Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Mkuu na Wajumbe wa Baraza Kuu la Intaneti Chapa
07/09/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo (Jumatatu) ameonana na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu na wajumbe wa Baraza Kuu la Masuala ya Intaneti la Iran na kulitaja baraza hilo kuwa ndicho kituo kikuu cha kuweka sera kwa uangalifu mkubwa, kwa kuzingatia majukumu na kwa kujiamini kuhusiana na masuala ya Intaneti na huku akiashiri kuzidi kukua na kuzidi kupanuka kila leo na kwa kasi kubwa suala hili la kipekee la Intaneti amesisitiza kuwa: Inabidi; kwa kutumia uwezo wa kila namna na vipaji vingi vya kila nui vya vijana nchini Iran na kwa kutumia sera sahihi na hatua makini na zenye uratibu mzuri wa pamoja tena bila ya kupoteza muda; kupigwe hatua za haraka na za maana za kutoka katika hali ya kufanya mambo kwa pupa katika uga wa Intaneti na kuingia kwa nguvu zote kwenye medani hiyo kwa lengo la kutoa taathira kubwa nzuri na kuzalisha mazalisho ya Kiislamu yenye umakini na mvuto wa hali ya juu na kuyaingia kwenye medani hiyo.
Vile vile ameashiria namna Intaneti ilivyo na taathira kubwa ikiwa ni nguvu ya kipekee katika nyuga tofauti zikiwemo za utamaduni, siasa, uchumi, mtindo wa maisha, imani, itikadi za kidini pamoja na maadili na amesisitizia ulazima wa kuweko mipango madhubuti na makini ya kuweza kulinda mipaka ya usalama wa kifikra na kimaadili wa jamii katika uga huo na kuongeza kwamba: Kuna mambo ya lazima yanayopaswa kuzingatiwa kwa ajili ya kushiriki vilivyo na kwa taathira kubwa katika masuala ya Intaneti nayo ni, kuwa na marejeo makuu mamoja ya kuchukulia maamuzi, kulipa uzito mkubwa suala la utekelezaji wa maamuzi yanayochukuliwa tena bila ya kupoteza wakati, kuweko uratibu wa pamoja baina ya taasisi husika na kujiepusha na mambo ya pembeni pembeni na yasiyo na umuhimu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vile vile amelitaja suala la kuwa na mipangilio mizuri na uungaji mkono wa Serikali hususan kitengo cha elimu na teknolojia cha ofisi ya Rais kwa ajili ya kupanua sekta inayohusiana na teknolojia ya masawiliano, kuwa ni jambo la dharura sana.
Amesisitiza kuwa: Kupanulia wigo wa sekta hiyo kupitia mashirika ya elimu msingi kutakuwa na taathira kubwa nzuri katika kuandaa nafasi za kazi na kuleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amemshukuru mheshimiwa Rais na wajumbe waliopita wa Baraza Kuu la Masuala la Intaneti la Iran pamoja na makatibu wa hivi sasa na wa zamani wa baraza hilo.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Muhandisi Entezari, Katibu wa Baraza Kuu la Masuala ya Intaneti la Iran wametoa ripoti fupi kuhusu umuhimu wa Intaneti na udharura wa kuwa na ratiba na mipangilio mizuri kwa ajili ya kuingia kikamilifu katika uga huo. Vile vile wameelezea hatua zilizochukuliwa na baraza hilo na kituo cha taifa cha Intaneti katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wa majukumu yake.
Vile vile Ayatullah Amoli Larijani, Mkuu wa Chombo cha Mahakama nchini Iran amezungumzia nukta kadhaa muhimu kuhusu mambo ya lazima na yanayohitajika katika masuala mazima ya Intaneti nchini.
 
< Nyuma   Mbele >

^