Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Kikao cha Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanachuo wa Barani Ulaya Chapa
23/01/2015
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma risala kwa kikao cha arubaini na tisa kikuu cha Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya barani Ulaya na kusisitiza kuwa, kutafuta elimu kwa nia ya kuwa na fikra bora, yote mawili yanapopambwa kwa ucha Mungu na usafi wa nafsi, yanaifanya nchi kupata kinga kutokana na kuwa na utajiri wa uwepo wa vijana kama hao na kuiweka salama mbele ya kila tatizo.
Ujumbe huo umesomwa katika Msikiti wa Kabud (Blue Mosque) huko Yerevan, mji mkuu wa Armenia na Hujjatul Islam Walmuslimin Javad Ejei, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya wanachuo wa barani Ulaya. Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
 

Bismillahir Rahmanir Rahim
Vijana! Wapendwa!
Kuwepo kwenu kwenye vituo vya Vyuo Vikuu vya nchi mbali mbali ni fursa nzuri sana ya kukuwezesheni kuwa na muono mpana uliojaa hekima na maarifa kuhusiana na matukio mbali mbali yanayojiri duniani. Jambo hilo linatoa fursa ya kupata Iran wasomi walioiona dunia na wanaouelewa vizuri ulimwengu. Mnapaswa kuthamini sana fursa hiyo.
Mghafala una madhara makubwa kwa kiwango kile kile cha kutojali mambo. Leo hii mnapaswa kulipa umuhimu wa aina yake na wa kipekee swali kwamba, kwa nini siasa za Magharibi zinalishikilia na kuling'ang'ania suala la kueneza chuki na woga kuhusu Uislamu? Mnapaswa kulipa umuhimu mkubwa suala la kuangalia na kuona ni kitu gani chenye nguvu katika Uislamu wa kisiasa kwa mtazamo wa Iran ambacho madola ya kibeberu yenye chuki, yaliyo vamizi na yanayopenda kutawala mataifa mengine, yanakabiliana nacho kwa nguvu zao zote?
Tafuteni elimu kwa nia ya kupanua maarifa na elimu yenu na yote hayo mawili yafanyeni kwa kutanguliza uchaji Mungu na kuziweka safi nafsi zenu. Mtakapofanya hivyo basi hakutakuwa na jambo lolote litakaloweza kuiletea matatizo nchi ambayo ina utajiri wa kuwepo vijana kama nyinyi.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu akusaidieni na akupeni taufiki katika juhudi zenu.

Sayyid Ali Khamenei,
3/11/1393 (Hijria Shamsia)
Januari 23, 2015

 

 
< Nyuma   Mbele >

^