Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi MuadhamuAonana na Wajumbe wa Kamati ya Kongamano la Kuwaenzi Mashahidi wa Semnan Chapa
13/05/2015
Wajumbe wa kamati ya Kongamano la Kuwaenzi Mashahidi Elfu Tatu wa Mkoa wa Semnan leo jioni (Jumatatu) wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika mazungumzo hayo, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amegusia sifa za kipekee na za aina yake za mkoa wa Semnan kutokana na kufanikiwa mkoa huo kulea shakhsia wakubwa wa kidini, kielimu na kisiasa na kuitaja hatua ya kufanyika kongamano la kuwaenzi mashahidi wa Semnan na kutukuza kujitolea kwao muhanga pamoja na ushujaa wao wa kupigiwa mfano kuwa ni jambo zuri sana lenye thamani kubwa.
Ameongeza kuwa: Kujitolea muhanga mashahidi ni utajiri wa kubakia milele wa Mapinduzi ya Kiislamu na kwamba kuwaenzi na kuhakikisha jina la mashahidi hao azizi halisahauliwi ni faradhi kwa kila mtu.
Ameashiria pia njama za baadhi ya wanaoitakia mabaya Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran ambao wanafanya kila njia ili kusahaulisha kazi kubwa iliyofanywa na mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Kazi za kukuza na kuenzi utajo wa mashahidi unapaswa ufanyike kwa lengo moja kuu nalo ni kutukuza mambo mema tunayojifunza kutoka kwa mashahidi hao yaani imani thabiti ya dini, ushujaa na kuwa tayari kwao kujitolea muhanga maisha yao kwa ajili ya kulinda matukufu yao na kwamba inabidi mambo hayo yafikishwe kwa njia bora kabisa kwa walengwa kwa maana halisi ya neno.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha pia udharura wa kutumiwa njia bora na mbinu za kisasa kwa ajili ya kuongeza kiwango cha taathira za mafundisho hayo kwa walengwa hususan kizazi cha vijana na kusisitiza kuwa: Nguvu, hima, nia, azma na imani ya vijana wa leo haina mapungufu yoyote ikilinganishwa na ya vijana wa muongo wa 60 (mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia sawa na muongo wa 80 wa mwaka wa Miladia) bali kijana wa leo anakabiliwa na vitisho mbali mbali na vya hatari zaidi vya kifikra, ambapo fikra hizo ghalati na mbaya zinazomkabili kijana wa sasa hivi zinaweza kuenezwa kwa wingi mno kwa kutumia zana na njia za kila namna za kisasa za mawasiliano.
Ayatullah Udhma Khamenei ametilia mkazo pia umuhimu wa kumjua vyema mlengwa na kudumisha mawasiliano yenye taathira baina ya wafikishaji na wapokeaji wa ujumbe fulani na huku akisisitizia ulazima wa kuzingatiwa tofauti za kiutamatuni katika kuwasiliana na walengwa amesema: Inabidi katika uwanja huo watumike wataalamu, maulamaa na watu wenye uzoefu katika masuala ya mawasiliano kama ambavyo kuna wajibu pia wa kutumiwa nguvu ya sanaa kwa kadiri inavyowezekana katika kufkisha inavyotakiwa kwa walengwa - ujumbe wa mashahidi hao.
Vile vile amezitaja nyuga za kisiasa, kiuchumi, kiusalama na muhimu kuliko yote uga wa kiutamaduni kuwa ni medani za mapambano ya Iran ya Kiislamu na maadui na kuongeza kwamba: Adui anaendesha mapambano kwa njia ya kipekee kabisa na tunatakiwa tuwe tumejiandaa kikamilifu na kukabiliana vilivyo na mashambulizi hayo ya adui tukiwa na welewa wa kina kuhusu njama zake.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mabwana Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Muhammad Shah Cheraghi, mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) ambaye pia ni Imam wa Ijumaa wa mkoa wa Semnan na Kamanda Shah Cheraghi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Sepah ya Qaim Aal Muhammad (AS) katika mkoa wa Semnan, wametoa ripoti zao mbele ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei.
 
< Nyuma   Mbele >

^