Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Kufuatia Maziko ya Mashahidi Yaliyohudhuriwa kwa Hamasana Wananchi wa Tehran Chapa
16/06/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe muhimu wa kuelezea shukrani zake kubwa kwa wananchi wa Tehran kutokana na kushiriki kwa wingi na kwa hamasa kubwa katika maziko ya miili mitoharifu ya mashahidi 270 wa kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu (vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa wakati huo wa Iraq dhidi ya Iran).

Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Rehema na amani ya Mwenyezi Mungu iwafikie mashahidi azizi waliowasha mwenge wa tawhidi katika taifa hili la Kiislamu kwa kujitolea kwao muhanga (katika njia ya haki). Na rehema na salamu za Mwenyezi Mungu ziwafikie mashahidi wapiga mbizi waliodhulumiwa ambao kwa dhati na uwepo wao wote wameendeleza njia ya mashahidi waliowasha mwenge huo wenye nuru isiyozimika na kupeperusha kwa ufakhari wa hali ya juu mno bendera ya kumbukumbu zetu azizi na zenye thamani kubwa na akiba ya kimaanawi ya umma katika nchi hii.
Amani iwe juu ya mikono iliyofungwa na viwiliwili vyenu vilivyoadhibiwa na amani iwe juu ya roho zenu safi na zilizopata radhi za Mwenyezi Mungu na kumea mbawa za rehema. Amani iwe juu yenu (mashahidi azizi) ambao kwa mara nyingine mumeeneza manukato katika anga ya maisha na kuzishibisha nyoyo na roho za viumbe. Na shukrani zisizo na kikomo ziende kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima na Mwingi wa huruma Ambaye hushusha bishara njema zisizo na shaka kutimia kwake kwenye nyoyo za watu wa taifa hili linalomwamini Mwenyezi Mungu na kupigana jihadi katika njia Yake. (Mwenyezi Mungu hususha bishara zake hizo zisizo na chembe ya shaka) katika nyakati na sekunde nyeti na muwafaka. Na salamu zikufikieni taifa kubwa, aminifu, erevu na linaloheshimu majukumu yake (la Iran) ambalo linaelewa vizuri mafundisho matukufu ya Mwenyezi Mungu na kuyakubali na kuyatekeleza ipasavyo. Kujitokeza kwenu - kwenye maana na malengo mapana - katika shughuli ya maziko ya vito hivi adhimu na vya kipekee vilivyorejea nchini, ni moja ya matukio yatakayokumbukwa milele katika historia ya matukio ya Mapinduzi ya Kiislamu. Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu.
Na shukrani zisizo na kikomo zinamstahikia Mwenyezi Mungu Ambaye Ndiye mmiliki wa nyoyo na amani zisizo na mwisho zimfikie Baqiyyatullah (Imam Mahdi AS) roho yangu iwe fidia kwake na ambaye ndiye mmiliki wa utajiri huu adhimu.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Sayyid Ali Khamenei,
26 Khordad, 1394
(Juni 16, 2015).
 
< Nyuma   Mbele >

^