Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Ahudhuria Sherehe za Kuhitimu Masomo Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Imam Husain AS Chapa
20/05/2015
 Katika wakati huu wa kukaribia maadhimisho ya "Siku ya Pasdar" na vile vile tarehe 3 Khordad (Mei 24) siku ya kuadhimisha operesheni yenye fakhari kubwa ya Baytul Muqaddas na kukombolewa mji wa Khorramshahr (wakati wa vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu vilivyoanzishwa na utawala wa wakati huo wa Iraq dhidi ya Iran) leo (Jumatano), kumefanyika sherehe za kuhitimu masomo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha maafisa wa kijeshi cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam na kuhudhuriwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wakati wa kuingia kwenye uwanja wa sherehe hizo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekwenda eneo la mashahidi na kuwasomea faatiha mashahidi hao wa vita vya kujihami kutakatifu akimuomba Mwenyezi Mungu awapandishe daraja za juu za utukufu. Baada ya hapo Amirijeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amekagua vikosi vilivyokuwa vimepanga paredi kwenye uwanja huo. Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amewaenzi na kuonyesha heshima na mapenzi yake makubwa kwa majeruhi wa vita waliokuwepo kwenye medani hiyo.
Ayatullah Udhma Khamenei ametoa hotuba muhimu katika sherehe hizo na huku akiashiria fikra mpya ya Uislamu na pia fikra ya kijahilia zikiwa ndizo fikra mbili kuu zinazotawala katika dunia ya leo amesema kuwa, ni jambo lisiloyumkinika kwa fikra hizo mbili kukurubiana na kupatana.
Vile vile amegusia namna kulivyozushwa mambo mapya na wapenda makuu katika mazungumzo yanayoendelea ya nyuklia kati ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 ikiwa ni pamoja na kutaka waruhusiwe kuyakagua maeneo ya kijeshi ya Iran na kuzungumza na wanasayansi wa nyuklia wa Iran akisisitiza kuwa: Ruhusa hiyo kamwe haitatolewa; na maadui watambue kuwa, wananchi na viongozi wa Iran hawatalegeza kamba hata kidogo katika kukabiliana na ubeberu na kupenda kwao makuu.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amegusia pia habari inayosema kwamba wanaolitakia mabaya taifa la Iran na baadhi ya viongozi wa eneo la Ghuba ya Uajemi wanafanya njama za kufikisha kwenye mipaka ya Iran vita vinavyopiganwa kwa niaba ya wengine na kusema: Kama kutafanyika uafiriti wowote ule, basi wajue kuwa majibu na radiamali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakuwa kali mno.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesisitiza katika sherehe hizo juu ya hima ya kufanya kazi mpya, kufanya ubunifu na kutekeleza mambo yenye faida kubwa katika masuala yote na huku akiashiria kuweko sifa hizo maalumu katika sherehe hizo za leo katika Chuo Kikuu cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam amesema: Inabidi tujiepushe kufanya vitu vyenye viwango vya chini katika masuala yetu yote.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni mti mwema ambao umefikia kwenye hatua nzuri za uwezo, maendeleo na kupevuka kifikra na kivitendo na kuongeza kuwa: Chuo Kikuu cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam ni moja ya ushahidi wa ukamilifu wa harakati zinazozidi kustawi za jeshi la Sepah.
Amesema, nguvu muhimu ya Chuo Kikuu hicho ni operesheni adhimu za kijeshi za kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu na jihadi ya kupigiwa mfano na kujitolea muhanga wanamapambano wa jeshi la Sepah wakati huo na amewaelekea wanachuo wa Chuo Kikuu hicho akiwaambia: Leo hii bendera ya Mapinduzi adhimu ya Kiislamu ambayo ni bendera ya fikra mpya ya Kiislamu, imefika mikononi mwenu na inabidi muendelee kuihifadhi na kuilinda kwa nguvu zenu zote na kwa umadhubuti wa hali ya juu kama walivyofanya waliokutangulieni.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja bendera ya fikra mpya ya Kiislamu kwamba ni kwa ajili ya kufanikisha saada na ufanisi wa mwanadamu na ni kwa ajili ya kukifungulia njia na kuvutia hisia za kizazi cha vijana duniani na kuongeza kuwa: Harakati hii iliyojaa fakhari, ilianzishwa na Imam wetu mtukufu (Imam Khiomeini - quddisa sirruh) na taifa la Iran nalo likajitolea na kukubali kuvumilia shida na tabu za kila namna ili kuilinda na kuiimarisha harakati hiyo na kupeperusha juu bendera yake kwa ushujaa mkubwa.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia kuwepo fikra nyingine ijulikanayio kwa jina la fikra ya kijahilia na kuongeza kuwa: Fikra ya kijahilia ambayo leo imejidhihirisha kwa sura ya fikra ya kidhulma, kibeberu, kiistikbari na ubinafsi kupitia madola ya kibeberu duniani, ni tofauti kikamilifu na fikra ya Kiislamu ambayo inapigania uadilifu, uhuru wa mwanadamu, kuangamiza nyuga za kuweza wanadamu kunyonywa na kukoloniwa pamoja na kuangamiza mfumo mzima wa kibeberu.
Vile vile amesisitiza kwamba macho ya watu wanaoangalia mbali duniani yanaweza kutofautisha baina ya fikra hizo mbili na kujua harakati ya kinafiki na ya ubinafsi iliyojikita ndani ya fikra ya ujahilia chini ya nyuma ya pazia la maneno kama vile haki za binadamu na kupiga vita machafuko.
Ameongeza kuwa, uwezekano wa kupatana na kukurubiana fikra hizi mbili kamwe hauwezi kuwepo kwani fikra moja inaunga mkono dhulma na ukandamizaji wa mataifa mengine duniani wakati ambapo fikra ya pili inapigania kuungwa mkono na kulindwa watu wanaodhulumiwa mbele ya dhulma ya madhalimu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia propaganda za maadui wanaodai kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetengwa kimataifa na kusisitiza kuwa: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu tangu awali kabisa ya kuundwa kwake, muda wote umekuwa unapendwa na watu wa mataifa ya dunia na mfano wa wazi kabisa wa uhakika huo ni namna watu wa nchi mbali mbali duniani wanavyoonesha mapenzi yao ya kustaajabisha kwa marais wa Iran wanapotembelea nchi hizo tena katika kipindi chote hiki cha miaka thelathini na sita (ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu).
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa, jina la taifa la Iran mbele ya mataifa ya dunia na hata mbele ya viongozi wenye insafu, wenye fikra huru na wanaopenda ukombozi duniani, ni jina tukufu na lililojaa fakhari na kusisitiza kwamba: Waliotengwa ni wale watu ambao wanaweza kuwavutia upande wao baadhi tu ya watu tena kwa kutumia vitisho na fedha.
Amesisitiza kuwa, taifa la Iran limefanikiwa kupata heshima yake kupitia Uislamu na harakati zake na malengo yake matukufu ya kimapinduzi kama ambavyo amegusia pia kuwepo changamoto mbali mbali zinazoukabili mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kusema: Sisi hatuna hofu wala woga wowote mbele ya changamoto hizo kwani kuwepo changamoto kuna maana ya kuwepo harakati, kuwa hai, kuwa na harakati na kuwa amilifu na ni kuzidi kupata nguvu harakati za ustawi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Taifa la Iran litaweza kuzivuuka changamoto hizo kwa nguvu zote na kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kwa kujiamini.
Ayatullah Udhma Khamenei ametaja moja ya changamoto hizo kuwa ni ubeberu na kupenda makuu upande wa pili unaofanya mazungumzo ya nyuklia na Iran na kusema kwa kusisitiza kwamba: Hadi hivi sasa maadui bado hawajalijua vyema taifa la Iran na viongozi wa Iran na ndio maana wanafanya ubeberu wao lakini taifa la Iran na serikali iliyochaguliwa na taifa hili, kamwe haitokubali kupigishwa magoti na ubeberu wa waistikbari.
Amesisitiza pia kuwa, kulegeza kamba kwa kiasi chochote kile mbele ya wapenda makuu wa upande wa pili basi kutawafanya wapenda makuu hao wasogee mbele zaidi na watake mambo makubwa zaidi na kuongeza kuwa: Inabidi tujenge ukuta madhubuti kwa kutumia nia na azma ya kweli, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kwa kutumia nguvu za kitaifa katika kukabiliana na kupenda makuu upande huo wa pili wa mazungumzo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mfano wa jamb hilo akisema kuwa, moja ya mifano ya kupenda makuu upande wa pili wa mazungumzo ya nyuklia ni kutaka kwao kukagua vituo na kambi za kijeshi za Iran pamoja na kuzungumza na wataalamu na watafiti wa nyuklia wa Iran.
Amesema: Kama ambavyo tulisema pia huko nyuma, hakutatolewa ruhusa ya aina yoyote ile ya kukagua vituo na maeneo yetu ya kijeshi wala kufanyika mazungumzo na wataalamu wetu wa nyuklia na sekta nyingine zote nyeti na kamwetu hatutoruhusu kuvunjia heshima mipaka ya maeneo hayo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Mimi sitoruhusu watu baki waje hapa kuzunguza na kuwasaili wataalamu wetu na wana azizi na muhimu wa taifa hili.
Amesema kuwa, hakuna taifa wala dola lolote lenye akili litakalokubali kufanyiwa jambo kama hilo na kuongeza kuwa: Adui jeuri na muovu anataraji kwamba sisi tutamruhusu azungumze na wataalamu na watafiti wetu kuhusu maendeleo fulani tuliyojipatia kwa jitihada zetu za ndani na maendeleo yetu ya kitaifa. Lakini ajue kuwa ruhusa kama hiyo kamwe haitatolewa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Suala hilo wanapaswa walitambue vyema maadui wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na wale wote wanaosubiri kusikia uamuzi wa Jamhuri ya Kiislamu kuhusiana na jambo hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa viongozi wetu azizi nchini ambao wanaendelea na harakati zao kwa ushujaa mkubwa kwenye medani hiyo, wajue kuwa njia pekee ya kukabiliana na adui huyu muovu ni kuwa na nia ya kweli, kutotetereka, msimamo madhubuti na kutofanya mambo kwa pupa.
Amesisitiza kwamba: Viongozi na maafisa wetu wanaoshiriki kwenye mazungumzo hayo wanapaswa waoneshe ujumbe wa utukufu wa taifa la Iran kwenye mazungumzo hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, viongozi wote nchini wameweza kuwa viongozi wa taifa hili kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Sisi sote ni watumishi wa wananchi na tuna jukumu la kusimama kidete kikamilifu kukabiliana na ubeberu, ujuba, jeuri, njama na kupenda makuu mabeberu - (kupenda makuu ambako) hakuna kichwa wala miguu.
Ayatullah Udhma Khamenei ameendelea na hotuba yake kwa kugusia baadhi ya habari zinazosema kwamba kuna njama za pamoja za maadui na baadhi ya viongozi wapumbavu katika eneo la Ghuba ya Uajemi ambao wana nia ya kufikisha vita vinavyopiganwa kwa niaba ya wengine, kwenye mipaka ya Iran na kusisitiza kuwa: Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na walinzi wote wa mipaka ya usalama wa taifa katika vikosi vyote vya ulinzi vya Iran wako makini na wako macho na kama kutatokea uafiriti wowote ule, basi radiamali na majibu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatakuwa makali mno.
Amesisitiza kuwa, taifa la Iran litaendelea kusonga mbele kwa matumaini kamili katika njia yake yenye upeo unaong'ara na kuongeza kuwa: Kuendelea na safari katika njia na harakati ya kufanikisha malengo aali na matukufu bila ya shaka yoyote ni jambo ambalo lina gharama kubwa na kwamba katika kipindi chote hiki cha historia pia, mataifa yote yaliyopata nishani za ushindi ni yale ambayo hayakusalimu mbele ya changamoto mbalimbali na ambayo yameonesha nguvu zao za kitaifa na kujijengea ngao na kinga madhubuti katika kukabiliana na uchokozi wa aina yoyote ile, mzito na mwepesi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja taifa la Iran kuwa ni miongoni mwa mataifa hayo na mwishoni mwa hotuba yake ameelezea matumaini yake kwamba vijana azizi na kizazi chipukizi cha Iran kitaisimamia vilivyo na kwa nguvu zake zote amana kiliyorithishwa na vizazi vya kabla yao.
Katika sherehe hizo, Meja Jenerali Muhammad Ali Jaafari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amelitaja lengo la kuimarishwa na kuongezwa ukakamavu na uimara wa kila upande wa jeshi la SEPAH kuwa ni kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu na kulinda mafanikio yake akisisitiza kuwa: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu linadiriki vilivyo mazingira ya Mapinduzi ya Kiislamu na mapambano ya kambi mbili za wanyonge na mabeberu na kufuatilia kwa kina suala la kuzalisha nguvu za ndani ya jeshi hilo ambazo kila leo zinazidi kustawi kwa kutegemea umaanawi, imani, mantiki na weledi wa mambo na kwa kutumia teknolojia za kisasa za kiulinzi na kiusalama na kuzifanya za kisasa mbinu zisizo maarufu na zisizotabirika za mapambano.
Meja Jenerali Jaafari amesisitiza kuwa, ushujaa wa kiungwana ni sehemu ya ulinzi na kuongeza kuwa: Kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu mbele ya maadui katika kivuli cha umeme wa panga zetu na nguvu zetu za kiimani na kiteknolojia za kisasa ambazo zinaingiza woga katika nyoyo za maadui na kuwafanya wahisi hatari kila wanapofikiria nguvu hizo.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amebainisha kuwa maadui wanaielewa zaidi lugha ya silaha na sisi tumedhamiria kukabiliana na adui kwa lugha hiyo hiyo na kusisitiza kwamba: Silaha za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH zinatumika kwa ajili ya kuwalinda wapigania uadilifu na wanaopambana na dhulma.
Kwa upande wake Admirali Morteza Safari, Kamanda wa Chuo Kikuu cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam ametoa ripoti kuhusu ratiba na hatua za kielimu na kiutamaduni za Chuo Kikuu hicho.
Kwenye sherehe hizo, makamanda wawili na wahadhiri na watafiti wawili pamoja na mwakilishi wa wanachuo waliohitimu masomo pamoja na wanachuo bora wa Chuo Kikuu cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam wamepata fakhari ya kupokea zawadi zao kutoka kwa Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo mwakilishi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam amepata fakhari ya kupanda cheo na kuvikwa nishani na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kuendeshwa ratiba ya wanachuo ya kujipanga na kutengeneza sura ya "mti mwema" wakiakisi sura ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni miongoni mwa ratiba zilizokuwemo kwenye sherhe hizo za leo ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha maafisa wa kijeshi cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam kula kiapo na kutangaza utiifu wao kwa Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa Mapinduzi ya Kiislamu.
Vile vile katika sherehe hizo, wanachuo wa Chuo Kikuu cha Imam Husain Alayhi ‘s-Salaam wameonyesha uwezo wao mbali mbali wa kivita na mbinu tofauti za kujilinda binafsi. Vile vile vikosi mbali mbali vilivyokuwepo kwenye uwanja wa sherehe hizo vimepita kwa gwaride mbele ya Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei.
 
< Nyuma   Mbele >

^