Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Mabasiji Walioshinda Medali za Olympiad za Kielimu Chapa
26/07/2015
 Majimui ya mabasiji walioshinda medali mbali mbali katika mashindano ya kielimu ya Olympiad ndani ya Iran na ya kimataifa, leo jioni (Jumapili) wameonana na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumkabidhi medali zao.
Katika mkutano huo uliofanyika baada ya Sala za Adhuhuri na Alasiri, mabasiji hao waliotwaa medali kwenye mashindano hayo ya kielimu ya ndani na nje ya Iran katika masomo ya hisabati, fizikia na kompyuta, wamemkabidhi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu medali zao 22 walizoshinda kwenye mashindano hayo.
Kwa upande wake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametumia mkutano huo mfupi kutoa shukrani zake nyingi na za dhati kwa washindi hao wa medali za mashindano ya kielimu akisisitiza kuwa, kupata ushindi kwenye mashindano kama hayo ya kielimu ni ushahidi wa kunawiri maendeleo ya kielimu na vipaji vikubwa vya wana wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa: Dalili na maendeleo hayo ndicho kitu ambacho kinaitwa uwezo na nguvu za kweli za ndani ya nchi.
 
< Nyuma   Mbele >

^