Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Ahudhuria Mahafali ya Kujenga Mapenzi Makubwa na Qur'aniTukufu Chapa
18/06/2015
 Sambamba na siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao imeshushwa ndani yake Qur'ani, alasiri ya leo (Alkhamisi) kumefanyika mjini Tehran, mahafali ya kujenga mapenzi makubwa na Qur'ani Tukufu yaliyohudhuriwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika mahafali hayo yaliyojaa nuru na kuhinikiza manukato na umaanawi wa Qur'ani, maqari na mahafidh 15 wa Qur'ani Tukufu pamoja na wahadhiri wa Qur'ani kutoka kona zote za Iran, wamesoma baadhi ya aya tukufu za maneno hayo ya Mwenyezi Mungu na kikundi cha kasida nacho kimepata fursa ya kusoma kasida za kumshukuru na kumhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Katika mahfali hayo, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amesifu maendeleo yanayozidi kuongezeka na kustawi kila uchao na ambayo yanashuhudiwa wazi wazi kati ya maqarii wa Kiirani na ameitaja sauti nzuri ya kusoma Qur'ani Tukufu kuwa ni utangulizi wa kuziandaa vizuri nyoyo za wasikilizaji kwa ajili ya kufikia kwenye malengo makuu ya maneno hayo ya Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa: Bado kuna nafasi kubwa na pana sana ya kuweza kuenea taathira zaidi za Qur'ani Tukufu katika jamii, na kwamba jambo la lazima la kuweza kutoa athari kubwa zaidi Qur'ani Tukufu katika jamii ni qiraa ambapo qarii mwenyewe mbali na kutakiwa kufikisha vizuri - kwa walengwa - mafundisho ya aya za Qur'ani Tukufu yeye mwenyewe naye ni lazima awe na imani ya kweli na ya kina kuhusu maneno hayo ya Mwenyezi Mungu.
Ameongeza kuwa: Maqarii wa Qur'ani Tukufu wanaweza kwa ajili ya kufikisha vizuri mafundisho ya Kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu, kusoma kwa kusisitiza baadhi ya maneno ya Qur'ani na kuyasoma kwa kuyakariri mara kadhaa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hapo hapo lakini ametahadharisha pia kuhusu ubaya wa kuchupa mipaka katika kukariri mno kusoma baadhi ya aya na vile vile amesema: Moja na jambo jengine la lazima la kukifanya kisomo cha Qur'ani Tukufu kuwa na taathira kubwa ni kuchunga mizani za sauti wakati wa kusoma aya za Qur'ani.
Ayatullah Udhma Khamenei ametoa pia nasaha nyingine muhimu kwa maqarii na kwa watu wote wanaofanya kazi za Qur'ani Tukufu kwamba hakuna haja ya kurefusha kusoma baadhi fulani tu ya maneno au aya za Qur'ani, kama ambavyo kushangiria kupita kiasi nako si jambo jema, bali ni jambo lisilo na udharura wowote ule.
 
< Nyuma   Mbele >

^