Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Mkutano wa Kiongozi Muadhamu na Wajumbe wa Kamati za Makongamano Matatu ya Mashahidi Chapa
26/02/2015
 Miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na wajumbe wa kamati za Kongamano la Mashahidi wa Masuala ya Malezi, Kongamano la Mashahidi wa Wanachuo na Kongamano la Mashahidi Wasanii, imesambazwa leo asubuhi katika Kongamano la Mashahidi wa Masuala ya Malezi lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mnara wa Milad, jijini Tehran. Mkutano wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wajumbe wa kamati hizo ulifanyika tarehe 16 Februari 2015.
Katika mkutano huo wa Februari 16, 2015, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei alikutaja kujitokeza inavyopasa watu wenye vipaji mbali mbali wakati wa vita vya kujihami kutakatifu (vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa wakati huo wa Iraq dhidi ya utawala mchanga wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na dhidi ya taifa la Iran) ni jambo lililothibitisha ukubwa na namna iliyokuwa imeenea na kujikita sana fikra na moyo wa kujitolea muhanga na kuuawa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya matabaka mbali mbali ya jamii ya Iran na huku akisisitizia udharua wa kuenziwa mashahidi na kuzuia kusahauliwa au kutopewa umuhimu kumbukumbu hizo zenye thamani kubwa amesema: Kwa hakika "Majalis" na mikutano ya kuwaenzi mashahidi ni harakati ya kijihadi na "ya kishahidi" na kwamba kumbukumbu za mashahidi na sira na mienendo yao mema ni lazima ipewe umuhimu zaidi na zaidi katika jamii kadiri siku zinavyosonga mbele.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aligusia nafasi muhimu na ya kimsingi ya kujitolea kuuawa shahidi Imam Husain AS katika njia ya Allah na namna harakati yake hiyo tukufu ilivyodumu na kuendelea kutoa taathira njema hadi leo hii katika kuulinda Uislamu, Qur'ani na mafundisho matukufu ya Kiislamu na kuongeza kwamba: Wakati kumbukumbu za mashahidi na fikra ya kuwa tayari kujitolea kufa shahidi zinapopewa umuhimu na kufanywa kuwa uhakika wa kudumu katika jamii, huwa ni jambo lisilo na nafasi kabisa kushindwa jamii hiyo katika mitihani yoyote ile na kwamba taifa lililojengeka kwenye fikra hiyo litazidi kupiga hatua katika njia yake ya maendeleo bila ya hofu wala kuhuzunika.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake hiyo aliyoitoa Februari 16, 2015, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliitaja kazi kubwa iliyofanywa na taifa la Iran kuwa ni kubatilisha mgao ghalati na usio sahihi waliotwishwa walimwengu yaani mgao wa kundi la madola ya kibeberu na kundi la mataifa yanayopasa kufanyiwa ubeberu na kuongeza kuwa: Ijapokuwa leo hii waistikbari na mabeberu duniani wana nyenzo na suhula nyingi za kuzidi kuyafanyia ubeberu mataifa ya manyonge na madhulumina duniani, lakini katika mkabala wa madola hayo kuna utambulisho unaojulikana kwa jina la Mapinduzi ya Kiislamu ambao umesimama juu ya misingi ya mafundisho matukufu ya Mwenyezi Mungu na maadili bora pamoja na kusimama kishujaa mbele ya mfumo wa kibeberu duniani.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile ameashiria harakati inayozidi kupata nguvu ya Mapinduzi ya Kiislamu kuelekea kwenye vilele vya juu vya mafanikio na maendeleo na katika upande wa pili kuzidi kufeli njama za maadui wanaofanya kila njia ili kuikwamisha harakati hiyo na kuongeza kuwa: Kuna baadhi ya watu wakati wa vita vya kujihami kutakatifu walikuwa wanaamini kwamba kuruhusiwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kwenda kwenye medani ya vita kungelivifanya vyuo hivyo vikose wanafunzi na kwamba harakati ya kielimu nchini ingelikumbwa na matatizo, lakini imebainika kuwa, baraka za fikra ya jihadi na kujitolea kufa shahidi katika njia ya Allah ni nyingi sana na kwamba jitihada na juhudi hizo kubwa za kwenye medani ya vita ndizo zilizopelekea leo hii kushuhudiwa fakhari kubwa zaidi za maendeleo ya kielimu nchini Iran ambapo maendeleo katika uwanja huo ni makubwa zaidi kuliko katika sekta nyinginezo nchini.
Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kubakisha hai jina la mashahidi na utamaduni wa kujitolea kufa shahidi katika njia ya Allah kuwa ni muhimu mno na kwamba ni moja ya mambo ya kimsingi nchini Iran.
Ameongeza kuwa: Utamaduni wa kujitolea kufa shahidi una maana ya kujitolea muhanga kwa ajili ya kufanikisha malengo makuu ya pamoja na ya muda mrefu ya wananchi na ya wanadamu wote na kwamba utamaduni huo umesimama kikamilifu dhidi ya utamaduni wa Kimagharibi wa ubinafsi na kila mtu kuzingatia maslahi yake kwanza kabla ya maslahi mengine na utamaduni wa kupiga mahesabu yote kwa kuzingatia nini mtu atanufaika kimaada na jambo analofanya.
Mwishoni mwa hotuba yake hiyo Ayatullah Udhma Khamenei alisisitiza kuwa: Utamaduni wa kujitolea muhanga na kufa shahidi kila unapokuwa mkubwa na kuenea katika nukta zote za jamii ndivyo jamii hivyo inavyozidi kupiga hatua za kimaendeleo na kwamba ni ndoto kwa jamii hiyo kukwama na kubaki nyuma kimaendeleo.
 
< Nyuma   Mbele >

^