Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi MuadhamuAonana na Maafisa wa Mazingira, Maliasili na Maeneo ya Kijani Kibichi Chapa
08/03/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumapili) ameonana na maafisa na wasimamiaji wa masuala ya maliasili na kulinda mazingira na kulitaja suala la kukabiliana na matatizo ya mazingira kama vile uchafuzi wa hali ya hewa, kuenea vumbi na kuvamiwa misitu na maeneo ya malisho ya wanyama pamoja na maeneo ya kijani kibichi kuwa kunahitajia mipango, tadibiri na ufuatailiaji mtawalia wa mambo wenye uzito wa hali ya juu na hatua kali za vyombo husika. Amesisitiza kuwa: Kulindwa mazingira ni jukumu la kiutawala ambapo inabidi kuandaliwe hati ya kitaifa ya kulindwa mazingira na kuingizwa na kupewa umuhimu suala la kulinda mazingira katika miradi yote ya maendeleo ya kiujenzi na kiviwanda nchini pamoja na kuhesabiwa kuwa ni uhalifu kuharibu mazingira. Amesema inabidi mambo hayo yatekelezwe kivitendo kama njia ya kufanikisha jukumu hilo muhimu sana.
Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia mtazamo wa Uislamu kuhusiana na umuhimu wa kutunza na kulinda ardhi na utajiri wa umma wa sayari ya dunia na kusema: Uislamu na dini za Mwenyezi Mungu zinasisitizia mno wajibu wa kila mwanadamu kuhisi ni jukumu lake kutunza mazingira na kulinda mlingano baina ya mwanadamu na mazingira kwani sababu kuu za kuzuka matatizo katika mazingira ni kuharibiwa na kutochungwa mlingano huo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameitaja changamoto ya mazingira kuwa ni changamoto inayowahusu watu wote na ni ya kila kona ya dunia na huku akiashiria taathira za muda mrefu za masuala ya mazingira amesema: Uzoefu unaoshuhudiwa katika nchi mbali mbali duniani unathibitisha kwamba sehemu kubwa sana ya matatizo ya mazingira inaweza kuepukwa na ina utatuzi wake.
Ametoa mfano kuhusu suala hilo kwa kutaja uchafuzi wa hali ya hewa kwenye miji mikubwa na suala zima la kuenea vumbi katika baadhi ya maeneo akisisitiza kwamba: Masuala kama hayo yanaweza kutatuliwa kwa subira, uvumilivu, tadibiri na ufuatiliaji unaotakiwa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kadhia ya kulindwa mazingira, si suala linaloihusu serikali hii au ile na wala si suala la mtu huyu au mtu yule kama ambavyo pia si suala la mrengo huu au mrengo ule, bali ni suala linalohusu nchi na taifa zima ambalo kila mmoja ana wajibu wa kushiriki katika jitihada za utatuzi wa matatizo yanayohusiana na suala hilo.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyataja maji, hewa na udongo kuwa ni vitu vitatu vikuu vinavyounda mazingira na kusema: Katika utatuzi wa masuala kama vile uchafuzi wa hali ya hewa katika miji mikubwa, suala la kuenea vumbi katika baadhi ya maeneo pamoja na upungufu wa maji na mmomonyoko wa udongo, kunapaswa kutumike njia za kivitendo na kufanyike jitihada za kweli na za kuendelea, kabla ya kutumia propaganda kukabiliana na matatizo hayo.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia misitu na maeneo ya malisho ya wanyama akiyataja maeneo hayo kuwa ni sawa na mapafu ya kupumulia miji ya watu na ni sababu za kutunzika ardhi na udogo na kuelezea kusikitishwa kwake mno ni vitendo vya baadhi ya watu wanaopenda kujinufaisha binafsi vya kuvamia misitu na maliasili za nchi hususan kaskazini mwa Iran na kuongeza kuwa: Vyombo vinavyohusika vinapaswa kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaovamia misitu kwa madai yoyote yale hata kwa madai ya kujenga mahoteli na kuvutia watalii au kujenga Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) au kwa madai mengine yoyote ambayo kidhahiri yanaonekana yanakubalika.
Aidha amelitaja tatizo la kupora ardhi na tatizo jingine lililozuka hivi sasa la kupora milima na kujenga majumba kwenye maeneo ya milimani kuwa ni suala jingine linalohuzunisha na kusononesha nyoyo na kusisitiza kwamba: Inabidi sheria ziyataje masuala kama hayo kuwa ni uhalifu na watu wanaotumia vibaya maeneo hayo wafuatiliwe kisheria bila ya kuwaonea haya na kama itaonekana kuna uzembe umefanyika katika baadhi ya vyombo husika, inabidi waliofanya uzembe huo nao wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kwamba kulinda na kutunza mazingira ni wajibu na ni jukumu la kiutawala na kuongeza kwamba: Kuandaa hati ya kitaifa ya kutunza mazingira, kuingizwa suala la mazingira katika miradi yote ya maendeleo ya kiujenzi, kiviwanda, kibiashara, ya uchimbaji na usafishaji mafuta pamoja na kuangaliwa upya sheria zinazohusiana na kuharibu na kutoheshimu mazingira na vile vile kutiwa nguvu kazi za usimamiaji usio na uzembe wala muhali wa sheria hizo ni miongoni mwa njia muhimu zaidi za kuweza kulinda mazingira na kukabiliana na watu wasioheshimu sheria na wanaopenda kujinufaisha binafsi.
Ayatullah Udhma Khamenei ameitaja nafasi ya wananchi katika suala zima la kutunza na kulinda mazingira na suala zima la kueneza utamaduni wa kulinda mazingira katika jamii kupitia vyombo vya habari kuwa ni miongoni mwa hatua muhimu zinazopasa kuchukuliwa na kusisitiza kuwa: Mambo ambayo yalipaswa kusemwa, tayari leo yameshasemwa, kilichobakia kuanzia sasa ni kwamba wananchi wenyewe wakae na kufuatilia kwa kina ili kuona ni vyombo gani vimeshindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yao kuhusiana na kulinda mazingira na vyombo gani vimechukua hatua zinazotakiwa na kufanya jitihada zinanazostahili kufanywa katika kutunza mazingira.
 
< Nyuma   Mbele >

^