Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Nouri al Maliki, Makamu wa Rais wa Iraq Chapa
10/11/2014
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na Bw. Nouri al Maliki, Makamu wa Rais wa Iraq na sambamba na kusifu ushujaa, uwezo na uongozi mzuri wa Bw. al Maliki wakati alipokuwa Waziri Mkuu wa Iraq na kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwa ajili ya kuleta utulivu, uhuru na maendeleo ya taifa la Iraq amemkhutubu Bw. al Maliki akimwambia: Umefanya kazi kubwa na ya busara ya hali ya juu wakati wa makabidhiano ya madaraka huko Iraq na kazi yako hiyo kamwe haiwezi kusahaulika katika historia ya Iraq.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia namna Bwana Nouri al Maliki alivyo na utambuzi wa kina na mzuri kuhusiana na masuala na matatizo ya Iraq na kuongeza kuwa: Msimamo wako kuhusu kuisaidia serikali mpya ya Bw. Haider al Abadi na juhudi kusaidia za kuleta umoja kati ya taasisi mbali mbali za Iraq ni jambo zuri mno na inabidi liendelee.
Katika mazungumzo hayo, Bw. Nouri al Maliki, Makamu wa Rais wa Iraq sambamba na kuelezea kufurahishwa kwake sana na kupata fursa ya kuonana tena na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada mkubwa zaidi kwa serikali na wananchi wa Iraq katika kupambana na magaidi na vibaraka wa kigeni.
 
< Nyuma   Mbele >

^