Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Makamanda na Maafisa wa Jeshi la Iran Waonana na Amirijeshi Mkuu Chapa
19/04/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumapili) ameonana na majimui ya makamanda, maafisa na familia za mashahidi wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuvitaka vikosi vya ulinzi vya Iran kulinda uimara wao, muono wao wa mbali na misimamo ya kidini na kimapinduzi sambamba na kuongeza uwezo wao wa kiulinzi, kisilaha na kuwa tayari wakati wote kiroho na kisaikolojia na kusisitiza kwamba: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haijawahi kuwa tishio kwa usalama wa eneo la Mashariki ya Kati wala kwa nchi jirani na katika siku za usoni pia katu haitokuwa tishio kwao lakini itaendelea kusimama kidete na kupambana vilivyo na uchokozi wa aina yoyote ile dhidi yake.
Katika mkutano huo ambao umefanyika sambamba na maadhimisho ya Siku ya Jeshi nchini Iran, Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa siku hiyo na kuutaja uamuzi wa kutangazwa tarehe 29 Farvardin (mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia sawa na Aprili 18) kuwa Siku ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulikuwa ni ubunifu mkubwa wa Imam Khomeini (Rahimahullah) mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran kwa ajili ya kukabilia na juhudi za baadhi ya mirengo za kutaka kuliangamiza jeshi hilo na kuongeza kuwa: Kwa werevu na muono wa mbali wa Imam wetu mtukufu (Rahimahullah), jeshi limeendelea kuwepo na kuwa imara na lenye nguvu kubwa na ni moja ya majimui ya kimapinduzi ambayo ilitoa mchango mkubwa sana katika nyuga tofauti kikiwemo kipindi cha miaka minane ya kujihami kutakatifu (miaka minane ya vita vilivyoanzishwa na utawala wa wakati huo wa Iraq dhidi ya utawala mchanga wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) na kuiletea nchi fakhari na hamasa kubwa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa, Farvardin 29 (Aprili 18) ina maana ya kusimama jeshi kwenye msingi wa Mapinduzi na katika njia ya kutumikia malengo ya wananchi na kuongeza kuwa, moja ya sifa za kipekee za jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ni kushikamana na sheria na misingi ya kidini.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia namna majeshi mengi duniani yasivyoheshimu sheria za kimataifa wala misingi ya kibinadamu wakati yanapopata ushindi au yanaposhindwa na kuongeza kuwa: Mfano wa wazi wa suala hilo ni mambo yanayofanywa na madola ya kibeberu duniani hususan Marekani ambayo hayachungi sheria zozote za kimataifa wala misingi yoyote ya kibinadamu, bali yanafanya kila aina ya jinai.
Vile vile amesema kuwa, matukio ya Yemen, vita vya Ghaza na vita vya Lebanon ni mifano ya wazi ya namna majeshi ya madola ya kibeberu yasivyoheshimu sheria za kimataifa na kusisitiza kuwa: Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima vimekuwa vikishikamana na sheria za kimataifa na kamwe havijawahi kukanyaga sheria za kimataifa iwe ni wakati wa kupata ushindi au wakati wa hatari na kamwe haijawahi kutumia zana na mbinu zilizopigwa marufuku.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Hivi mnavyoona kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza sana kwamba haina haja na silaha za nyuklia, inafanya hivyo kwa msingi huo huo na kwa msingi wa kushikamana kwake na mafundisho na itikadi zake za kidini.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia baadhi ya propaganda na tuhuma zinazodai kuwa Iran inaingilia masuala ya ndani ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa: Tuhuma hizo ni kinyume na ukweli wa mambo kwani Iran haijawahi na haitowahi kuingilia masuala ya nchi nyingine.
Ameongeza kuwa: Sisi tunawachukia na tunakasirishwa na watu wanaoshambulia raia, wanawake na watoto wadogo na tunaamini kuwa ni watu wasiojali mafundisho ya Uislamu na wala nafsi zao haziwasuti, lakini pamoja na hayo hatuingilii masuala ya nchi nyingine.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja sifa ya wazi ya kushikama vikosi vya ulinzi vya Iran na misingi ya Kiislamu na sheria za Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo sababu kuu inayowafanya watu wavipende vikosi hivyo na kuongeza kuwa: Sifa nyingine maalumu ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuzidi kuwa na nguvu na kuwa imara katika upande wa kiulinzi, vifaa na silaha na hilo ni katika kutekeleza yale yale maamrisho ya Mwenyezi Mungu aliposema kwenye Qur'ani Tukufu kwamba "Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo..."
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa, maendeleo ya kijeshi na kiulinzi ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa maendeleo makubwa ya kielimu na kiteknolojia, ni kitu cha kupigiwa mfano na ni sehemu ya mambo bora ya taifa la Iran na kuongeza kuwa: Maendeleo na uwezo huo wote umeweza kupatikana chini ya mashinikizo na vikwazo visivyo na mfano vya maadui na kuwepo uchache wa vyanzo muhimu jambo ambalo linayafanya maendeleo hayo kuwa jambo la kujivunia mno na inabidi kasi hiyo ya maendeleo iongezeke zaidi na zaidi.
Vile vile ameashiria namna watu wanaolitakia mabaya taifa la Iran wasivyofurahishwa na maendeleo ya kiulinzi ya vikosi vya ulinzi vya Iran na njama zao za kuzuia kuendelea kushuhudiwa maendeleo hayo akiongeza kuwa: Ni kwa sababu hiyo ndio maana utawaona wanaelekeza zaidi mashinikizo yao ya kipropaganda kwenye suala hilo hususan kwenye maendeleo katika nyuga za makombora na ndege zisizo na rubani. Lakini mantiki sahihi na ya kimantiki na ambayo inategemea aya ya Qur'ani Tukufu inatwambia kuwa, lazima tuendelee na njia hiyo kwa nguvu zetu zote.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia vitisho vya kipumbavu vya Wamarekani na kusema: Baada ya kupita muda fulani wa kukaa kimya upande wa pili, mmoja wa viongozi wa upande huo amezuka hivi karibuni na kwa mara nyingine amezungumzia machaguo yao ya juu ya meza. Kwa upande mmoja wanabambanya mambo namna hiyo na upande mwingine wanasema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isimamishe maendeleo yake ya kiulinzi. Maneno hayo kwa kweli ni ya kipuuzi kabisa.
Ayatullah Udhma Khamenei ambaye pia ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amesema: Kamwe Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiwezi kukubaliana na matamshi hayo ya kipuuzi na kwamba taifa la Iran limethibitisha kuwa, linapochokozwa, linajihami kwa nguvu zote na linashikamana vilivyo na litatoa pigo kali kwa yeyote atakayefanya uchokozi dhidi yake.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran ameviambia vikosi vya ulinzi nchini kwamba: Taasisi zote ziwe zile za Wizara ya Ulinzi au zile za (Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu) SEPAH, zote zinapaswa kujiimarisha zaidi na zaidi katika upande wa kijeshi, kiulinzi, na masuala mengine ya kijeshi sambamba na kujiimarisha kiroho na kisaikolojia, na kuyafanya mambo hayo wakati wote kuwa ndiyo ajenda yao kuu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, moyo wa mapambano wa vikosi vya ulinzi vya Iran likiwemo jeshi ni mkubwa sana na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na kuwa na nguvu za kiulinzi na kijeshi, lakini kamwe haiweza kuwa tishio kwa usalama wa nchi za Mashariki ya Kati na majirani zake.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia namna Wamarekani, nchi za Ulaya na baadhi ya vibaraka wao wanavyoeneza ngano za uongo za kudai kuwa Iran ina mpango wa kumiliki silaha za nyuklia ili kwa njia hiyo waweze kuonesha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ni tishio kwa usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na duniani na kuongeza kuwa: Leo hii tishio kubwa la usalama wa dunia na eneo la Mashariki ya Kati ni Marekani na utawala wa Kizayuni madola ambayo hayana udhibiti wowote na hayaheshimu misingi ya ubinadamu bali hata nafsi zao haziwasuti wala hawajali sheria za kidini na wanaingia popote wanapoamua na kufanya mauaji wanavyotaka.
Vile vile ameyataja matukio ya kusikitisha ya Yemen na namna Marekani na nchi za Magharibi zinavyowaunga mkono wavamizi wa Yemen kuwa ni mfano mwingine wa vitendo vya kuvunja amani na usalama duniani na kuongeza kuwa: Tofauti na nguvu zisizodhibitiwa za madola hayo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa upande wake inauhesabu usalama na amani kuwa ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu na imesimama imara kulinda na kutetea usalama wake na wa watu wengine duniani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza mwishoni mwa hotuba yake kwamba: Kulinda usalama wa nchi, mipaka na maisha ya wananchi wote ni miongoni mwa majukuu makuu ya viongozi wa masuala ya kijeshi na kiulinzi nchini.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Meja Jenerali Salehi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa hotuba fupi na sambamba na kutoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Farvardin 29 (Aprili 18) ambayo ni Siku ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Jeshi la kimapinduzi na la wacha Mungu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran liko imara kikamilifu kwa ajili ya kulinda mipaka mitukufu ya Iran na kulinda manufaa ya kiistratijia ya nchi.
Meja Jenerali Salehi amesisitiza kuwa: Wanajeshi bila ya kuangalia kufikiwa au kutofikiwa makubaliano katika milingano ya kimataifa, hawajui kitu kingine isipokuwa heshima ya taifa na wako tayari wakati wote na katika mazingira yoyote yale kujenga hamasa nyingine ya kukumbukwa milele.
 
< Nyuma   Mbele >

^