Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Wasimamiaji wa Amali ya Hija Waonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Chapa
22/08/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumamosi) ameonana na wafanyakazi na wasimamiaji wa amali ya Hija na safari za kuelekea katika maeneo matakatifu na kusema kuwa, Hija ni dhamana ya (inadhamini) kuendelea kuweko Uislamu na ni dhihirisho la umoja na adhama ya Umma wa Kiislamu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kusisitiza umuhimu wa kutiliwa maanani masuala ya kijamii na ya mtu binafsi ya ibada kubwa ya Hija amesema kuwa, kuhamisha uzoefu na tajiriba ya umoja wa taifa la Iran katika mkusanyiko mkubwa wa ibada ya Hija kutapelekea kupatikana mshikamano, umoja na nguvu zaidi kwa Umma wa Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria sifa maalumu na isiyo na kifani ya ibada ya Hija ikilinganishwa na faradhi nyingine za Kiislamu na kuongeza kuwa, Hija ina pande mbili tofauti za mtu binafsi na jamii ambapo kuchunga pande zote mbili hizo ni jambo lenye taathira isiyo ya kawaida katika saada (ufanisi) ya dunia na akhera kwa Mahujaji na mataifa ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu amesema kuwa, kuzuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu (al-Kaaba) na kutekeleza ibada ya Hija ni fursa isiyo na mithili kwa ajili ya kutoharisha (kusafisha) roho, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kukusanya na kujipatia faida za kipindi cha umri wote na akawahutubu wanaozuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa kusema, tambueni thamani ya kila amali (kitendo) katika ibada ya Hija na zijishibisheni roho na nyoyo zenu kupitia chemchemi hii ya neema kubwa na safi.
Katika kubainisha upande wa kijamii ya Hija Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameashiria mahudhurio ya mataifa yote yanayotofautiana kimbari, kimadhehebu, kiutamaduni na katika dhahiri yao katika miji ya Makka na Madina na akasema kuwa, Hija ni dhihirisho na fursa halisi ya "Umoja wa Kiislamu."
Kiongozi Muadhamu amewakosoa vikali watu wanaotumia mbinu mbalimbali kudhoofisha hakika na umuhimu wa Umma wa Kiislamu ikiwemo mbinu ya kukuza na kutia chumvi mafuhumu (maana) ya utaifa na akasema kwamba, Hija ni mfano wenye maana wa kuundwa Umma wa Kiislamu na fursa kubwa mno ya kudhihirisha umoja, mshikamano na mfungamano wa Waislamu kote duniani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kudhihirika adhama ya Umma wa Kiislamu na fursa ya kubadilishana tajiriba (uzoefu) kuwa ni nukta nyingine muhimu za upande wa kijamii wa ibada ya Hija na kuongeza kuwa, kubainisha na kuonesha tajiriba zenye sudi na faida kwa mataifa ya Kiislamu ni jambo ambalo huambatana na kuimarika Umma wa Kiislamu.
Kuhusiana na hilo, Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria tajiriba athirifu na yenye utendaji ya taifa la Iran katika kumtambua adui, kutomuamini adui na kutokosea kumfahamu (au kuchagua) rafiki na adui na akaongeza kuwa, "wananchi wetu kwa ufahamu na welewa wa kusifika wamefahamu kwamba, ubeberu wa kimataifa na Uzayuni ndio maadui halisi wa taifa la Iran na Umma wa Kiislamu na ni kwa muktadha huo ndio maana katika mikusanyiko na mijumuiko yote mikubwa ya kitaifa na Kiislamu wamekuwa wakitoa nara dhidi ya Marekani na Uzayuni.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, katika miaka 36 ya hivi karibuni kuna wakati Uistikabari ulikuwa ukilifanyia uadui taifa la Iran kwa ulimi na kwa muamala na nchi nyingine, lakini daima taifa la Iran lilikuwa macho na lilikuwa likifahamu vyema hilo kwamba, nchi hizo zimehadaiwa na zimekuwa zikitumiwa na kwamba, adui wa kweli ni Marekani na Israel.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria tajiriba iliyoshindwa ya kuingia madarakani baadhi ya makundi ya Kiislamu katika baadhi ya nchi na kusema kuwa, makundi hayo kinyume na taifa la Iran yalikosea katika kumtambua na kumuainisha rafiki na adui na wakapata pigo la kukosea kwao huko.
Ayatullah Udhma Khamenei ameutaja umoja kuwa moja ya uzoefu na tajiriba nyingine ya taifa la Iran ambayo inaweza kupatiwa mataifa mengine katika ibada ya Hija na kuongeza kuwa, wananchi wa Iran wameuhifadhi umoja wa kitaifa licha ya kuwa na hitilafu zote za kiitikadi, kifikra na kisiasa pamoja na tofauti za kikaumu na wanatambua vyema nguvu ya neema hii ya Mwenyezi Mungu kwamba, tajiriba hii yenye thamani inapaswa kuhamishwa na kupatiwa mataifa mengine ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mapigano ya ndani katika baadhi ya nchi yanayofanyika kwa kisingizio cha madhehebu, siasa au hata vyama, ni natija ya kutotambua thamani ya ujazi na neema ya umoja na akaongeza kuwa, Mwenyezu Mungu hana uhusiano wa kidugu na taifa lolote lile na kama watu hawatatambua thamani ya umoja na mshikamano basi Allah atawafanya wakumbwe na balaa la hitilafu, mapigano na umwagaji damu.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amekumbusha njama za madhalimu wa kimataifa dhidi ya Uislamu na mfumo wa Kiislamu na kusema kwamba, kimsingi watu hao hawako dhidi ya Ushia au Iran bali wanafanya njama dhidi ya Qur'ani; kwani wanatambua Qur'ani na Uislamu ni kitovu cha kuleta mwamko wa mataifa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ushahidi wa njama zisizokoma (za kuendelea) za mabeberu zenye lengo la kupata njia tofauti za kupenya na kutoa pigo kwa Waislamu na kuongeza kuwa, kwa himaya ya kifedha yenye kuendelea ya Uistikbari, kuna makumi ya vituo vya kifikra na kisiasa huko Marekani, Ulaya, Palestina inayokaliwa kwa mabavu na nchi zinazofungamana nao, vituo ambavyo viko katika hali ya kudurusu na kufanya uchunguzi kuhusiana na Uislamu na Ushia ili viweze kupata njia ya kukabiliana na sababu zinazopelekea kupatikana mwamko na nguvu za Umma wa Kiislamu. Na baada ya kupata njia hizo viweze kuanzisha operesheni za kukabiliana na masuala hayo.
Ameongeza kuwa, watumaiji mabavu wa kimataifa wanalifuatilia kwa umakini mkubwa suala la kuzusha utumiaji mabavu na mifarakano kwa jina la Uislamu na wanafanya hima kubwa ya kuichafua dini tukufu ya Kiislamu na hivyo kuyagombanisha mataifa ya Kiislamu na hata kuzusha vita na mapigano baina ya taifa moja ili kwa njia hiyo waudhoofishe Umma wa Kiislamu. Pamoja na hayo, hatua ya Iran ya kuhamisha uzoefu na tajiriba yake ya kuleta umoja na kumtambua adui kwa mataifa mengine katika ibada ya Hija inaweza kusambaratisha njama hizi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa, tab'ani uhamishaji wa tajiriba yenye faida ya mataifa baina yao katika ibada ya Hija una upinzani, lakini pamoja na hayo kuna haja ya kupata njia ya (kufikia) hilo.
Mwishoni mwa hotuba yake Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameashiria tena ulazima wa kuzingatiwa kwa pamoja upande wa ibada ya Hija kwa mtu binafsi na wa kijamii na kusisitiza kwamba, isije Mahujaji wapendwa wakatumia kimakosa fursa isiyo na kifani ya kuweko kwao katika mji wenye uturi wa Makka na kuwa na mahudhurio ya kiibada na yenye shauku huko Makka na katika nyumba ya Mwenyezi Mungu na wakaipoteza fursa hiyo kwa kutembea na kurandaranda katika masoko na kununua vitu na wakaijutia katika umri wao wote fursa hiyo isiyo na mithili na yenye nishati ya kuweko katika Masjd al Haraam na Masjdu an-Nabawi.
Aidha katika hotuba yake hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, kufanya juhudi kwa ajili ya kufanya ibada ya Hija ni majukumu mazuri zaidi na yanayopendeza kabisa ambapo sanjari na kuwashukuru maafisa na wasimamizi wa ibada ya Hija kutokana na juhudi kubwa wanazofanya katika uwanja huo ameongeza kwa kusema kuwa, " tumieni nguvu na uwezo wenu wote kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, ibada ya Hija inafanyika kwa njia matulubu na inayotakiwa."
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Hujjatul Islam Walmuslimin Kadhi Askari, Mwakilishi wa Fakihi Mtawala na Msimamiaji wa Mahujaji wa Kiirani sambamba na kutoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa Kumi la Ukarimu amesema kuwa, nara ya Hija ya mwaka huu ni " Hija, umaanawi, muono wa mbali na mshikamano wa Kiislamu" na kusema kuwa, kuandaliwa mikakati kumi na mipango aali ya Hija, kuinua kiwango cha welewa cha nguvu kazi, kutoa mafunzo ya kimaarifa (welewa) kwa ajili ya mahujaji na viongozi wa kidini wa misafara ya mahujaji, kuandaliwa vikao vya kielimu na kutumia uwezo wa mahujaji na wafanyaziara na wasimizi wao ni miongoni mwa harakati ma utendaji katika kutekeleza ibada ya Hija. Mwakilishi wa Fakihi Mtawala na Msimamiaji wa Mahujaji wa Kiirani ameongeza kuwa, Hija ya mwaka huu sambamba na kupaswa kulinda izza na utukufu wa taifa la Iran inapaswa pia kubadilishwa na kuwa kituo cha umoja wa Waislamu ulimwenguni.
Naye Bw. Awhadi, Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kutoa ripoti kuhusiana na kazi za taasisi hiyo, amezungumzia kuhusu kuwa rahisi mwenendo wa uandikishaji mahujaji na mazuwwar (wafanyaziara) na kubainisha kwamba, kutumwa asilimia 62 ya wafanyaziara kwa ndege ya moja kwa moja kuelekea Madina, kuandaa aina kwa aina ya mipango ya chakula, kudhamini sehemu kubwa vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya wafanyaziara kutoka ndani ya nchi na kupungua kwa gharama na huduma za ufikishaji habari ni miongoni mwa mipango ya Taasisi ya Hija na Ziara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kufanya marasimu ya ibada ya Hija mwaka huu na akaongeza kuwa, makaridio ya lazima yamefanyika kwa ajili ya kupelekwa mahujaji elfu 64 wa Kiirani katika kalibu ya misafara 455.
Vile vile kabla ya kuanza mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitembelea maonyesho ya picha na vitabu maalumu vya Hija
 
< Nyuma   Mbele >

^