Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Hukumu ya Kiongozi Muadhamu ya Kuanzisha Duru Mpya ya Kazi za Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni Chapa
19/10/2014
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika wakati huu wa kukaribia kuanza duru mpya ya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiiislamu ya Iran ametoa hukumu muhimu akisisitizia suala la kuwa na mikakati mizuri ya kukabiliana na changamoto za kiutamaduni kwa kutumia fursa na uwezo uliopo kikamilifu, kwa umakini wa hali ya juu, na kwa kuunganishwa pamoja nguvu za pande zote. Kama ambavyo amesisitizia pia wajibu wa kudhibiti vitisho na taathira mbaya zinazojitokeza, kwa hekima na kwa mantiki pamoja na kukabiliana kwa busara ya hali ya juu na mashambulizi ya kiutamaduni. Amesisitiza kuwa, hilo ndilo jukumu kuu la Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Vile vile ameongeza vipaumbele vingine saba vya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi ya huko nyuma na kuhakikisha yanafanikishwa haraka, kupambana kikweli kweli na kwa sura ya kiubunifu na suala la mirengo ya wafuasi wa utamaduni wa kimapinduzi na wa Kiislamu na wapinzani wake, kufuatilia kwa uzito wa hali ya juu maendeleo na kasi ya harakati ya kielimu na kiteknolojia pamoja na mabadiliko na kuingizwa mambo mapya ndani ya mfumo wa elimu na ufundishaji nchini hususan mabadiliko katika Sayansi ya Kijamii. Vile vile ameongeza wanachama na wajumbe wengine watatu wa kisheria katika majimui ya wajumbe wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu.
Matini kamili ya hukumu ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu suala hilo ni kama ifuatavyo:
 

Bismillahir Rahmanir Rahim
Falsafa ya kuweko Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni (la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) ni kufahamu, kubainisha, kuimarisha na kuokoa muundo wa kiutamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuitathmini upya mtawalia kambi ya utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu na msingi wa maendeleo ya kiutamaduni nchini yanayonasibiana na kuoana na hali halisi ilivyo nchini na ustahiki adhimu wa Iran ya Kiislamu na ya Kimapinduzi.
Kuwa na mikakati mizuri ya kuamiliana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika suala hilo kwa kutumia fursa na uwezo uliopo; kwa njia ya ukamilifu na kwa umakini wa hali ya juu na kwa ushirikiano wa watu wote na vile vile kudhibiti vitisho na taathira hasi kwa kuangalia mambo kwa jicho la hekima la uhalisia wa mambo na kukabiliana kibusara na wapinzani, wafanya mashambulizi ya kiutamaduni na maadui. Hayo ni miongoni mwa majukumu makuu ya baraza hilo. Nyuga za kimsingi na kuu kama vile uga wa kuzalisha elimu, uwanja wa mtindo wa maisha, elimu na utafiti, utamaduni wa umma na uhandisi wa kiutamaduni ni nyuga muhimu ambazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezikabidhi kwa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni kuziendesha na kuzisimamia.
Kutekeleza vilivyo Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni majukumu yake kama jina lake lilivyo ndilo sharti la kufanikiwa kwake katika majukumu yake ya hatari liliyokabidhiwa.
Kwa kuzingatia kumalizika kipindi kingine cha majukumu ya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu na katika kipindi hiki cha kukaribia kuanza kipindi kipya cha wajumbe wa baraza hilo, kama ilivyokuwa kwa duru iliyopita, duru hii pia ninawateuaa na kuwaongeza ndani ya baraza hilo wajumbe wapya ambao ni Makamu wa Rais katika masuala ya mipango na usimamiaji wa kiistratijia na Makamu wa Rais katika masuala ya wanawake na familia pamoja na mkuu wa ofisi ya tablighi ya Kiislamu kwa ajili ya kuhudumu katika baraza hilo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Ni wajibu kwangu kuwashukuru wajumbe wapendwa wa baraza lililopita na hususan katibu mpendwa na sekretarieti ya baraza hilo waliohudumu katika kipindi kilichopita na hapa chini ninaorodhesha masuala mbali mbali muhimu ambayo yanapaswa kuwa vipaumbele vya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Vipaumbele hivyo ni kama ifuatavyo:
1 - Pamoja na kuwepo jitihada mbali mbali nzuri za baraza hilo katika kutekeleza na kufuatilia vipaumbele vilivyowasilishwa katika miaka ya huko nyuma, lakini leo kipaumbele kikuu cha baraza hilo ni kufanikisha na kutekeleza kwa haraka na kiukamilifu; maamuzi na miswada inayopitishwa.
2 - Kwa kuzingatia kuundwa kambi kwa nguvu zote kati ya wafuasi wa utamaduni wa Kimapinduzi na Kiislamu na wapinzani wenye inadi waliodhamiriana kukabiliana kwa nguvu kubwa na kambi ya upande wa pili, Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni lina wajibu wa kufanya harakati na ubunifu wa kukabiliana kwa kina na kambi na mirengo hiyo iliyo wazi ya kiutamaduni ili wafuasi na wapenzi wa utamaduni wa kidini na kimapinduzi wa ndani na nje ya nchi waweze kushibisha kiu zao na wawe na utulivu wa moyo na wakati huo huo kuwatia wasiwasi na woga pamoja na kuwakatisha tamaa wapinzani wa utamaduni wa kidini na kimapinduzi.
3 - Kwa kuzingatia ukuaji mkubwa wa dhati na hima na kuweko mwamko mkubwa katika harakati za kiutamaduni ndani ya matabaka mbali mbali ya watu hususan kati ya vijana wenye imani thabiti ya dini na wanamapinduzi, taasisi za masuala ya kiutamaduni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na juu yao kabisa likiweko Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni, zinapaswa kutekeleza vizuri majukumu yao kiubunifu na kuwakamilishia na kuwasahilishia kazi pamoja na kuwapa ilhamu wanaharakati hao wanaojitokeza wenyewe na kwa hamu kubwa kushughulikia masuala ya utamaduni wa kidini na Kiislamu. Ni jukumu la taasisi hizo kuwaondolea vizuizi na vikwazo vyote wanaharakati hao.
4 - Kunyanyua kiidadi, kiubora na kiviwango matumaini na uzalishaji wa bidhaa za kiutamaduni hakuwezekani bila ya kuwekwa sera sahihi na kuweko ufuatiliaji wa kuendelea na kuingiza katika medani uwezo wote wa taifa katika uga huo. Kuangalia upya muundo wa harakati na usimamiaji wa masuala ya kiutamaduni kwa mtazamo na msimamo huo ndiko kunakoweza kudhamini mafanikio katika jukumu hilo zito la kihistoria. Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu linapaswa kuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kutumia uwezo wote wa suhula zote na vyanzo vya kibinadamu katika kufanikisha malengo yaliyokusudiwa katika masuala ya kiutamaduni kulingana na mazingira yaliyopo na kutathmini upya mambo na kuyafanya ya kisasa, kujipanga upya na kuzidi kufanya kazi kwa pamoja.
5 - Kufuatilia kwa uzito wa hali ya juu maendeleo na kasi kubwa ya harakati ya kielimu na kiteknolojia nchini, ni moja ya vipaumbele vikuu na vya kimsingi kabisa vya nchi ambavyo Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lina nafasi kubwa ndani yake. Alhamdulillah baada ya kupasishwa na kuwasilishwa Ramani Kuu ya Kielimu nchini, medani ya elimu na teknolojia imeweza kupata muongozo na ramani yake ya njia, suala hilo limepelekea kuundwa kamati maalumu ya kusimamia na kuongoza Ramani Kuu ya Njia, na kazi zimeanza katika uga huo na hadi hivi sasa zimefanikiwa kuleta taathira na matunda mazuri. Ni jambo la wajibu kuhakikisha kuwa jambo hilo linaendelea kupewa uzito mkubwa na hima zaidi hususan na viongozi wa wakuu wa Mihimili Mitatu Mikuu ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama) na hasa hasa Serikali. Kasi kubwa ya ustawi wa kielimu nchini haipasi kuruhusiwa kusita hata chembe kwa hali yoyote ile, bali inabidi kasi hiyo iwe kubwa zaidi, siku baada ya siku na Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni nalo inabidi itekeleze wajibu wake kiukamilifu na kwa hima ya hali ya juu katika kusimamia, kuwekea misingi mizuri na kuongoza vyema kazi hizo.
6 - Uhandisi wa masuala ya kiutamaduni na kadhia ya mabadiliko na kufanywa upya na wa kisasa zaidi mfumo wa masomo na elimu nchini, ni sawa tu iwe ni katika Elimu ya Juu au katika Wizara ya Elimu na Malezi, na pia mabadiliko katika masomo ya Sayansi ya Kijamii suala ambalo huko nyuma pia lilisisitiziwa kupeda umuhimu mkubwa na vipindi vilivyopita vya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni nchini, ni mambo ambayo hadi hivi sasa hayajafanikishwa. Kuendelea kuakhirishwa ufanikishaji wa mambo hayo kunayaleta hasara kubwa Mapinduzi ya Kiislamu. Hivyo inabidi masuala hayo yapewe uzito wa hali ya juu zaidi na njia za kufanikisha mambo hayo inabidi ziangaliwe upya na kuwekewa mipangilio mipya na wakati maalumu unaoingilika akilini kwa ajili ya kuyafanikisha.
7 - Kufanyika kwa mpangilio maalumu na kwa muda unaotakiwa vikao vya Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni la Jamhuri ya Kiislamu na kushiriki vilivyo na kufanya utafiti mkubwa wajumbe wa baraza hilo hususan wakuu wapendwa wa Mihimili Mitatu Mikuu ya dola katika vikao na mijadala ya baraza hilo na suala la wajumbe wa baraza hilo kutenga wakati wa kutosha na hima inayotakiwa kwa ajili ya mijadala na kazi za baraza hilo, ni kipaumbele kingine ambacho napenda kukisisitizia hapa.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu akupenda taufiki katika kazi zenu wapendwa na waheshimiwa nyote.

Sayyid Ali Khamenei
26/7/1393 (Hijria Shamsia)
(18/10/2014).

 
< Nyuma   Mbele >

^