Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Akabidhi Siasa Kuu za Mpango wa Sita wa Taifa wa Maendeleo Chapa
30/05/2015
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amemwandikia barua Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ndani yake mna siasa kuu za Mpango wa Sita wa Taifa wa Maendeleo.
Siasa hizo kuu zimesimama juu ya msingi wa mihimili mitatu ya "Uchumi wa Kusimama Kidete," "Kuwa mstari wa mbele katika uga wa elimu na teknolojia" na "Kuimarisha na kutia nguvu masuala ya kiutamaduni." Siasa hizo zimeandaliwa kwa kuzingatia uhalisia wa mambo ulivyo hivi sasa ndani na nje ya Iran ili baada ya kufanikishwa malengo na shabaha za Mpango wa Sita wa Taifa wa Maendeleo, kuweze kutolewa kigezo kinachotokana na tafakuri ya Kiislamu katika uwanja wa maendeleo ambayo yatakuwa yako mbali kikamilifu na mfumo wa kibepari duniani.
Siasa kuu za Mpango wa Sita wa Taifa wa Maendeleo zina vifungu 80 na zina vifungu vikuu vinavyohusiana na masuala ya "Uchumi," "Teknolojia ya Habari na Mawasiliano," "Masuala ya Kijamii," "Ulinzi na Usalama," "Siasa za Nje," "Sheria na Masuala ya Mahakama," "Masuala ya Kiutamaduni" pamoja na "Sayansi, teknolojia na elimu za kisasa."
Matini kamili ya barua hiyo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo pia imetumwa kwa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na kwa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:
 
 
Bismillahir Rahmanir Rahim.

Janab Dk Rouhani
Mheshimiwa Rais
Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh

Kwa vile tumekaribia kwenye miezi ya mwanzoni mwa muongo wa pili wa malengo ya miaka 20 ya maendeleo nchini, nimeamua kuwasilisha kwako siasa kuu za Mpango wa Sita wa Miaka Mitano ya Maendeleo ya Taifa.
Majimui ya siasa hizo imewasilishwa baada ya kufanyiwa utafiti wa kina na mashauriano na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu na kwa kutilia maanani mihimili mitatu mikuu ya "Uchumi wa Kusimama Kidete," "Kuwa Mstari wa Mbele katika Uwanja wa Elimu na Teknolojia" na "Kuimarisha na Kutia Nguvu Masuala ya Kiutamaduni."
Kutegemea uwezo wa nguvu-kazi na maliasili pamoja na suhula za ndani ya nchi na fursa pana zinazoletwa na miundombinu iliyopo nchini sambamba na kustafidi vizuri na uongozi na usimamiaji wa kijihadi wa mambo na moyo wa kimapinduzi pamoja na kutegemea vipaumbele vikuu vilivyoainishwa kwenye siasa kuu za kifungu cha 44 cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uchumi wa Kusimama Kidete, Sayansi na Teknolojia, Mfumo mzuri wa kiidara na idadi ya watu katika jamii na muhimu kuliko yote kutegemea na kutawakali kwenye nguvu isiyo na mwisho ya Mwenyezi Mungu Mungu kunaweza kutuwezesha kufanikisha malengo ya Mpango wa Sita wa Taifa wa Maendeleo licha ya kuweko njama nyingi za maadui za kutaka kutuzuia kufanikisha malengo hayo na hatimaye kuweza siasa hizo kutusaidia kuonesha kigezo cha tafakuri ya Kiislamu katika upande wa maendeleo ambayo kiujumla yatakuwa yako huru na yako mbali na mfumo wa kibepari duniani.
Katika kutunga na kupangilia siasa hizo kumefanyika juhudi za kuhakikisha kunazingatiwa uhalisia wa mambo ulivyo katika nyuga za ndani na nje ya nchi na hatimaye kuzaliwa majimui ya siasa kuu ambazo zitakuwa msingi wa Sheria ya Sita ya Miaka Mitano ambacho ni kitu kinachoweza kufanikishwa kikamilifu katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya utekelezaji wake.
Kuchunga na kufanya kwako mambo kwa uangalifu mkubwa wewe na viongozi wengine wa mihimili mitatu mikuu ya dola pamoja na usimamiaji wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kunatufanya tuwe na utulivu wa moyo kuhusu kutekelezwa vizuri siasa hizi kuanzia hatua za kupangiliwa na kuratibiwa kwake hadi kwenye hatua ya utekelezaji wake.
Ni wajibu wangu kutumia fursa hii kushuhuru jitihada za Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, Baraza la Mawaziri, sekraterieti ya halmashauri hiyo na wataalamu amilifu na kila aliyetoa mchango wake katika uandaaji wa majimui hizo pamoja na asasi nyinginezo nchini kwa kazi yao kubwa ya kuratibu na kupanga siasa hizo katika sura na mchakato mpya.
Nakala ya siasa hizo ninaituma kwako sambamba na kwa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Sayyid Ali Khamenei
9/Mwezi Tir/1394 (Hijria Shamsia)
(Juni 30, 2015 Milaadia).
 
 

Bismillahir Rahmanir Rahim
Siasa kuu za Mpango wa Sita wa Taifa wa Maendeleo


- Masuala ya Kiuchumi

1 - Kuhakikisha kunakuweko ustawi wa kasi na wa kudumu wa kiuchumi na wenye kuzalisha nafasi za kazi kwa namna ambayo, iwezekane kunyanyua uchumi huo kwa asilimia nane hadi ifikapo mwisho mwa muda wa utekelezaji wa siasa hizi kupitia kuingizwa katika medani ya kustawisha uchumi, suhula na uwezo wote wa nchi.
2 - Kustawisha kwa sura ya kuendelea anga ya kazi na kutafuta rizki na kutia nguvu muundo wa mashindano na kuufanya uwe na sura kukubali mashindano katika masoko mbali mbali.
3 - Ulazima wa kuweko ushirikishaji mzuri na kustafidi vilivyo na uwezo wa asasi mbali mbali za umma na zisizo za kiserikali na kuzipa nafasi ya kutoa mchango wao kitaifa na zaidi ya kitaifa katika kufanikisha malengo ya uchumi wa kusimama kidete.
4 - Kustawisha na kupanua mifungamano ya kiuchumi na kibiashara ya kanali zinazoingiliana hususan baina ya Iran na nchi za Mashariki ya Kati, za bara la Asia na nchi za Kiarabu za kusini na kuifanya mifungamano hiyo kuwa kambi ya kibiashara ya usafirishaji bidhaa pamoja na kutiwa saini mikataba ya kifedha ya pande mbili na pande kadhaa kwa ajili ya kuimarisha biashara ndani ya kalibu na fremu ya vifungu vya 10. 11, na 12 vya Siasa Kuu za Uchumi wa Kusimama Kidete.
5 - Kupanua na kuimarisha mfumo mpana wa kudhamini fedha na njia zake (soko la fedha, soko la uwekezaji na bima) kwa kuwashirikisha watu wenye sifa za dhati na za kisheria wa ndani na nje na kuongeza hisa yenye taathira nzuri katika soko la uwekezaji kwa shabaha ya kupanua wigo wa uwekezaji na uthabiti na kutoyumba pamoja na kupunguza uwezekano wa kutumbukia kwenye hatari - harakati za kibiashara na kiuchumi za nchi - kupitia kutilia mkazo uongezaji wa kiwango kwa uwazi na usalama wa mfumo wa kifedha nchini.
6 - Kudhamini fedha kwa ajili ya kazi ndogo ndogo na za kati na kati kupitia mfumo wa kibenki.
7 - Kunyanyua kiwango cha ubora na idadi cha mfumo mkuu wa sekta ya bima na njia za kuendeshea sekta hiyo (masoko ya ushindani, bima ya kulinda bima nyinginezo na...) kwa kuwashirikisha watu wenye sifa za dhati na za kisheria wa ndani na nje ya Iran kwa lengo la kustawisha uwekezaji, uthabiti na kutoyumba na kupunguza uwezekano wa kutumbukia katika hatari - harakati za kibiashara na kiuchumi nchini.
8 - Kuvutia uwekezaji wa Wairani walioko nje ya nchi na uwekezaji wa kigeni kupitia kuleta vivutio vizuri na vihamasishaji vinavyotakiwa.
9 - Kufanyika usimamiaji wa kikamilifu na wa pande zote wa Benki Kuu katika soko na taasisi za fedha, benki na za utoaji itibari sambamba na kuandaa asasi na masoko yasiyo chini ya taasisi maalumu ya fedha na mali kwa lengo la kunyanyua uwazi na usalama na kupunguza kiwango cha mahitaji yasiyo ya lazima ya kutaka kurahisishiwa mambo.
10 - Kubadilisha mtazamo wa kutegemea pato la mafuta na gesi kwa ajili ya kudhamini mahitaji ya bajeti ya umma na badala yake kutegemea vyanzo vya uwekezaji na vya uzalishaji wa kiuchumi na kuifanya ya kudumu ajenda ya mfumo wa maendeleo ya taifa kupitia kutekeleza ajenda iliyopo na kuingiza fedha kwa asilimia 30 kila mwaka kutoka katika vyanzo vitokanavyo na usafirishaji nje mafuta ya bidhaa za gesi na gesi asilia kwenye mfumo wa maendeleo ya taifa na kuongeza ndani ya mfumo huo kwa uchache asilimia 2 ya vitu vipya kila mwaka.
10 - 1 - Kutolewa uendeshaji na udhibiti wa hesabu za benki, mikononi mwa Benki Kuu
10 - 2 - Kutolewa vitu vya kusahilisha kazi kutoka katika vyanzo vya Mfumo wa Taifa wa Maendeleo na kupatiwa sekta zisizo za kiserikali kwa sura ya fedha za kigeni.
10 - 3 - Kutohusishwa matumizi ya Mfuko wa Taifa wa Fedha na majukumu ya bajeti na sheria za kawaida za kila siku.
10 - 4 - Kuwekeza akiba ya fedha za kigeni kwa uchache kwa asilimia 20 kutoka katika vyanzo vya kuingia kwenye Mfuko wa Taifa wa Fedha na kupelekwa kwenye benki husika katika mkabala wa kupewa mfuko huo itibari ya sarafu ya Riyal na benki hizo ili mfuko huo uweze kuzipatia visahilishaji vitokanavyo na sarafu ya Riyal - sekta za kilimo, viwanda vidogo vidogo na vya kati na kati na asasi za ushirika zinazotambuliwa na Mfuko wa Taifa wa Fedha.
11 - Kukamilisha silisila ya thamani za sekta ya mafuta na gesi na kupungua kiwango cha nishati.
12 - Kusaidia uanzishaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kuwekeza na kufanya kazi za uvumbuzi (si kwa ajili ya kazi za kumiliki vitu), kustafidi na kupanua medani za mafuta na gesi nchini hususan medani za pamoja ndani ya fremu ya Siasa Kuu za Kifungu cha 44 cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
13 - Kuongeza hisa ya nishati jadidika na mpya na kupanua vinu vya maeneo mbali mbali na vya vipimo vidogo.
14 - Kutekeleza kikamilifu siasa za kutoa ruzuku kwa malengo maalumu kwa ajili ya kuongeza kiwango cha uzalishaji, nafasi za kazi, kutumia vizuri sekta mbali mbali, kupunguza nguvu za nishati na kupandisha juu vielelezo vya uadilifu wa kijamii.
15 - Kukabidhiwa wananchi mipango na miradi ya kukusanya, kudhibiti, kuendesha na kuzalisha gesi na uzalishaji katika medani zote za mafuta na taasisi za sekta ya mafuta.
16 - Kupandisha kiwango cha nyongeza ya thamani ya vitu mbali mbali kupitia kukamilisha silisila ya thamani za sekta za mafuta na gesi na ustawi wa uzalishaji bidhaa zenye kipato kikubwa (kulingana na vielelezo vya kiwango cha matumizi ya nishati).
17 - Kuvifanya viwanda vya daraja za juu na vya daraja la chini vya mafuta na gesi kutegemea elimu msingi pamoja na kuanzisha na kutia nguvu mashirika ya elimu msingi kwa ajili ya kubuni, kufanyia uhandisi, kuunda na kuweka vifaa vinavyohitajika na pia kupeleka teknolojia sehemu zinazotakiwa kwa ajili ya kuongeza kiwango cha kujitosheleza taifa katika uwanja huo.
18 - Kuongeza kwa sura ya kuendelea kiwango cha uzalishaji upya bidhaa na uzalishaji wa mwisho kutoka katika hazina za visima vya mafuta na gesi.
19 - Kugawanya kazi na kuainisha nafasi ya kitaifa kwa kila eneo, mikoa, sehemu na fukwe na visiwa vya nchi kwa kuchunguza mambo ya lazima ya jambo hilo ndani ya fremu ya siasa kuu zinazohusiana na mambo hayo kwa shabaha ya kuongeza kiwango cha uzalishaji wa utajiri wa taifa na uungaji mkono wa serikali kwa sekta ya uwekezaji katika maeneo yenye ustawi mdogo na ya vijijini.
20 - Kutekeleza miradi na kuchukuliwa hatua za utekelezaji kwa ajili ya kustawisha vijiji vya Iran kwa lengo la kudhibiti kuhama wakazi wa maeneo hayo na kushajiisha watu kuhama miji na kuhamia maeneo ya vijijini na kwenye maeneo ya makabila yanayohamahama (kituo kikuu cha uzalishaji na utoaji thamani za kweli) kwa kuweka mipangilio mizuri na kutumia vizuri fursa hiyo katika upeo wa kitaifa, kieneo na kisehemu na kuainisha hisa ya kweli ya kugawanya utajiri na vyanzo vya nchi na kupandisha juu heshima na shani ya kijamii, kuandaa fursa mpya za kiuchumi na kutoa uungaji mkono maalumu kwa harakati za kuzalisha kazi na kuzalisha fursa za kufanya kazi kwa sura inayokubaliana na mila na desturi za ndani na kuimarisha taasisi na miundombinu ya maeneo ya vijijini kwa kusisitizia kifungu cha 9 cha Siasa Kuu za Kilimo nchini.
21 - Kustawisha uchumi wa bahari ya kusini mwa Iran hususan katika maeneo ya Chabahar - Khoramshahr kwa kuzipa umuhimu mkubwa fukwe za Makran.
22 - Kuweka mipangilio mizuri kwa ajili ya kufikia "Uwiano wa Gini" wa 0.34.
23 - Kustawisha masoko ya baharini na kuanzisha maeneo muhimu ya kiuchumi katika mambo yenye faida nzuri.
24 - Kuipa kipaumbele sekta ya njia za reli na kustawisha sekta ya uchukuzi na usafirishaji na kuiletea sekta hiyo fursa na sura ya kuweza kutoa ushindani unaotakiwa.
25 - Kustawisha sekta ya uchukuzi na usafiri wa njia za reli za mizigo kwa kuzipa kipaumbele zana za kanali na vituo vya usafirishaji mizigo na kuziunganisha kanali hizo na vituo vikuu vya kiuchumi, kibiashara na kiviwanda na kuviunganisha vituo muhimu vya kuingiza na kutoa bidhaa nchini na kanali za reli za kieneo na kimataifa hususan ukanda wa kaskazini-kusini kwa lengo la kustawisha usafirishaji nje bidhaa na upitishaji bidhaa.
26 - Kuongeza kiwango cha ukuaji wa ongezeko la thamani ya sekta za viwandani, madini, bidha za madini na kuongeza kiwango cha kusafirisha nje bidhaa zake kupitia utekelezaji wa siasa kuu za viwanda na madini
27 - Kuzifanya mbinu za uzalishaji na bidhaa za viwanda na huduma zinazotokana na bidhaa hizo, kuwa na sura ya elimu msingi, kutoa vielelezo vizuri vya kibiashara na kutia nguvu uwepo wa Iran kwenye masoko ya kieneo na ya kimataifa.
28 - Kuyapa kipaumbele maeneo ya kiistratijia ya masuala ya viwanda (kama vile sekta za mafuta, gesi, petrokemikali, usafirishaji, mada za kisasa, majengo, teknolojia ya habari na mawasiliano, anga za juu, bahari, maji na kilimo) na kuzidisha kiwango cha ushawishi wa teknolojia za kisasa ndani ya vitu hivyo.
29 - Kulipa kipaumbele suala la kudhamini mambo yanayohitajika kwa ajili ya kuimarisha viwanda vya ndani ya nchi kwa kutilia mkazo ukamilishaji wa silisila ya nafasi za ongezeko la thamani za madini na utekelezaji wa kifungu cha 3 cha siasa kuu za madini nchini.
30 - Kutunga na kutekeleza hati kuu ya muongozo na ramani ya njia ya mabadiliko ya mfumo wa uwekaji viwango nchini na kudhibiti ubora wa bidhaa.
31 - Kuweka mfumo mkuu na wenye faida wa takwimu na taarifa nchini.
- Masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano
32 - Kuhakikisha Iran inakuwa na nafasi ya juu katika eneo hili katika ustawi wa mfumo wa serikali ya elektroniki kwa kutumia kanali ya taifa ya mawasiliano na upashaji habari.
33 - Kupanua wigo wa mitandao ya Intaneti kwa kuzingatia ramani ya uhandisi wa kiutamaduni nchini kwa uchache mara tano zaidi ya hali iliyopo hivi sasa na kuifanya mitandao ya kijamii katika Intaneti kuoana na mila na desturi za ndani ya Iran.
34 - Kuanzisha, kukamilisha na kupanua kanali ya taifa ya taarifa na upashaji habari na kudhamini usalama wake, kudhibiti milango ya kuingilia na kutokea kwenye mitandao ya Intaneti, uchujaji wa kiakili mitandano ya Intaneti na kudhibiti vizuri mitandao hiyo, na kutoa utambulisho wa mabadiliko katika vielelezo vya foleni za watumiaji wa mitandao hayo kiasi kwamba asilimia yake 50 iwe ni ya ndani.
35 - Kutumia vizuri nafasi nzuri iliyo nayo Iran hivi sasa kwa shabaha ya kuigeuza nchi hii kuwa kituo kikuu cha mawasiliano ya posta na mitandao na mawasiliano ya kompyuta katika eneo hili sambamba na kupanua wigo wa uwepo wa Iran kwenye masoko ya kimataifa.
36 - Ushiriki wenye taathira na wenye malengo maalumu wa Iran katika miamala ya kimataifa ya mwasiliano ya Intaneti.
37 - Kuongeza kiwango cha hisa ya uwekezaji katika miundombinu kwenye maeneo ya teknolojia ya habari na mawasiliano hadi kufikia kwenye daraja ya nchi zenye kiwango cha juu kwenye suala hilo katika eneo hili.
38 - Kupanua na kustawisha teknolojia ya anga za juu kwa kubuni, kutengeneza, kutoa mafunzo, kurusha hewani na kutumia mitandao ya anga za juu na kulinda daraja ya juu kwa kadiri inavyowezekana kwa ajili ya matumizi hayo kwa kutokea kwenye nukta ya mzingo wa Iran.

- Masuala ya Kijamii
39 - Kuboresha na kustawisha usalama wa kiidara na kiuchumi na kupambana na ufisadi katika uga huo kupitia kubuni mkakati wa kitaifa wa kupambana na ufisadi na kupasishwa sheria kuhusu jambo hilo.
40 - Kuweka mfumo mkuu, ulioshikamana, ulio wazi, wenye manufaa na wenye tabaka kadhaa kwa ajili ya kudhamini usalama wa kijamii nchini.
41 - Kuwatia nguvu na kuwafanya wajitegemee watu wa matabaka na makundi yenye ustawi mchache katika mpango unaohusiana na ustawi wa kijamii.
42 - Kunyanyua ubora na kufanyia marekebisho muundo wa bima za awali za kudhamini usalama wa jamii (ikiwa ni pamoja na bima za matibabu, bima za watu wanaostaafu, bima za walioshindwa kuendelea na kazi na...) kwa ajili ya matabaka yote ya wananchi.
43 - Kuendesha siasa kuu za usalama wa kiafya kupitia kupasisha sheria na kanuni zinazohitajika kwa kusisitizia mambo yafuatayo:
1 - 43 - Kuandaa viambatanisho vya masuala ya usalama wa kiafya kwa ajili ya kutungiwa sheria zinazohusiana navyo na kwa ajili ya mipango mikuu ya ustawi nchini.
2 - 43 - Kufanyiwa marekebisho muundo wa mfumo wa usalama wa kiafya kwa kuzingatia msingi wa kifungu cha 7 cha Siasa Kuu za usalama wa kiafya.
3 - 43 Kudhamini vyanzo vya kudumu vya kifedha kwa ajili ya sekta ya usalama wa kiafya na kupanua wingi na ubora wa bima za afya.
4 - 43 - Kuongeza na kutia nguvu ubora na usalama wa huduma na utunzaji wa pande zote na ulioshikamana wa usalama wa kiafya kwa kutumia kanali ya afya na matibabu inayotabikiana na mfumo wa viwango vilivyoanishwa pamoja na marejeo yake.
44 - Kustawisha mazoezi ya viungo na mazoezi ya watu wote.
45 - Kuanzisha utamaduni na kuandaa uwanja na utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kufanikisha siasa kuu za idadi ya watu.
46 - Kuitia nguvu taasisi ya familia na nafasi ya mwanamke ndani ya familia na kulindwa haki za kisheria na kikanuni za akinamama katika nyuga zote na kuipa mazingatio maalumu nafasi yao muhimu sana katika jamii.
47 - Kuwapa kipaumbele watu wanaojitolea muhanga katika njia ya Mapinduzi ya Kiislamu katika usahilishaji na uwepeseshaji wa mambo wa Serikali katika masuala ya kifedha, utoaji fursa, suhula na majukumu ya kiserikali katika nyuga tofauti za kiutamaduni na kiuchumi
48 - Kuzipa utambulisho maalumu mandhari za miji na vijiji kwa kuzingatia ndani yake ujenzi wa majengo ya Kiislamu - Kiirani.
49 - Kuboresha maeneo ya watu wanaoshi pambizoni mwa miji mikubwa na kuzuia pamoja na kudhibiti madhara ya kijamii yanayotokana na jambo hilo.
50 - Kuleta ustawi wa kudumu katika sekta ya utalii wa ndani ya Iran kwa namna ambayo utalii wa wageni wanaotembelea Iran upandishwe kwa uchache mara tano zaidi ifikapo mwishoni mwa utekelezaji wa Mpango wa Sita wa Maendeleo.
51 - Kuungwa mkono sanaa za mikono na kulindwa turathi za kiutamaduni za nchi.

- Masuala ya Ulinzi na Usalama
52 - Kuongeza uwezo wa kiulinzi katika kiwango cha nguvu za kieneo kwa ajili ya kudhamini manufaa na usalama wa taifa kwa kutenga kwa uchache asilimia 5 ya bajeti kuu ya nchi kwa ajili ya masuala ya ulinzi.
53 - Kunyanyua uwezo wa kuilinda na kuipesha nchi na mashambulizi kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1 - 53 - Kupanua nguvu za makombora na teknolojia pamoja na uwezo wa kuzalisha silaha na zana muhimu za ulinzi wa hali ya juu kwa ajili ya kuzuia kutokea mashambulizi kwa kutumia mbinu zinazonasibiana na kila aina ya vitisho.
2 - 53 - Kupanua kwa njia za kiakili kinga ya ulinzi usio wa kutumia mashambulizi ya kijeshi kwa kutekeleza kikamilifu ulinzi wa namna hiyo katika maeneo nyeti na muhimu sana nchini.
3 - 53 - Kuongezea nguvu uwezo wa programu za kompyuta na ulinzi wa mawasiliano ya kompyuta na kudhamini ulinzi na usalama wa mawasiliano hayo kwa ajili ya miundombinu ya nchi ndani ya kalibu na fremu ya siasa kuu zinazopasishwa.
54 - Kuiboresha na kuiimarisha kiidadi na kiubora Basiji ya wanyonge.
55 - Kuleta udhamini wa kudumu wa usalama wa maeneo ya mipakani kwa kuweka vizuizi kikamilifu kupitia programu na zana za kompyuta sambamba na kupanua na kuvitia nguvu vikosi vya ulinzi wa mipakani, kuwashirikisha katika ulinzi watu wa miji ya maeneo ya mipakani katika mipango ya kiusalama na kazi za kukusanya taarifa za kiusalama pamoja na kutia nguvu udiplomasia ya mipakani.
56 - Kuweka mipangilio mizuri kwa shabaha ya kupunguza vitendo vya uhalifu na jinai kwa lengo la kupunguza kwa asilimia 10 kila mwaka vitendo hivyo.
58 - Kupambana vilivyo na kwa nguvu zote na mihadarati na wafanya magendo wote wa madawa ya kulevya ndani ya fremu ya siasa kuu zinazowasilishwa na kuwarejesha katika hali ya kawaida watumiaji wa madawa hayo kwa shabaha ya kupunguza kwa asilimia 25 ya waathiriwa wa madawa ya kulevya hadi ifikapo mwishoni mwa utekelezaji wa mpango huo.
58 - Kuzuia na kupambana na magendo ya bidhaa na fedha za kigeni kutoka maeneo yanakoanzia magendo hayo, maeneo yanayongilia na hadi sehemu zinakoishia bidhaa za magendo.

- Masuala ya Siasa za Kigeni
59 - Kulinda na kuongeza mafanikio ya kisiasa ya Jamhuri ya Kiislamu katika eneo la Asia ya kusini magharibi
60 - Kuipa kipaumbele diplomasia ya kiuchumi kwa shabaha ya kupanua wigo wa uwekezaji wa kigeni, kuingia katika masoko ya kimataifa na kupata teknolojia ya kufanikishia malengo ya uchumi wa kusimama kidete na hati ya malengo ya maendeleo.
61 - Ustawi wa idadi na ubora wa vyombo vya habari vya nje ya mipaka ya Iran kwa kutumia lugha maarufu kimataifa.
62 - Kuandaa mazingira yanayotakiwa kwa lengo la kuvutia uwekezaji na uwezo wa kielimu na kiutaalamu wa Wairani waishio nje ya nchi katika kuleta ustawi wa kitaifa na kuziathiri siasa za mfumo wa kibeberu katika kulinda manufaa ya taifa.
63 - Kutumuia kwa kadiri inavyowezekana mbinu na njia mpya na za umma za kidiplomasia.

- Masuala ya Sheria na Mahakama
64 - Kuziangalia upya sheria za utoaji hukumu kwa shabaha ya kupunguza hukumu za vifungo na kuzibadilisha kuwa adhabu nyinginezo na kuzifanya adhabu zinazotolewa zioane na makosa yaliyotendeka.
65 - Kuboresha hali za jela na korokoro.
66 - Kuunga mkono na kusaidia uwepo wa mazingira yenye taathira kubwa kwa ajili ya kudhamini haki za umiliki wa mali na kutia nguvu mikataba kwa lengo la kupanua wigo wa uwekezaji katika sekta binafsi na uwekezaji wa kigeni.
67 - Kupanua wigo wa kuorodhesha rasmi hati na nyaraka za milki zikiwemo milki za kimaanawi pamoja na kuandikisha rasmi milki za serikali na za wananchi kwa ajili ya milki za ardhi za nchi kwenye mfumo wa ‘Cadastre' na kueneza teknolojia mpya kwa ajili ya huduma za uorodheshaji na uandikishaji hati na nyaraka.

- Masuala ya kiutamaduni
68 - Juhudi zinazostahiki kwa ajili ya kubainisha thamani za Mapinduzi ya Kiislamu na vita vya kujihami kutakatifu (vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa zamani wa Iraq dhidi ya utawala mchanga wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) na mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu.
69 - Kuonesha na kueneza mtindo wa kimaisha wa Kiislamu - Kiirani na kueneza utamaduni wa kurekebisha kigezo cha matumizi na siasa za uchumi wa kusimama kidete.
70 - Utekelezaji wa ramani ya uhandisi wa kiutamaduni nchini na umuhimu wa kuandaliwa kiambatanisho ya kiutamaduni kwa ajili ya mipango na miradi muhimu.
71 - Kuwaunga mkono kimaada na kimaanawi wasanii, wabunifu, watafiti na wazalishaji wa bidhaa za kiutamaduni na kisanaa zinazotia nguvu maadili mema, utamaduni na utambulisho wa Kiislamu - Kiirani.
72 - Uwepo wenye taathira kubwa wa taasisi za masuala ya kiutamaduni za serikali na za wananchi katika mitandao ya Intaneti kwa sabaha ya kupanua, kukuza na kueneza utamaduni, mafundisho na utambulisho wa Kiislamu - Kiirani na kukabiliana na vitisho vya aina yoyote ile.
73 - Kulipa mazingatio maalumu suala la kuyatia nguvu na kuyadhihirisha kwa uwazi mafundisho, nembo na vielelezo vya Kiislamu - Kiirani katika miundo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi.

- Masuala ya Elimu, Teknolojia na Ubunifu
74 - Kuhakikisha kuwa Iran inafikia daraja ya kwanza katika eneo hili kwenye masuala ya elimu na teknolojia na kuhifadhi na kuilinda daraja hiyo kwa kutilia hima ufanikishaji wa siasa kuu za elimu na teknolojia nchini.
75 - Kutekeleza hati ya mabadiliko ya kimsingi ya Wizara ya Elimu na Malezi na kuzingatia sana vipindi vya masomo vya watoto wadogo na vijana mabarobaro.
76 - Kuongeza hisa za masomo ya utaalamu na ufundi ndani ya mfumo wa masomo nchini.
77 - Kuendeleza na kupanua elimu za kimsingi na utafiti wa masuala ya kimsingi, suala la kutoa fikra na ubunifu katika fremu ya siasa kuu za elimu na teknolojia na kwa kuzingatia ramani kuu ya kielimu nchini.
1 - 77 - Kuandaa mfumo wa taifa wa takwimu na taarifa za kielimu, kiutafiti na teknolojia pana na yenye manufaa.
2 - 77 - Kufanyia mabadiliko na kunyanua viwango vya masomo ya Sayansi ya Kijamii hususan kuzama katika kujifunza na kuelewa mafundisho ya kidini na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu.
78 - Kuandaa mahusiano ya pande mbili baina ya masomo na ufanyaji kazi na kuyafanya yaoane na viwango na aina za masomo nchini kwa kutumia ramani kuu wa kielimu nchini na kwa kuzingatia mahitaji ya kazi na uzalishaji.
79 - Kupanua ushirikiano na kuleta mawasiliano amilifu, madhubuti na yenye taathira kubwa katika sekta ya elimu na teknolojia kati ya Iran na nchi nyinginezo pamoja na vituo vya kielimu na kiufundi vyenye itibari vya kieneo na kimataifa hususan vya ulimwengu wa Kiislamu na kupanua wigo wa biashara na usafirishaji bidhaa na mazalisho yatokanayo na elimu za kimsingi.
80 - Kustawisha na kutia nguvu mfumo wa taifa wa ubunifu na kuunga mkono miradi ya masuala ya kimsingi na kuifanya itoe faida za kibiashara miradi na uvumbuzi huo pamoja na kustawisha mfumo mkuu wa kudhamini fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya uchumi unaotokana na elimu za kimsingi.

 
< Nyuma   Mbele >

^