Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Atembelea Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran Chapa
13/05/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatano) ametembelea Maonyesho ya Ishirini na Nane ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran yanayoendelea katika eneo la Musalla wa Imam Khomeini (quddisa sirruh).
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametembelea maonyesho hayo kwa muda wa masaa mawili na nusu ambapo Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bw. Jannati, naye ameandama na Kiongozi Muadhamu katika kutembelea maonyesho hayo.
Wahusika kwenye vibanda vya maonyesho hayo na baadhi ya wasambazaji na wachapishaji wa vitabu wamepata fursa ya kutoa ufafanuzi na maelezo tofauti kuhusu kazi zao za karibuni kabisa na hatua walizopiga katika uwanja wa kuchapisha na kusambaza vitabu.
 
< Nyuma   Mbele >

^