Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Tanzia wa Kiongozi Muadhamu Kufuatia Kifo cha Ayatullah Mahdavi Kani Chapa
21/10/2014
 Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametoa ujumbe wa mkono wa pole kufuatia kufariki dunia Ayatullah Mahdavi Kani, Mkuu wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyefariki dunia Jumanne, Oktoba 21, 2014 akiwa na umri wa miaka 84.
Ujumbe wa Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ni kama ifuatavyo:

Bisimillahir Rahmanir Rahim

Nimeipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kufariki dunia mwanachuoni mwanaharakati na mchaji mungu, Ayatullah Bwana Alhaj Sheikh Muhammad-Reza Mahdavi Kani, (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) na kuzitia majonzi nyoyo za wapenzi na watu walio azizi kwake. Mwanachuoni huyo mkubwa ni miongoni mwa wanamapambano wa kwanza kabisa walioingia katika njia nzito ya Mapinduzi ya Kiislamu na ni mmoja wa shakhsia waliokuwa na taathira kubwa na wapenzi wakubwa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Aidha alikuwa miongoni mwa watu waaminifu, wenye ghera na wakweli kwa Imam wetu mtukufu (Imam Khomeini - quddisa sirruh) ambaye alikuwa katika medani zote muhimu nchini na katika kipindi cha mapinduzi; akipambana kiushujaa na alikuwa na misimamo ya wazi katika maisha yake. Wakati wote alidhihiri kwa sura na msimamo mmoja tangu wakati alipokuwa mjumbe katika Baraza la Mapinduzi na baadaye kuundwa kamati za Mapinduzi mwanzoni mwa kuasisiwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu hadi alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na baadaye kukubali kushika nafasi ya Waziri Mkuu katika vipindi vigumu sana vya Jamhuri ya Kiislamu na hadi alipoingia katika uga wa kuzalisha elimu na kulea vijana wema na kuasisi Chuo Kikuu cha Imam Sadiq AS na hadi alipoteuliwa kuwa Imam wa Sala ya Ijumaa na hatimaye kuwa mkuu wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu (wanaomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu). Katika hatua na sehemu zote hizo alidhihiri kwa sura na msimamo mmoja wa mwanachuo wa kidini, mwanasiasa mwaminifu na mkweli na mwanamapinduzi aliye muwazi. Kamwe hakuwa akimfanyia muhali mtu kwa kuzingatia nafasi yake na wala hakuruhusu masuala ya kimirengo na kikabila kuingia au kuathiri kazi zake ambazo kwa kweli ni kubwa na zenye taathira ya kupigiwa mfano. Alikuwa mwanachuoni mkubwa, mcha Mungu na alielekeza nguvu na hima yake yote katika makumi ya miaka yote hiyo kwenye kupigania haki na uhakika na katika kulinda njia na sira ya Mapinduzi ya Kiislamu na mfumo wa Jamhuri ya Kiisalmu na hakuzembea hata chembe kutekeleza wajibu wake. Rehema na Radhi za Allah ziwe pamoja naye.
Ninatumia fursa hii kutoa mkono wa pole kwa udhati wa moyo wangu kwa familia yake, kwa ndugu yake mpendwa, kwa wananchi wote wa Iran, kwa jamii ya watu wa dini nchini, kwa wapenzi na kwa wanafunzi wote na kila aliyepata malezi ya mwanachuoni huyo, nikimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amnyanyue daraja za juu mbele Yake.

Sayyid Ali Khamenei,
29/7/93 (Hijria Shamsia)
(21/10/2014).

 
< Nyuma   Mbele >

^