Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina Chapa
26/01/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonana na Bw. Ahmad Jibril, Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (Komandi Kuu) na kuitaja kadhia ya Palestina kuwa ndilo suala muhimu zaidi la ulimwengu wa Kiislamu na kusisitiza kwamba: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama kidete katika kulinda na kupigania malengo matukufu ya Palestina hadi yatakapozaa matunda na kwamba si jambo lililo na shaka hata chembe kwamba kuna siku vijana watanayaona kwa macho yao matunda hayo.
Ayatullah Udhma Khamenei amempongeza Bw. Ahmad Jibril kwa kazi na juhudi zake kubwa za kupigania ufanikishaji wa malengo matukufu ya Palestina na amemkhutubu Bw. Jibril akimwambia: Kwa yakini hivi sasa wewe ni moja ya misingi na nguzo kubwa za kadhia ya Palestina na ni matumaini yetu kwamba utaendelea kuwa na moyo huo huo wa muqawaman hadi utakapopatikana ushindi kamili.
Kwa upande wake, Bw. Ahmad Jibril ameelezea kufurahishwa kwake na kupata fursa ya kuonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Mapinduzi ya Kiislamu yameifanya Iran kuwa nchi yenye taathira katika nyuga za kimataifa na amemkhutubu Kiongozi Muaedhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akimwambia: Maendeleo makubwa iliyo nayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa yamepatikana chini ya kivuli cha busara na heshima zako kubwa.
Vile vile ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa misimamo yake thabiti na isiyotetereka ya kupigania haki za taifa la Palestina.
 
< Nyuma   Mbele >

^