Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Chapa
23/05/2015
 Katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mwana mtukufu wa Imam Ali AS, Abul Fadhlil Abbas Alayhi ‘s-Salaam, anga ya Husainia ya Imam Khomeini quddisa sirruh imehinikiza manukato na uturi wa kimaanawi wa aya zenye kuleta uhai mpya za maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu wakati maustadh, wahadhiri, maqarii na ‘mahuffadh' bora wa Qur'ani Tukufu walioshiriki kwenye Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Qur'ani Takatifu ya mjini Tehran walipoonana na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika sherehe zilizopambwa na nuru ya kujikurubisha kwa Kitabu hicho kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.
Katika mkutano huo, Ayatullah Udhma Khamenei amesisitizia ulazima wa kupewa kipaumbele Qur'ani Tukufu katika vipengee vyote vya maisha ya mtu binafsi na ya kijamii ya Waislamu na kulitaja jambo la lazima la kufikia kwenye lengo hilo aali na takatifu kuwa na masuala mawili makuu ambayo ni busuri na muono wa mbali na nia na azma ya kweli.
Ameongeza kuwa dawa ya kutibu matatizo ya hivi sasa ya ulimwengu wa Kiislamu ni kujisalimisha mbele ya amri na mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kutojisalimisha mbele ya mambo yanayotwishwa na ujahilia wa zama hizi na pia kusimama kidete katika kukabiliana na ubeberu utokanao na ujahilia huo.
Amesema, kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu ni utangulizi wa kujipamba kwa maadili ya Qur'ani na ni utangulizi wa kuundika jamii iliyosimama juu ya misingi na mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kuongeza kuwa: Jambo la kusikitisha hivi sasa ni kuona kwamba ulimwengu wa Kiislamu ni dhaifu, ni fakiri, na ni uliojaa mizozo na vita vya ndani vinavyotokana na mashinikizo ya mifumo ya kijahilia na kwamba ulimwengu huo wa Kiislamu unateseka sana hivi sasa kutokana na mambo hayo. Amesema njia pekee ya kukabiliana na mashinikizo hayo ya kutwishwa; ni Waislamu kujisalimisha mbele ya mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kuwa na nia na azma ya kweli ya kufaniksha ipasavyo malengo matukufu ya umma wa Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Iwapo itapigwa hatua moja mbele kuelekea kwenye ufanikishaji wa malengo ya Qur'ani; Mwenyezi Mungu ataongeza nguvu maradufu kwenye hatua hiyo na hilo ni jambo ambalo taifa la Iran lina uzoefu nalo na kutokana na taifa hili kusimama kidete katika kukabiliana na mabeberu, limeweza kuwa na nguvu, uwezo mkubwa na matumaini zaidi.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kustafidi vizuri na uzoefu wa taifa la Iran katika kusimama kidete kukabiliana na madola ya kibeberu kuwa ni dawa ya kutibu matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Kuzusha mizozo na mifarakano katika umma wa Kiislamu, leo hii imekuwa ni moja ya mipango mikuu ya maadui, hivyo watu wote wanapaswa kuwa macho ili - Mwenyezi Mungu apishie mbali - Waislamu wasije wakatumika katika kueneza mifarakano kati ya Waislamu na kugeuzwa kuwa mabomba ya sauti za maadui wa Uislamu na wa Qur'ani Tukufu.
Amesisitiza kuwa, koromeo lolote litakalotoa sauti ya kueneza mizozo na mifarakano kati ya Waislamu basi ijulikane kwamba koromeo hilo limekuwa bomba la sauti ya adui na kuongeza kuwa: Kuzusha mizozo kwa jina la Ushia na Usuni, Uarabu na Uajemi, mifarakano ya kikaumu na kitaifa pamoja na taasubu za kitaifa ni katika ajenda kuu za maadui wanaoutakia mabaya umma wa Kiislamu na inabidi kupambana na njama hizo kwa kutumia muono wa mbali na nia na azma ya kweli.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kuwa na busuri na muono wa mbali na kumtambua vyema nani rafiki na nani adui kuwa ni jambo la dharura sana na kusisitiza kwamba: Wakati nia na azma ya kweli inapokuwa pamoja na busuri na muono wa mbali, huwa rahisi kuendelea na njia ya kusimama kidete katika kukabiliana na mashinikizo pamoja na njama na utwishaji wa mambo wa maadui na hiyo ndiyo hiyo inayoitwa nusura ya Mwenyezi Mungu.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kuzidi kueneza utamaduni wa kuwa na ukuruba na Qur'ani katika jamii kuwa ni jambo linaloleta matumaini na kutoa biashara njema na kusisitizia udharura wa viongozi nchini Iran kulipa uzito wa hali ya juu suala hilo la kueneza mapenzi na ukuruba mkubwa na Qur'ani Tukufu na kuongeza kuwa: Inabidi vijana na wasomi wajenge mapenzi makubwa na wawe na ukuruba mkubwa zaidi na Qur'ani Tukufu kwani wakati akili ya mtu inapokuwa na utajiri wa maarifa na mafundisho ya Qur'ani, athari za jambo hilo huonekana katika maneno, matendo na maamuzi yote ya mtu huyo.
Amekutaja kuwa na mapenzi na ukuruba na Qur'ani Tukufu kwamba kunadhamini mustakbali bora uliojaa saada na ufanisi na kusisitiza kwamba: Kwa bahati nzuri leo hii harakati ya kuelekea kwenye Uislamu na Qur'ani imeanza katika jamii za Waislamu ambapo baraka ya jambo hilo ni kuenea mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Mwamko wa Kiislamu ni uhakika ambao hauyumkiniki kuukandamiza na kuumaliza bali taathira za mwamko huo zinaongezeka siku hadi hadi siku.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja jukumu la maulamaa, wasomi, waandishi, wanafunzi wa Vyuo Vikuu, watafiti, maqarii na wote wanaohifadhi Qur'ani Tukufu kuwa ni kubwa sana katika kueneza mwamko wa Kiislamu na kusisitiza kwamba: Inabidi tuimarishe matumaini ya watu kuhusiana na mambo mazuri na mustakbali mwema ambao umebashiriwa na Qur'ani Tukufu.
Mwishoni mwa miongozo yake, Ayatullah Udhma Khamenei ameelezea matumaini yake kwamba tawala za nchi za Waislamu zitatekeleza kivitendo maamrisho ya Qur‘ani Tukufu badala ya kusema kwa maneno tu kuhusu umuhimu wa mafundisho hayo.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammadi, mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqiih) na Mkuu wa Taasisi ya Wakfu na Mambo ya Kheri ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa kuanza sikukuu za mwezi mtukufu wa Shaabani na ametoa ripoti fupi kuhusiana na mchakato mzima wa kufanyika Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu, mjini Tehran.
Amesema kuwa, mashindano ya mwaka huu ya Qur'ani Tukufu ya mjini Tehran yamekuwa bora zaidi katika upande wa idadi na ubora ikilinganishwa na mashindano ya mwaka jana na kuongeza kuwa: Washiriki wote wamezingatiwa na kupewa uzito sawa bila ya kubaguliwa jambo lililojenga mapenzi makubwa baina yao, kuwepo maqarii vijana na chipukizi, kufanyika hafla za kuwa na mapenzi na ukuruba na Qur'ani tukufu katika mikoa ya Iran wakishiriki pia maqarii kutoka nje, kuenziwa akina mama wanaofanya harakati katika masuala ya Qur'ani na kujitokeza kwa wingi wananchi na viongozi katika mashindano hayo ni miongoni mwa sifa maalumu za kipekee zilizokuwemo kwenye Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya mjini Tehran.
 
< Nyuma   Mbele >

^