Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Afghanistan Chapa
19/04/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jioni ya leo (Jumapili) ameonana na Rais Muhammad Ashraf Ghani wa Afghanistan na sambamba na kugusia maingiliano na mambo mengi ya pamoja ya kiutamaduni na kihistoria baina ya nchi mbili ameitaja nafasi ya maulamaa na wana fasihi wa Afghanistan katika kukuza na kueneza mafundisho ya Kiislamu na lugha ya Kifarsi kuwa ni kubwa sana na kuongeza kwamba: Mbali na kuwa na vyanzo tajiri vya watu na utamaduni tajiri, Afghanistan ina pia rasilimali nyingi tajiri ambapo mambo yote hayo yanapokusanywa pamoja na mambo mengine ambayo nchi mbili zinashirikiana, yanalifanya suala la kukuza ushirikiano wa nchi mbili kuwa na faida kubwa sana.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitizia udharura wa kuwa na irada thabiti na uamuzi wa kweli wa kustawisha ushirikiano na maelewano baina ya Iran na Afghanistan na kutahadharisha kwa kusema: Tab'an Wamarekani na baadhi ya nchi za eneo hili haziujui uwezo na nafasi hiyo ya Afghanistan na haziafikiani na suala la kuelewana na kushirikiana nchi mbili, lakini Iran inayahesabu maendeleo ya jirani yake Afghanistan kuwa ni sawa kabisa na usalama na maendeleo yake.
Vile vile amekumbushia maendeleo makubwa ya Iran katika sekta na nyuga tofauti za kielimu, kiteknolojia, kiutamaduni na kidiplomasia zikiwa ni nyuga nzuri za ushirikiano wa nchi mbili na kuongeza kuwa: Masuala yanayozihusu nchi hizi mbili kama vile wahamiaji, maji, usafirishaji na usalama nayo yanaweza kutatuliwa na inabidi watu wote wayape uzito mkubwa masuala hayo na wayawekee jedwali ratiba na wakati maalumu wa kuyajadili kwa kina na kuyatatua.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia ulazima wa kutatuliwa suala muhimu la wahamiaji kwa kuashiria namna mamia ya wahamiaji wa Kiafghanistan walivyopewa fursa za masomo katika hatua tofauti nchini Iran na kuongeza kuwa: Wananchi wa Afghanistan ni watu wenye vipaji vingi, vikubwa na werevu na kwamba vipawa hivyo vinapaswa vitumiwe vizuri katika kutafuta elimu kwani wasomi wa Afghanstan ni muhimu mno kwa ajili ya kuijenga upya nchi yao.
Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja Tehran kuwa ni sawa na nyumbani kwa ndugu zao wa Afghanistan na huku akiashiria maingiliano na urafiki wa muda mrefu na madhubuti baina ya Iran na jirani yake Aghanistan amesema kuwa, ana matumaini kwamba kadiri siku zinavyopita ndivyo serikali ya Afghanistan na taifa la nchi hiyo litakavyozidi kupata nguvu za ndani na kuimarika zaidi.
Katika mazungumzo hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Muhammad Ashraf Ghani wa Afghanistan ameelezea kufurahishwa kwake na safari yake ya mjini Tehran na kugusia uhusiano mkongwe na madhubuti wa kihistoria na kiutamaduni baina ya Iran na Afghanistan na kuongeza kuwa: Lengo letu ni kuifanya Afghanistan kuwa kituo kikuu cha kuunganisha maeneo tofauti ya eneo hili na kuirejeshea hadhi yake ya zamani ya kuwa makutano ya mawasiliano ya nchi za eneo hili.
Rais wa Afghanistan amebainisha pia kuwa hivi sasa kuna Tehran na Kabul zinakabiliwa na hatari zinazofanana na kuna fursa nyingi za pamoja baina ya Iran na Afghanistan na kuongeza kwa kusema: Irada na nia yetu ya kweli ya kisiasa imesimama juu ya msingi wa kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na inabidi tufanye juhudi zetu zote kuhakikisha kuwa mambo ya pamoja na nukta chanya zinapata nguvu na kuimarisha uhusiano wa nchi mbili kadiri inavyowezekana.
Amesema, lengo la siasa za serikali ya Afghanistan ni kubadilisha migongano na mapigano ya ndani ya nchi hiyo kuwa nukta na fursa nzuri za kuimarisha ushirikiano nchini humo na kuhusu uhusiano wa nchi mbili za Iran na Afghanistan amegusia kuweko baadhi ya matatizo kama vile suala la ugaidi, madawa ya kulevya, wahamiaji, maji na mipaka ya pamoja na kusisitiza kuwa: Inabidi masuala hayo yanayozihusu nchi mbili yatatuliwe kwa nia ya kweli ya kisiasa ya serikali za nchi zote mbili na kulingana na jedwali ya wakati maalumu ambayo tayari imeandaliwa katika safari yake hii ya mjini Tehran.
Bw. Ashraf Ghani aidha amesema kuwa, suala la magendo ya mihadarati na madawa ya kulevya linaisababishia Iran hasara kubwa na kuongeza kuwa hakuna jirani yeyote wa Afghanistan aliyelipa kipaumbele kikubwa mno suala la kupambana na madawa ya kulevya kama inavyofanya Iran na kwamba serikai yake iko tayari kusaidiana na Iran kwa kadiri ya uwezo wake katika kupambana kwa pamoja na balaa hilo angamizi.
Rais wa Afghanistan amegusia pia suala la kustawishwa uhusiano wa nchi mbili katika masuala ya usafiri na usafirishaji bidhaa, uwekezaji na ushirikiano katika masuala ya kiutamaduni na kiuchumi na kumwambia Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba: Iran ikiwa chini ya uongozi wako wa busara, imeweza kusimamisha thabiti utambulisho wake wa kihistoria na ni matumaini yetu kwamba kwa kutegemea uongozi wako huo wa busara, tutaweza kushuhudia maendeleo makubwa katika ushirikiano wa nchi mbili.
 
< Nyuma   Mbele >

^