Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi MuadhamuAonana na Washiriki wa Kongamano la Nane la Kitaifa la Vijana wenye Vipawa Chapa
22/10/2014
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na mamia ya vijana wenye vipaji wa Vyuo Vikuu na walioteuliwa kushiriki katika mashindano ya Olympiad na matamasha ya kimataifa na ya ndani na huku akisisitizia udharura wa kuweko silisila kamili iliyoshikamana vyema pamoja na kanali kubwa ya kuzalisha elimu katika Vyuo Vikuu na kwenye vituo vya kielimu na kiutafiti nchini Iran ameongeza kuwa: Iran inapaswa kutumia vizuri vyanzo vyake ilivyo navyo juu ya ardhi yaani akili na vipaji vya vijana wake na watu wenye vipawa nchini kwa ajili ya kuimarisha uchumi wake na sio kutumia vyanzo vyake vyake vilivyo chini ya ardhi na ambavyo vina panda shuka nyingi kama vile mafuta na vyanzo vingine vya chini ya ardhi.
Amesema kuwa, vinamfurahisha na kumpendeza mno vikao ni mikutano yake na vijana wenye vipawa ambao wanatoa bishara ya mustakbali bora wa nchi na amewausia vijana hao waijenge nchi yao yenye fakhari nyingi kwa nguvu za kifikra na juhudi kubwa zilizopambwa kwa nia na azma ya kweli kwa namna ambayo itakuwa ni fakhari kwa taifa hili lenye historia kongwe ya kujivunia.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mwito kwa watu wote wenye vipaji kutafakari na kuangalia kwa kina suala la sifa ya asili ya mtu mwenye kipaji na maana yake ya kweli na kuongeza kwamba: Kuwa na kipaji ni majimui na ni mjumuiko ya sifa tatu maalumu; akili na kipaji, hima kubwa ya kutalii na kujifunza mambo mapya, kufanya kazi na jitihada zisizochoka na kuwa na subira na uvumilivu wa kupigiwa mfano katika ufuatiliaji wa kuendelea wa mambo na kwamba wakati mtu anapoziangalia kielimu na kihekima sifa hizo maalumu itambainikia wazi kuwa sifa zote hizo ni neema na ni riziki kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Aidha ametoa ushahidi wa aya ya Qur'ani Tukufu kuhusiana na upana wa maana ya riziki za Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa: Riziki ya kuwa na elimu na vipaji inabidi itumiwe na itolewe katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwafanyia wema waja wa Mwenyezi Mungu na itumike kwa ajili ya manufaa ya hivi sasa na ya mustakbali, ya jamii, taifa na nchi.
Ayatullah Udhma Khamenei amewakumbusha vijana wenye vipaji akiwaambia: Kama mtaitumia vizuri neema ya kuwa na vipaji mliyopewa na Mwenyezi Mungu basi mtapata pia uongofu kutoka kwa Allah yaani vipaji vyenu vitaongezeka na pia Mwenyezi Mungu atakuongozeni katika nyuga ambazo elimu na maarifa yenu yanahitajika kikweli kweli ndani yake.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja uwepo wenye taathira kubwa wa Shahid Chamran katika vita vya kujihami kutakatifu na kazi kubwa zilizofanywa na shahid Shahriyari katika upande wa nyuklia kuwa ni mifano ya wazi ya kutoa na kutumia vipaji kwa ajili ya jamii na nchi kama ambavyo pia hiyo ni mifano miwili mikubwa ya uongofu wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye vipaji.
Vile vile ameashiria maendeleo makubwa ya kielimu iliyopita Iran katika muongo mmoja uliopita na kwa mara nyingine amesisitiza kuwa kuendelea harakati yenye kasi kubwa ya ustawi wa kielimu chini ni mahitaji makuu na ya kweli ya Iran na kuongeza kuwa: Kama tulivyosisitiza katika hukumu tuliyotoa hivi karibuni kuhusiana na Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni, hakuna sababu wala jambo lolote linalopaswa kusimamisha harakati ya kielimu nchini kwani kusita kwa namna yoyote ile kunakwenda sambamba na kurudi nyuma.
Ayatullah Udhma Khamenei amekumbushia mashindano yaliyopo kimataifa na kasi kubwa ya mataifa na nchi za dunia katika kujiimarisha kielimu na kimaarifa na kuongeza kuwa: Licha ya kuwepo kasi kubwa ya maendeleo ya kielimu lakini kutokana na kubaki nyuma kukubwa (Iran kutokana na siasa mbovu za tawala za kitaghuti za kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu) kumepelekea hadi hivi sasa Iran kushindwa kufikia katika daraja inayostahiki kuwa nayo licha ya kufanyika jitihada kubwa mno za kuziba pengo hilo. Hivyo kuna ulazima wa kuendelea harakati ya kielimu kwa kutumia mbinu na njia zote ikiwemo kuimarishwa na kutiwa nguvu mashirika ya elimu msingi na ya uchumi unaotokana na elimu.
Amesema, wokovu wa nchi na mustakbali bora wa taifa la Iran umo ndani ya uimara wa kielimu na kuongeza kuwa: Kama alivyosema Mkuu wa Taasisi ya Watu wenye Vipaji, na kwa hakika amesema kweli kwamba uchumi unaogemea kwenye vyanzo vya chini ya ardhi, huwa ndani yake hakuhisiki haja yoyote ya kutafutwa, kushirikishwa au kuvutiwa kazi za watu wenye vipaji, na kamwe nchi haiwezi kupata maendeleo ya kweli kwa kutumia uchumi wa namna hiyo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, kuendesha nchi kwa kutegemea kuuza maliasili ya chini ya ardhi kuwa kunafanana na maisha ya mtoto aliyerithi utajiri kutoka kwa wazee wake na kuongeza kuwa: Mtoto anayeishi kwa mali ya kurithi hajui thamani ya fedha na tabu zilizopatikana wakati wa kuchuma mali hiyo hivyo anaitumia kwa fujo na ubadhirifu, hali ni hiyo hiyo wakati nchi inapoongozwa kwa msingi wa kutegemea fedha zitokanazo na kuuza mafuta ghafi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kuegemeza mipango ya uchumi wa nchi kwenye mapato yatokanayo na kuuza mafuta kuwa ni kuutia uchumi wa Iran mikononi mwa wapangaji wakuu wa siasa za dunia na huku akiashiria kuyumba na panda shuka nyingi zinazoonekana katika bei ya kimataifa ya mafuta amesema: Nchi ambayo inapanga mipango yake ya kiuchumi kwa kutegemea jambo hilo, mwisho wake (mbaya) uko wazi.
Ayatullah Udhma Khamenei ametoa mifano ya matukio ya kweli yaliyotokea kuhusu suala hilo akisisitiza kuwa: Iran inapaswa kutegemea nguvu zake za ndani na hazina zake za juu ya ardhi yaani akili na vipaji vya vijana wake katika kuzalisha elimu na maarifa badala ya kutegemea mapato yatokanayo na uuzaji mafuta nje na kwamba ni kwa njia hiyo ndipo madola makubwa ya dunia hayataweza kuuchezea uchumi wa Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia udharura wa kutofautisha baina ya uzalishaji wa elimu na uzalishaji wa makala na kuongeza kuwa: Tab'an uzalishaji wa makali ambazo zinakuwa ni marejeo yenye thamani ya kielimu ni jambo zuri, lakini kazi haipaswi kuachiwa kuishia hapo.
Ameusia kuwa: Makala za kielimu zinazozalishwa zinapaswa zizalishe ubunifu wa kivitendo na zizingatie mahitaji halisi ya ndani ya nchi.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kufanya jitihada za kuliletea taifa maendeleo ya kielimu kuwa ni jukumu la taasisi na wizara zote nchini na kuongeza kwamba: Ramani kuu ya kielimu nchini Iran inaweza kuainisha majukumu ya kila taasisi katika suala hilo.
Akitoa muhtasari wa hotuba yake kuhusu suala hilo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Inabidi kutumiwe jitihada na mipango iliyowekwa kwa ajili ya taasisi zote ili kuunda silisila kamili na kanali adhimu wa uzalishaji elimu nchini ambapo kwa kutumia njia hiyo, taasisi na sekta zote zitaweza kukamilishana na kuongezeana nguvu.
Aidha amewausia vijana wenye vipawa kuimarisha uhusiano na ukuruba wao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwakhutubu vijana hao akiwaambia: Nyoyo zenu safi na zenye nuru nyinyi vijana ni fursa yenye thamani kubwa ya kuweza kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kuongezeka neema Zake kwenu.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesifu hotuba nzuri mno ya Dk Sattari, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Masuala ya Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Watu wenye Vipawa na kuongeza kuwa: Baba yake Dk Sattari ambaye ameuawa shahidi, naye sambamba na kuwa na vipaji vikubwa vya kiakili, kifikra na kioperesheni, kwa hakika alikuwa na kipaji kikubwa pia suala zima la kuainisha malengo, nia, azma na kuingia kwenye medani ngumu na nzito.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Dk Sattari, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Masuala ya Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Watu wenye Vipawa ametoa hotuba fupi na ndani yake amelitaja suala la kuwa na imani, kujiamini, ikhlasi, kujitolea vilivyo katika njia ya haki na kuipenda nchi na taifa kuwa ni miongoni mwa sifa kuu za watu wenye vipawa nchini Iran na kuongeza kuwa: Watu wenye vipaji wanatambua kuwa wana deni kubwa kwa nchi yao iliyotoa gharama kubwa kwa ajili yao, na kwamba mtu mwenye kipaji ni yule ambaye yuko tayari kutoa sehemu kubwa ya alicho nacho kwa ajili ya kutumikia watu na nchi yake.
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Watu wenye Vipawa nchini Iran amesema kuwa, lengo kuu la taasisi hiyo ni kuwawezesha na kuwarahishia kazi watu wenye vipaji nchini na huku akiashiria ulazima wa kufanyiwa marekebisho baadhi ya mbinu za kukuza na kustawisha uchumi zinazotumiwa nchini Iran amesema: Katika uchumi wa mafuta ambao msingi wake wa kuzalisha utajiri unategemea kuuza mafuta ghafi, maliasili za chini ya ardhi na madini, uchumi wa namna hiyo hauwezi kuzalisha na kulea watu wenye vipaji.
Makamu huyo wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya Sayansi na Teknolojia amebainisha pia kuwa, watu wenye vipaji nchini wanaweza kubadilisha haraka mno mwelekeo wa uchumi wa nchi na kuongeza kwamba: Muelekeo wa uchumi wa nchi unapaswa uende upande wa uchumi wa kutegemea elimu za kimsingi na jambo hilo haliwezekani ila kwa ubunifu na kufanyika jitihada kubwa zisizosita.
Bw. Sattari ametaja baadhi ya kazi zilizofanywa na taasisi ya watu wenye vipawa ya nchini Iran kuwa ni pamoja na kufanyia marekebisho hati za taasisi hiyo, kuongezeka mara nne watu waliosajiliwa katika taasisi hiyo katika mwezi wa Mehr mwaka huu wa Kiirani wa Hijria Shamsia, kuendesha mpango wa "Shahab" kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na malezi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kufanya marekebisho ya kimsingi katika masuala ya utamaduni ya taasisi ya taifa ya watu wenye vipawa nchini, kutumia vizuri fursa ya Wairani walioko nje ya nchi pamoja na kuweka ratiba na mipangilio mizuri kwa ajili ya kulea na kuzalisha wasomi katika masuala na nyuga zinazohitajika nchini.
 
< Nyuma   Mbele >

^