Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Tanzia kufuatia kifo cha Ayatullah Khazali Chapa
16/09/2015
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe wa mkono wa pole kufuatia kufariki dunia alimu mwenye taqwa, Ayatullah Bwana Abul Qasim Khazali.
Ujumbe kamili ya ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatafvyo:

Kwa jina Lake Mtukuka

Ninatumia fursa hii kutoa mkono wa pole kwa familia na wafiwa wote na vile vile kwa wapenzi na marafiki kufuatia kufariki dunia alimu mwanaharakati na mchaji Mungu, marhum Ayatullah Bwana Alhaj Sheikh Abul Qasim Khazali, Mwenyezi Mungu amrehemu. Umri uliojaa baraka wa mwanachuoni huyo mwenye fadhila, umesheheni nukta nzuri zinazong'ara na kumeremeta. Alipitisha miaka mingi kwa kupiga goti la kuchimba elimu kutoka kwa Imam Khomeini na wanachuoni wengine wakubwa katika miji ya Qum na Mash'had. Alikuwa pamoja na Imam wetu mtukufu tangu katika siku za awali kabisa za mwamko wa Mapinduzi ya Kiislamu na alisimama imara kumtetea kiushujaa mtu huyo mkubwa katika vipindi vigumu vya ukandamizaji wa utawala wa taghuti (utawala wa Shah) na alikuwa akitangaza waziwazi na kwa ufasaha mkubwa msimamo wake huo. Aidha alichukua majukumu mazito baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na alikuwa pia mjumbe katika Baraza la kulinda Katiba na Baraza la Wanavyuoni Wataalamu (linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu). Alionesha subira ya hali ya juu baada ya kuuawa shahidi mwanawe huko Qum na katika zama za harakai ya Mapinduzi ya taifa la Iran. Alikuwa amehifadhi Qur'ani nzima na kuwa na ukuruba nayo mkubwa na alijipamba pia kwa bahari pana isiyo na mwisho ya Hadith kama ambavyo alikuwa na harakati za muda mrefu za kufanya tablighi na kufundisha dini tukufu ya Kiislamu na alisimama imara katika njia asili na sirati iliyonyooka ya Mapinduzi ya Kiislamu kwa kila hali, nyakati zote na mwahala mote hadi mwisho wa umri wake.

Hivyo ni miongoni mwa vipengee muhimu katika maisha ya alimu huyu mwenye taqwa na aliyekuwa mwingi wa harakati. Tunamuombea maghufira mbele ya Allah tukimuomba Mwenyezi Mungu amlipe kheri na awe radhi naye. Tunamuomba Allah Mwenye kurehemu, ammiminie rehema na maghufira Yake.

Sayyia Ali Khamenei
25 Shahrivar 1394 (Hijria Shamsia)
(16 Septemba 2015).
 
< Nyuma   Mbele >

^