Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Kyrgyzstan Chapa
05/09/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo Alasiri ameonana na Rais Almazbek Atambayev wa Kyrgyzstan na huku akitilia mkazo udharua wa kuimarishwa na kutiwa nguvu kadiri inavyowezekana uhusiano wa pande mbili wa nchi ndugu za Waislamu amesisitiza kuwa: Msingi wa siasa za mambo ya nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umesimama juu ya kupanua uhusiano na mfungamano wake madhubuti na wa pande zote kati yake na nchi nyingine zote ndugu za Kiislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kupinga ubeberu wa madola makubwa ya kiistikbari kuwa ni msingi wa mafundisho ya Mwenyezi Mungu na ya Kiislamu na huku akiashiria matamshi ya Rais wa Kyrgyzstan kuhusiana na kufungwa kituo cha anga cha Marekani nchini humo na udharura wa kusimama kidete kupambana na ubeberu wa madola makubwa amesema: Madola ya kiistikbari na vamizi, siku zote yanafanya njama dhidi ya mataifa mengine duniani, lakini dini tukufu ya Kiislamu inapigania heshima ya mataifa ya Waislamu na kwamba njia pekee ya kuweza kukabiliana vilivyo na kuzishinda shari za madola ya kibeberu ni kusimama kidete na kuimarisha uhusiano baina ya nchi za Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile amelitaja suala la kupanuliwa ushirikiano wa nchi mbili katika sekta tofauti zikiwemo za mawasiliano kuwa ni jambo linalowezekana na linategemea nia ya kweli kwa ajili ya kuleta mfungamano madhubuti na makini baina ya nchi za Kiislamu.

 

Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Almazbek Atambayev wa Kyrgyzstan ameelezea furaha yake kwa kupata fursa ya kutembelea Tehran na kuongeza kuwa: Iran na Kyrgyzstan ni mataifa mawili ndugu ambayo yana dini, historia na utamaduni wa pamoja na ndani ya mataifa yote hayo mawili kuna moyo wa kupigania uhuru, ukombozi na kujitegemea.
Rais wa Kyrgyzstan ametoa mwito wa kupanuliwa zaidi uhusiano wa nchi mbili katika masuala ya uchukuzi, kuanzishwa njia za mawasiliano za barabarani, reli na njia za angani na kuongeza kwamba: Kuna wajibu wa kuongezwa maradufu na kadiri inavyowezekana kiwango cha uhusiano na mabadilishano ya kibiashara baina ya nchi mbili.
Rais Almazbek Atambayev amegusia pia suala la kufungwa kambi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Minas huko Kyrgyzstan na kufutwa mkataba wa ushirikiano baina ya nchi hiyo na Marekani na kuongeza kuwa, hakuna nchi yoyote duniani iliyo na haki ya kujiona bora kuliko nchi nyingine na kufanya mambo yaliyo dhidi ya nchi nyinginezo ikiwa ni pamoja na kuziwekea nchi hizo vikwazo vya kidhulma.
Rais Atambayev ameongeza kuwa: Nchi ya Marekani ambayo iliasisiwa miaka karibu 200 tu iliyopita inataka kuitwisha mambo yake nchi kama Iran yenye historia ndefu na ustaarabu wa miaka elfu tano iliyopita. Amesema, jambo hilo haliwezekani kabisa.
Vile vile amelipongeza taifa na serikali ya Iran kwa kusimama kidete mbele ya Marekani na kusema: Iran imesimama imara bila ya kutetereka mbele ya vikwazo vya madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani, na kadiri siku zinavyopita ndivyo taifa hili linavyozidi kuimarika. Amesema: Sisi tunaihesabu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni ruwaza na kigezo bora kwetu.

 
< Nyuma   Mbele >

^