Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Amirijeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran Aonana na Maafisa wa Kituo cha Ulinzi wa Anga Chapa
01/09/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo adhuhuri (Jumanne) ameonana na makamanda na maafisa wa kituo cha ulinzi wa anga cha Khatamul Anbiya SAW cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na huku akiashiria umuhimu wa kutekelezwa vilivyo majukumu na kazi za kituo hicho katika ulinzi wa nchi amewasisitizia makamanda na maafisa wa kituo hicho akiwaambia: Kujiweka tayari wakati wote na kuwa na machaguo yanayofaa kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya kila aina ni jambo la dharura sana kwenu.
Katika mkutano huo uliofanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa kuanzishwa kituo cha ulinzi wa anga cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amesifu juhudi za makamanda na wafanyakazi wa kituo hicho na kuongeza kuwa: Kuguswa mno na matukio mbali mbali na kufanya kazi zao kwa uchungu maafisa wa kituo hicho kunazidi kutilia nguvu uhakika kwamba kuna wajibu wa kuzijua vizuri nukta dhaifu na njia zote zinazoweza kutumiwa na adui na kuwa na mipangilio bora ya kila namna na mizuri kwa ajili ya kukabiliana na njama hizo kwa njia zote.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la viongozi kuwashirikisha vilivyo wananchi katika mambo yao yote kuwa ni jambo muhimu na kuongeza kuwa: Maafisa katika sekta tofauti wakiwemo wale wa vikosi vya ulinzi nchini wanapaswa kuitumia vizuri sana fursa hiyo ya kuaminiwa na wananchi na wana jukumu la kutekeleza vizuri majukumu yao ili kujibu kwa njia bora matarajio ya wananchi.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Ismaili, Kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya SAW cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kituo hicho kiko tayari wakati wote kulinda usalama wa nchi kwa nguvu zake zote na kutekeleza kikamilifu mikakati ya kiulinzi ya Amnirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi nchini.
Mwanzoni mwa mkutano huo, makamanda na maafisa wa kituo hicho cha ulinzi wa anga wamesali Sala za Adhuhuri na Alasiri zilizosalishwa na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ambaye ndiye Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
 
< Nyuma   Mbele >

^