyojaa fakhari, heshima na umaanawi.
Amani ya Mwenyezi Mungu na salamu za malaika na waja wema ziwafikie watu hao waliofanya mambo makubwa katika jamii za wanadamu.

Sayyid Ali Khamenei,
3 Mehr 1393
(19 Mfunguo Pili 1435)
(25 Septemba 2014)

 
< Nyuma   Mbele >

^