Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kuteuliwa Bw.Sarafraz kuwa Mkuu Mpya wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu Chapa
08/11/2014
İran Radyo-Televizyon Kurumu Başkanlığına Muhammed Serefraz GetirildiAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa hukumu ambayo ndani yake amemshukuru Mhandisi Izzatullah Zarghami, kutokana na jitihada zake kubwa mno na uchapaji kazi wake usiojua kuchoka na ambao alikuwa akiufanya kwa mapenzi makubwa ya moyoni wakati alipokuwa Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na amemteua Bw. Mohammad Sarafraz kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika hukumu yake hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria jukumu la kihistoria la shirika hilo la utangazaji la taifa katika kulinda na kuimarisha uhuru wa kiutamaduni na utambulisho wa Mapinduzi ya Iran ya Kiislamu na kusisitiza kwamba: Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambalo lina jukumu la hatari mno la kuongoza na kusimamia utamaduni wa taifa na kutoa miongozo kwa fikra za walio wengi katika jamii, ni sawa na Chuo Kikuu cha watu wote. Amesema, shirika hilo lina jukumu la kutangaza dini, maadili bora, kueneza matumaini na elimu na maarifa pamoja na pia kueneza mtindo wa maisha wa Kiislamu - Kiirani kati ya matabaka mbali mbali ya wananchi. Amesema, shirika hilo ambalo ni mfano wa injini ya kutia nguvu na hamasa katika maendeleo ya nchi, lina jukumu la kulisaidia kwa pande zote na kiubunifu; suala zima la kujitolea watu wote katika taifa la Iran na vile vile kusaidia viongozi watendaji katika kudhamini na kufanikisha malengo na utekelezaji wa siasa kuu za Jamhuri ya Kiislamu pamoja na ufanikishaji wa malengo makuu ya nchi.
Matini kamili ya hukumu hiyo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Janab Bwana Muhammad Sarafraz (daama taufiquh)
Baada ya kumalizika kipindi cha kazi za Janab Bwana Mhandisi Sayyid Izzatullah Zarghami (Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB), aliyemaliza muda wake) ambaye alitekeleza jukumu lake kwa jitihada kubwa, zisizochoka na kwa mapenzi makubwa na ubunifu, ninakuteua kuwa mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kutokana na ustahiki ulio nao na kwa kuzingatia welewa na uzoefu wako mkubwa wa uongozi ambao umekuwa nao kwa muda mrefu katika shirika hilo la taifa la utangazaji na welewa wako mkubwa na wa kina kuhusiana na majimui hiyo kubwa na muhimu.
Shirika la Sauti na Televisheni (la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) ambalo lina jukumu la hatari la kuongoza na kusimamia masuala ya utamaduni na fikra za walio wengi katika jamii, ni sawa na Chuo Kikuu cha watu wote. Shirika hilo ambalo kwa kuzingatia harakati mbali mbali na mipangilio yake tofauti yenye utaalamu mkubwa, ya maendeleo na ya kina ya kiutangazaji, vile vile lina jukumu kueneza dini na maadili bora na matumaini na maarifa na kueneza mtindo wa maisha wa Kiislamu - Kiirani kati ya matabaka mbali mbali ya wananchi.
Jukumu la kihistoria la chombo hicho cha habari cha taifa katika kipindi cha hivi sasa ni kulinda na kutia nguvu uhuru wa kiutamaduni na utambulisho wa Iran ya Kiislamu. Azma ya kitaifa na hamasa ya kimaanawi na nishati ya kimapinduzi ya matabaka mbali mbali ya jamii katika njia ya kufanikisha malengo makuu ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni mambo ambayo yanaweza kupatikana tu kwa wananchi kuwa na welewa na maarifa ya kina na makubwa kama ambavyo aidha watu wananahitajia pia kuwa na mfungamano wa kina na wa karibu na chemchemu za kuzalisha fikra asili za kidini na wimbi la wapenzi na maashiki wenye mapenzi makubwa na ya kweli wa Mapinduzi ya Kiislamu. Shirika la Sauti na Televisheni (la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) ni mithili ya injini ya kuendesha na kutia nguvu maendeleo ya nchi na ina jukumu la kuunga mkono - kwa pande zote na kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu pamoja na kwa kuzingatia nafasi yake muhimu ya upashaji habari na utangazaji - suala zima la kuwafanya watu wote ndani ya taifa la Iran washiriki katika ufanikishaji wa jambo hilo muhimu na vile vile kuwasaidia viongozi watendaji katika kufanikisha malengo yaliyokusudiwa na katika utekelezaji wa siasa kuu za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na pia katika ufanikishaji wa vipengee vya hati ya kuainisha malengo ya muda mrefu ya nchi. Pamoja na hukumu hii, kumeambatanishwa stratijia muhimu zaidi ambazo Inshaallah zitaweza kulisaidia shirika la utangazaji la taifa kutekeleza na kufanikisha jukumu lake hilo kubwa.
Mwisho ni wajibu kwangu kumshukuru kwa dhati, Janab Bwana Mhandisi Zarghami na wafanyakazi wenzake ambao wote kwa pamoja wameweza kuleta maendeleo makubwa ndani ya Shirika la Utangazaji la Taifa (IRIB) katika kipindi cha uongozi wao nikimuomba Mwenyezi Mungu awape taufiki ya kuweza kuendelea kutoa michango yao kwenye nyuga tofauti za kisiasa, kijamii na kiutamaduni.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mpaji, akupe taufiki Janab (Bwana Mohammad Sarafraz) ambaye umepata fakhari ya kwamba unatoka kwenye familia ya mashahidi watukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu; taufiki ambayo itakuwezesha kutekeleza vilivyo jukumu lako la hatari na nyeti mno kwa kutawakali na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu. Dua hiyo ninakuombea wewe na wafanyakazi wenzako wote wapendwa.

Sayyid Ali Khamenei
15 Aban 1393 (Hijria Shamsia)
(6 Novemba, 2014 Milaadia).

 
< Nyuma   Mbele >

^