Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais na Baraza la Mawaziri Chapa
27/08/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na Rais pamoja na wajumbe wa Baraza la Mawaziri la serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuitaja falsafa ya kupewa siku za kumbukumbu ya mashahidi Rajai na Bahonar jina la "Wiki ya Serikali" kwamba, ni kubakisha hai vigezo vya kifikra, kimuamala na vya kishakhsia vya mashahidi hao wawili azizi, ambapo sambamba na kupongeza juhudi za serikali hususan katika uga wa kupunguza ughali (ugumu) wa maisha, kuleta utulivu na uthabiti wa kiuchumi, afya na kumalizika mazungumzo ya nyuklia na kusisitiza kuwa, katika mwenendo wa harakati jumla ya nchi ni "kuzingatia kikamilifu kuendelea kwa uadui wa maadui, kuwa macho mkabala na upenyaji wa wageni, kujiepusha na mambo ya kando (yasiyo na umuhimu), kulindwa kasi ya kielimu, kuweko usimamiaji wa uga wa utamaduni kwa misingi na nara za Imam (Imam Khomeini) na mapinduzi, kuzingatiwa uadilifu katika njia ya maendeleo na ustawi, usimamiaji wa jaddi kwa wafanyabiashara wa kigeni, kuandaliwa mipango imara na yenye jedwali kwa ajili ya kupatikana uchumi wa kimuqawama" kuwa ni mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa kikamilifu na viongozi.
Katika mkutano huo uliofanyika kwa mnasaba wa Wiki ya Serikali, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kutoa mkono wa kheri, baraka na fanaka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ali bin Mussa ar-Ridha (as) amekutaja kusadifiana kumbukumbu hiyo na Wiki ya Serikali kuwa ni jambo lenye baraka na kuongeza kwamba, kuweko haram tukufu ya Imam wa Nane Imam Ridha (as) nchini Iran ni miongoni mwa fakhari kubwa za nchi hii na kwamba, inapaswa kufanyika juhudi kubwa kadiri inavyowezekana katika kuadhimisha siku hii.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei sanjari na kuadhimisha na kukumbuka utajo wa mashahidi Rajai na Bahonar (Rais na Waziri Mkuu wa zamani wa Iran) amesisitiza kuwa, moja ya malengo ya kupatiwa jina Wiki ya Serikali katika masiku haya ni kutaka kutoa vigezo kwa sifa na miamala ya kiakhlaqi vya mashahidi wa serikali.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kuamini malengo ya Imam Khomeini (ra), ikhlasi, kuwa na moyo wa kuhudumia, viongozi kuwa miongoni mwa wananchi (kuishi kama wananchi, kukaa na kuwa na mdakhala na wananchi), viongozi kutotumia cheo na masuuliya waliyonayo kama wenzo wa kujidhaminia utajiri wa mustakbali wao na kufungamana na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu ni miongioni mwa sifa za dhahiri za mashahidi Rajai na Bahonar na kubainisha kwamba, viongozi (wa serikali) wanapaswa kufahamu kwamba, muamala, maisha na mahusiano yao katika jamii yanajenga utamaduni.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu baada ya kubainisha utangulizi huo, ametoa shukurani na pongezi kwa juhudi za Rais na baraza lake la mawaziri katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ambapo sambamba na kuashiria ripoti mbalimbali za mawaziri katika mkutano huo ameongeza kuwa, ripoti zilizobainishwa leo zilikuwa nzuri na zenye kufaa na kwamba, zinapaswa kuwafikia wananchi.
Wakati huo huo, Ayatullah Udhma Khamenei ametanabahisha pia nukta hii kwamba, ripoti za maafisa wa serikali zinapaswa kuwa kwa namna ambayo wananchi wazisadikishe kwa kuzingatia uhakika na ukweli wa maisha yao.
Katika kuendelea na matamshi yake, Kiongozi Muadhamu ameashiria baadhi ya hatua chanya zilizochukuliwa na serikali na kusema, kupungua ughali wa maisha, kuweko utulivu na uthabiti wa kiwango fulani katika uga wa kiuchumi na kupunguza hali ya kasi ya panda shuka, ni moja ya hatua nzuri zilizochukuliwa na serikali na ambazo zinapaswa kuendelea.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwamba, haturidhii kuona mfumuko wa bei na ughali wa gharama za maisha zikifikia tarakimu mbili na mfumuko huo kwa kila mwaka unapaswa kuwa chini ya asilimia kumi.." Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, juhudi za serikali za kuondokana na hali ya kudorora uchumi (mkwamo wa kiuchumi), kuleta mpango wa mabadiliko katika afya, kuandaa ratiba ya ya kuendeleza harakati ya kielimu hapa nchini na kufanya juhudi kwa ajili ya kusimamia matumizi ya maji katika sekta ya kilimo na mipango ya umwagaliaji ni miongoni mwa hatua nzuri zilizochukuliwa na serikali ambapo sanjari na kuashiria suala la nishati ya nyuklia amesema kwamba, kufikisha mwisho mazungumzo ya nyuklia ni moja ya kazi muhimu sana ambazo zimefanyika na tuna matumaini kwamba, kama katika uwanja huu kutakuwa na baadhi ya mambo na matatizo basi yapatiwe ufumbuzi.
Wakati huo huo, kuhusiana na suala la nishati ya nyuklia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kuweko uwezekano wa kupuuzwa malengo ya maadui ni miongoni mwa wasiwasi na daghadagha zake na kusisitiza kuwa, tangu mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu hadi leo, uadui wa Wazayuni na Wamarekani kwa Mapinduzi na Jamhuri ya Kiislamu haujapungua na huu ni uhakika na ukweli ambapo katu haujafifia katika fikra na viongozi.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa, tab'ani, yamkini mbinu na mikakati ya uadui kwa ajili ya kutoa pigo inawezekana ikawa mipya, lakini viongozi (na maafisa serikali) wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wanapaswa kuzingatia suala hili kwamba, katu hawapaswi kutumbukia katika mipango iliyoandaliwa na adui na maamuzi yao kwa kukusudia au bila kukusudia ikasaidia kutekeleza mipango ya wageni.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, malengo ya kiadui na bayana ya maadui yanaweza kudirikiwa vyema katika maneno na maandishi yao na hakuna mtu anayepaswa kusahau kwamba, kambi ya adui imesimama ikiwa imejindaa na silaha kwa ajili ya kukabiliana na wananchi na taifa hili na sisi tunapaswa kujizatiti na kujiandaa na kuchukua maamuzi kwa makini kulingana na hali ilivyo kwa ajili ya kukabiliana na maadui.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa, tab'ani udharura wa kudiriki uadui usio na mwisho wa Wazayuni na Wamarekani sio jambo ambalo linawahusu viongozi peke yao, bali wananchi hususan wale ambao wana uchungu na mapinduzi wanapaswa kuuzingatia ukweli huu. Hata hivyo jukumu la viongozi katika uwanja huu ni kubwa zaidi.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kuwa macho mkabala na njama za adui za upenyaji tata wa adui na za hatua kwa hatua kwamba, ni jambo la dharura na kusisitiza kwamba, kuna ulazima wa kuwa wazi katika uchukuaji misimamo ya Kimapinduzi katika mazingira yoyote yale tena bila ya kuoneana muhali. Katika kukabiliana na adui misimamo ya mapinduzi na misingi ya Imam Khomeini (MA) inapaswa kubainishwa bila ya woga wala aibu.
Ametanabahisha kuwa, kama kutakuwa na hali ya kughafilika (mghafala) ghafla tutaona kuwa, adui ameshaingia na anajishughulisha na shughuli hatari za kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa; hivyo basi kwa muktadha huo kuna haja ya kuwa makini kikamilifu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kulindwa umoja na mshikamano wa wananchi kuwa ni dharura nyingine na kuongeza kuwa, hata katika maandamano ya 22 Bahman pia (ambayo hufanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu), wananchi wote hawako sawa na hawatoki katika mrengo na kundi moja, lakini muelekeo wao ni mmoja hivyo basi kuna haja ya kulindwa kikamilifu umoja na muelekeo mmoja uliopo katika jamii.
Kuhusiana na jambo hilo ameongeza kuwa, ili kulinda umoja na mshikamano wa jamii, kuna ulazima wa kujiweka mbali na kuzusha mambo ya pembeni (yasiyo na umuhimu) na ufarakishanaji na kutotamka neno au kutoa matamshi ambayo yanatia dosari umoja.
Katika kubainisha mambo ambayo yanapaswa kupewa kipaumbeke katika kipindi cha hivi sasa, Ayatullah Udhma Khamenei ametilia mkazo suala la kulindwa kasi ya maendeleo ya kielimu hapa nchini na kubainisha kwamba, elimu ni muundo msingi wa kweli wa ustawi wa nchi na kila hatua ambayo itachukuliwa katika uwanja huu ni uwekezaji kitega uchumi kwa ajili ya mustakbali wa Iran.
Ameongeza kuwa, kunapaswa kufanyika juhudi na kuandaliwa mipango ili kasi ya elimu katika muongo wa pili wa mpango wa maendeleo ilindwe na Inshallah tuweze kuingia katika kundi la nchi kumi duniani ambazo zinashikilia nafasi za juu za kielimu ulimwenguni.
Kiongozi Muadhamu wa Mpainduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kubadilishwa harakati ya kielimu na kuwa gumzo la umma katika muongo mmoja uliopita ni jambo ambalo limedhamini ukuaji wa kielimu na kuongeza kuwa, mazunguzmo haya yenye kuleta nishati na kuchochea yanapaswa kulindwa na kuimarishwa.
Ameongeza kuwa, kuegemea mashirika yenye misingi ya kielimu na vituo vya elimu na teknolojia ni jambo la dharura na ambalo linazalisha nafasi za ajira na kuongeza kuwa, pangeni mipango na kuandaa mikakati kwa namna ambayo wanachuo wa viwango mbalimbali vya masomo wataweza kuingia katika soko la ajira na kupata kazi.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali khamenei Khamenei amesema kuwa utamaduni ni kipaumbele kingine katika kipindi cha sasa na kuongeza kuwa, matatizo ya kiuchumi hayaparaganyishi fikra lakini matatizo ya kiutamaduni wakati mwingine humnyima mtu usingizi. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa uzalishaji wa bidhaa zinazofaa za kiutamaduni na kuzuia uzalishaji wa bidhaa zenye madhara ya kiutamaduni ni nyadhifa mbili kuu za viongozi wa serikali. Ameongeza kuwa, katika nchi zote duniani kuna usimamizi wa masuala ya kiutamaduni, kwa msingi huo kama baadhi ya bidhaa hizo- sawa ziwe za maonyesho (filamu na kadhalika) au za maandishi- zinapingana na misingi na sheria, zizuiyeni bila ya kuona haya. Amepinga suala la kuachiwa hivihivi (bila ya mipaka) sekta ya utamaduni na kusema: Medani ya utamaduni inapaswa kusimamiwa kwa mujibu wa misingi na kaulimbiu za Imam Khomeini na Mapinduzi ya Kiislamu na zizalishwe bidhaa salama za kiutamaduni kwa ajili ya jamii.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja uchumi kuwa ni jambo linalopaswa kupewa kipaumbele zaidi hapa nchini na akabainisha nukta kadhaa katika uwanja huu ambapo nukta ya kwanza ilikuwa ni kuweko maendeleo yanayokwenda sambamba na uadilifu. Ameongeza kuwa, kuna haja ya kuwa makini katika harakati ya uchumi ili isije kukatokea tofauti ya kimatabaka na haki za masikini zisipotee.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kubadilishwa kazi na juhudi kuwa mazungumzo ya umma (gumzo) na kubadilishwa uvivu na kukaa bila kazi na kufanywa kuwa jambo baya na linachukiza katika utamaduni wa jamii ni miongoni mwa nukta muhimu katika mipango na hatua na akaongeza kuwa, sambamba na kushajiisha na kutangaza ujasiriamali na kuzalisha utajiri katika nchi, kuna haja pia ya kuletwa njia sahihi ya kazi na hilo kuwekwa katika mipango na wakati huo huo kuonyeshwa wananchi njia za kutafuta kazi katika vyombo vya habari ambapo baadhi ya vipindi vya televisheni vimefanya kazi nzuri katika hili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ameashiria uwezo mkubwa wa nchi katika kufikia ukuaji wa kiuchumi wa juu na kueleza kwamba, suala la kusimamia wafanyabiashara wa kigeni ni muhimu. Amesisitiza pia juu ya suala la mabadilishano na biashara ya uadilifu na kutoibadilisha Iran na kuwa soko la bidhaa za kigeni.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la uchumi wa kimuqawama kuwa ni jambo muhimu ambalo linapaswa kuzingatiwa na serikali katika kila mpango.
Kiongozi Muadhamu ametoa shukurani zake kwa ripoti za vyombo vya serikali katika uwanja huo lakini akasema, baadhi ya kazi zilizofanyika ni utangulizi, baadhi ya nyingine hazihusiani na uchumi wa kimuqawama na huku baadhi ya kazi nyingine zikiwa ni kazi ya vyombo vya serikali ambazo ni katika harakati za uchumi wa kimuqawama.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amekumbusha kwamba, uchumi wa kimuqawama ni kifurushi kamili na chenye mfungamano na ni matokeo yaa akili ya pamoja na kwa ajili kufikiwa hilo, kuna haja ya kuweko ratiba ya utekelezaji na operesheni yenye mfungamano.
Ameongeza kluwa, katika mpango huu hisa ya utendaji wa kila chombo inapaswa kuainishwa na kuwekewa jedwali (ratiba) na kuweko na harakati ya vyombo (maalumu) vya kufuatilia kuondolewa matatizo na vikwazo vilivyoko katika uwanja huo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, baada ya kuandaliwa mipango hiyo ya utekelezaji, hatua ya pili katika kupatikana uchumi wa kimuqawama ni kuundwa kamati imara ya uongozi, yenye umahiri na utekelezaji ili kwa uwezo wake zichukuliwe hatua za haraka kwa ajili ya kutatua matatizo na kuchukuliwa maamuzi sahihi na ya wakati unaofaa na hivyo kuandaliwa uwanja na mazingira ya kutekelezwa mipango hiyo na kisha wananchi kupatiwa ripoti (juu ya kinachoendelea).
Ayatullah Udhma Khamenei amewasisitizia viongozi wa serikali kwa kuwaambia, msiweke katika ratiba mpango wowote ule wa kiuchumi ambao hauoani na sera za uchumi wa kimuqawama na andaeni haraka mpango wa sita wa ustawi na uwe kwa mujibu wa msingi huu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitathmini suala la kutumia uwezo wa sekta isiyo ya serikali (sekta binafsi) na kunufaika na wana uchumi na wanaharakati wa masuala ya kiuchumi kwa ajili ya kupatikana uchumi wa kimuqawama kuwa ni jambo la dharura.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, amebainisha kwamba, endapo utekelezaji wa sera na siasa za uchumi wa kimuqawama unahitajia mashiko ya kisheria na kimahakama, Bunge na Chombo cha Mahakama viko tayari kutoa ushirikiano huo.
Kiongozi Muadhamu ameashiria suala la uzorotaji pamoja na ripoti ya Rais ya kuweko ukuaji uchumi kwa asilimia tatu na kusema, ukuaji huu unaonyesha kuweko mabadiliko madogo katika kuzoroza (uchumi), lakini kama suala hilo la kuzorota uchumi halitapigwa vita kikwelikweli, ukuaji huu wa sasa nao utakabaliwa na hatari na ughali wa maisha utachukua mkondo wa kuongezeka.
Kiongozi Muaadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria vituo vya kiuchumi ambavyo kutokana na uzorotaji huo vimekabiliwa na matatizo na kuongeza kuwa, baadhi ya vituo hivyo vya uzalishaji vina matatizo ya fedha taslimu ambapo Benki inapaswa kuingia katika medani hii. Lakini baadhi ya vituo hivyo havina matatizo ya fedha taslimu na vimeshapata mambo ya kuvirahisishia shughuli zake, lakini vimechukua suhula hizo na kuzitumia katika mambo mengine ambapo katika hili kuna haja ya kuchukuliwa hatua mwafaka.
Ayatullah Udhma Khamenei amebainisha kuwa, ili kutatua tatizo la uzorotaji, baadhi ya mipango inapaswa kukabidhiwa kwa sekta binafsi. Ameashiria baadhi ya takwimu zinazohusiana na kuweko mpango wenye thamani ya bilioni laki nne Tomani ambao haujakamilika na kuongeza kuwa, endapo asilimia kumi ya mipango hiyo itakabidhiwa kwa sekta binafsi, basi bilioni 40 Tomani zitaingia katika mzunguko wa kiuchumi wa nchi na kuwa na taathira muhimu katika kuondoa uzorotaji.
Kisha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria juu ya ulazima wa kuzingatiwa zaidi sekta ya kilimo ambapo sambamba na kusisitiza juu ya kuweko mipango kwa ajili ya kujitosheleza katika bidhaa za kimsingi na kusema, ni lazima sambamba na kustafidi na teknolojia ya kisasa katika kilimo kutumike na kustafidi pia na uwezo wa wahandisi na wataalamu vijana wa kilimo katika mikoa mbalimbali (hapa nchini).
Ayatullah Udhmaa Khamenei amelitaja suala la kuzuia uingizaji wa matunda kiholela na kwa tamaa kuwa muhimu na kutanabahisha kwamba, kuna haja ya kutilia mkazo wa hali ya juu vijiji na viwanda na kustafidi na uwezo wa viwanda vya vijijini.
Kiongozi Muadhamu ameitaja sekta ya madini kuwa muhimu kwa nchi na kusema, soko la mafuta huporomoka kutoka dola mia moja kwa pia na kuwa dola 40 kwa ishara moja tu ya madola makubwa na kufuatiwa na hatua za makhabithi wa Mashariki ya Kati na katu si ya kutegemea, hivyo tuna haja ya kufikiria jambo jingine litakalochukua nafasi yake ambapo sekta ya madini ni mbadala bora kabisa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, katika suala la madini kuna haja ya kustafidi na uwezo wa sekta binafsi na lizuiwe suala la kuuzwa mali ghafi.
Kiongozi Muadhamu amezungumzia suala la maji na utumiaji mzuri kuhusu hilo na kurekebishwa umwagiliaji wa kilimo kuwa nalo ni muhimu.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Rais Hassan Rouhani alitoa ripoti kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na serikali katika nyanja mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Rais Roouhani alisema kuwa, kuleta utulivu katika anga ya kiuchumi na kijamii hapa nchini kwamba, ni matunda makubwa na rasilimali muhimu ya serikali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na akasema kwamba, serikali imefanya kila iwezalo ili iweze kutekeleza kivitendo ahadi ilizotoa likiwemo suala la kupunguza kiwango cha ughali wa maisha wa hatua kwa hatua na kukifisha asilimia 11.5 na kiwango cha ughali wa maisha wa miezi kumi na mbili (mwaka mmoja) kukifikisha kwa asilimia 13.8.
Bwana Rouhani amesema kuwa, kuondokana na uzorotaji (wa kiuchumi) ni moja ya hatua zilizochukuliwa na serikali kwa ajili ya kutekeleza ahadi zake na kuongeza kuwa, kuondoka katika ukuaji hasi wa uchumi na kufikia kiwango cha ukuaji uchumi chanya wa +3 katika mwaka wa Kiirani (1393) ni ishara ya wazi ya kuondokana na uzorotaji huo na ni matumaini yetu kwamba, mwaka huu pia ukuaji chanya wa kiuchumi utaendelea.
Rais Hassan Rouhani sambamba na kusisitiza hatua ya serikali ya kulipa umuhimu suala la utekelezaji wa sera za uchumi wa kimuqawama amesema kuwa, kuongeza kwa asilimia 19 usafirishaji nje ya nchi bidhaa zisizo za mafuta na kuleta uwiano wa kiwango fulani baina ya uingizaji bidhaa na usafirishaji ni miongoni mwa dalili za kufanya harakati katika njia ya uchumi wa kimuqawama na kusema kwamba, tab'ani, serikali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ilikabiliwa na changamoto na vizingiti vikubwa ambapo moja ya hayo ni utoaji wa ruzuku kwa fedha taslimu.
Bwana Hassan Rouhani amesema kuwa, kuheshimiwa haki za kiraia na kuheshimiwa haki za kaumu zote na dini zao ni hatua nyingine zilizochukuliwa na serikali ambapo sanjari na kuashiria nafasi ya 16 ya kielimu ya Iran duniani ameongeza kwamba, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumeanzishwa mfuko wa uvumbuzi na uchanuaji vipaji (ustawi) na kwamba, mwaka huu kuna kiasi cha tomani bilioni 1,500 ambazo yatapatiwa mkopo mashirika ya kielimu.
Kuhusiana na utendaji wa serikali ya awamu ya 11 katika suala la siasa za kigeni, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kufikiwa makubaliano ya nyuklia kwa miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni matunda muhimu katika uga huo na kubainisha kwamba, timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran hakuna wakati ambao ilizembea, bali ilikuwa huru na ilikuwa na ushujaa katika kutetea manufaa ya kitaifa, izza ya kitaifa na uwezo wa kiulinzi wa taifa hili na kwa hakika imefanya kazi kubwa katika uwanja huo.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kulindwa teknolojia ya nyuklia, kufutwa maazimio ya hapo kabla ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, kuondolewa vikwazo vya kifedha na kiuchumi baada ya kutekelezwa makubaliano na kuondolewa faili la Iran katika Baraza la Usalama katika miaka kumi ijayo, ni miongoni mwa matunda ya mazungumzo ya nyuklia.
Vile vile Rais Hassan Rouhani ameashiria hatua za serikali ya awamu ya 11 katika uga wa kiutamaduni, kijamii na afya, kuitisha uchaguzi wa Bunge na Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu na Kusimamia Kazi Zake katika mwezi wa Isfand mwaka huu (kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia) na kubainisha kwamba, hayo ni mambo muhimu ambayo yanaikabili serikali hapo mbeleni na kuongeza kwamba, serikali inajitambua kwamba, ni yenye kufungamana na sheria na inaziheshimu asasi zote zinazofungamana na uchaguzi.
Katika mkutano huo, baada ya hotuba fupi ya Bwana Jahangiri Makamu wa Kwanza wa Rais, Bwana Mohammad Reza Nematzadeh, Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara naye alitoa ripoti ya shughuli na kazi za wizara yake na kubainisha ukuaji wa asilimia 6.7 katika uga wa viwanda na kuongezeka uwekezaji vitega uchumi na vile vile kukua kwa asilimia 19 ya usafirishaji bidhaa zisizo za mafuta na kusema kuwa, serikali imepiga marufuku uingizaji wa magari aina ya Lexus na imewekea mipaka uingizaji wa bidhaa zisizo za dharura na kwamba, kumefanyika juhudi za kuhakikisha kwamba, bidhaa zonazotakiwa na vyombo vya serikali vinadhaminiwa hapa hapa nchini.
Kukombolewa asilimia 80 ya ardhi za nchi katika uwanja wa madini kwa ajili ya kugunduliwa na kukamilisha uzalishaji wa madini ni mafanikio mengine mawili ya Wizara ya Viwanda, Madini na Biashara ambayo yaliashiriwa na Bwana Nematzadeh.
Bwana Hamid Chitchian Waziri wa Nishati naye alitoa ripoti kuhusiana na utendaji wa wizara yake na kubainisha kwamba, changamoto kubwa ya wizara hiyo ni tofauti ya kipato na gharama na mrundiko wa madeni, ukame, mabadiliko ya hali ya hewa na kuchukuliwa kusiko na mpangilio na kuliko kinyume na sheria kwa vyanzo vya utajiri vya ardhini na kueleza kwamba, kubadilishwa muelekeo na kuweko usimamizi wa matumizi na usimamiaji wa pamoja wa vyanzo vya maji sambamba na kuandaliwa vikao vya Baraza Kuu la Maji na kupunguzwa matatizo ya kijamii katika uwanja wa suala la maji ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Nishati katika uga wa suala la maji.
Waziri wa Nishati ameongeza kuwa, kustafidi na vituo 29 vya nishati vyenye uwezo wa (kutoa) zaidi ya megawati 4,000, kuandaliwa mipango ya kupunguza hasara za vituo vya usambazaji, kustafidi na asilimia 17 ya teknolojia mpya katika sekta ya umeme kwa kutegemea uwezo wa hapa ndani, kusafirisha nje huduma za kitaalamu na kiuhandisi zenye thamani ya dola bilioni 3.8 ni miongoni mwa harakati na kazi zilizofanywa na Wizara ya Nishati katika uga wa umeme.
Kwa upande wake Waziri wa Mafuta ameitaja mipango ya serikali katika medani za pamoja (za mafuta) kuwa ni kuongeza uzalishaji na kusema kuwa, katika medani za pamoja za mafuta, kiwango cha uzalishaji kimetoka mapipa elfu sabini na kufikia laki moja kwa mwaka huu na kwamba, kufikia mwaka ujao (1395 Hijria Shamsia) kiwango hicho kitafikia mapipa laki mbili na sitini elfu.
Bwana Bijan Namdar Zangeneh ameashiria ongezeko la asilimia 12 la uzalishaji gesi katika mwaka uliopita (wa 1393 Hijria Shamsia) na kuongeza kuwa, kukamilika kwa awamu 25 kati ya awamu 27 huko Pars Kusini mpaka mwishoni mwa muhula wa serikali na kuzifikishia familia milioni mbili na nusu huduma ya gesi ni miongoni mwa mipango ya Wizara ya Mafuta mpaka mwishoni mwa muhula wa serikali.
Waziri wa Mafuta ameashiria pia ongezeko la asilimia 15 la usafirishaji mafuta katika miezi minne ya awali ya mwaka huu ikilinganishwa na muda kama huo mwaka uliopita na kusema kuwa, sekta ya mafuta ilikuwa moja ya sehemu kuu zilizokuwa zikilengwa na vikwazo vya maadui, lakini pamoja na hayo tumeweza kusukuma mbele na kwa nguvu zote mipango na mikakati yetu katika mazingira kama haya.
Bwana Mahmoud Hojjati, Waziri wa Jihadi ya Kilimo naye ametoa ripoti kuhusiana na wizara yake na kuashiria kusimamisha mwenendo wa kupunguza misitu kaskazini (mwa nchi) na kupunguza mashinikizo kwa mbuga na mimea na kuongeza kuwa, katika sekta ya uzalishaji na kilimo cha umwagiliaji, ratiba na mipango ya serikali ni kueneza utamaduni na kuwashajiisha wananchi wapunguze kutumia ovyo vyanzo vya maji, kupunguza matumizi ya maji kwa kueneza mfumo mpya wa umwagiliaji na kuongeza kilimo cha nyumba za vioo (ya kuhifadhi mimea). Waziri wa Afya, tiba na Mafunzo ya Udaktari alikuwa waziri wa mwisho ambaye alisimama na kutoa ripoti ya wizara yake.
Bwana Hassan Ghazizadeh Hashem amezungumzia suala la kuweko ukuaji wa kielimu katika sekta ya afya na tiba na kulipwa madeni katika sekta ya afya, kuongezeka mwenendo wa wananchi kupata dawa sambamba na kupungua uingizaji wa dawa hizo kutoka nje na kusema kuwa, katika hali ya hivi sasa madaktari wanatoa huduma katika vituo vyote vya afyt katika miji yenye idadi ya wakazi walio chini ya elfu ishirini.
Ghazizadeh Hashemi amesema, kuandaliwa huduma za afya kwa ajili ya wakazi wa maeneo ya mbali (kando kando yaliyo mbali na huduma), kupunguzwa gharama za matibabu, vifaa na suhula za kitiba na kupatiwa bima watu milioni 10 ni miongoni mwa huduma nyingine zilizotolewa na Wizara ya Afya na kuongeza kwamba, kuna madaktari wataalamu elfu nne katika maeneo mbalimbali ya nchi ambao wanaendelea na shughuli zao na wananchi walioko katika maeneo ya mbali (yasiyo na huduma muhimu) na ya mpakani, wanaweza kuwapata na kuwafikia madaktari hao mabingwa.
Mwishoni mwa mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Khamenei, amewasalisha hadhirina Sala za Adhuhuri na Alasiri.

 

 
< Nyuma   Mbele >

^