Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana naMajeruhi wa Vita Waliovunjika Migongo na Waliojeruhiwa kwa Asilimia 70 Chapa
20/09/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi, (Jumapili) ikiwa ni katika kipindi hiki cha kukaribia Wiki ya Kujihami Kutakatifu, amewatembelea kwa muda wa masaa mawili na nusu, majeruhi kadhaa wa vita waliovunjika migongo na waliojeruhiwa asilimia 70 ya miili yao ambapo baadhi yao imma wamepoteza macho yote mawili au jicho moja au viungo viwili vya miili yao. Ameonana kwa karibu pia na familia za majeruhi hao wa vita na kuzungumza nao katika anga ya kushibana na ya mapenzi makubwa.
Baada ya kuonana na majeruhi hao wa vita na familia zao, Ayatullah Udhma Khamenei ametoa hotuba fupi na huku akigusia tabu na mashaka ya kimwili ya majeruhi hao wa vita amesema kuwa, malipo yao mbele ya Mwenyezi Mungu ni makubwa maradufu kutokana na mtihani mkubwa walio nao.
Ameongeza kuwa: Majeruhi wa vita nchini Iran ni taswira ya kipindi cha mtihani mkubwa uliolikumba taifa la Iran wakati wa vita vya kujihami kutakatifu (Vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa zamani wa Iraq dhidi ya utawala mchanga wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) na kwamba kuwepo majeruhi hao katika jamii kwa hakika kunaakisi na kubainisha uhakika wa kihistoria, kimaarifa, kisiasa na kimataifa.
Amesisitiza kuwa: Katika upande mmoja, majeruhi wa vita ni uthibitisho wa jinai za madola ya kibeberu ambayo yalimuunga mkono Saddam na katika upande wa pili majeruhiwa hao wa vita wanaonesha adhama na utukufu aliokuwa nao Imam Khomeini (quddisa sirruh) na utukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambayo kwa pamoja yameweza kulea watu wakubwa na watukufu kama hao na kuwapelekea kwenye medani ya mapambano.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja subira na uvumilivu wa hali ya juu unaooneshwa na wake wa majeruhi hao wa kivita katika kipindi kigumu mno cha kuwahudumia waume zao na kusema kuwa, jambo hilo kwa hakika ni kujitolea katika njia ya haki na ni jihadi na hamasa kubwa kwa maana halisi ya neno, na amewataka wake na watoto pamoja na jamaa wa majeruhi hao wa kivita waulinde na wautunze vizuri utajiri huo adhimu wa kimaanawi.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Shahidi Mahallati, mwakilishi wa fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) ambaye pia ni mkuu wa Taasisi ya Mashahidi na Watu Wanaojitolea katika Njia ya Haki ametoa ripoti fupi kuhusu kazi za taasisi hiyo katika kuwahudumia watu wanaojitolea katika njia ya haki na familia zao na kuongeza kuwa: Kuwaenzi watu wanaojitolea katika njia ya haki ni kuenzi watu waliounda hamasa kubwa ambao wamekuwa kigezo bora kwa jamii na wametoa funzo la namna ya kupambana vilivyo na mabeberu wa kimataifa.
Kwa upande wake, Meja Jenerali Muhammad Ali Jaafari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amegusia namna lilivyofanyika kongamano la pili la kitaifa la kuwaenzi majeruhi wa vita nchini na kusisitiza kuwa: Watu wanaojitolea katika njia ya haki ambao wamevaa medali ya fakhari shingoni mwao, hawajawahi hata mara moja kuona kuwa jukumu hatari la kuyalinda Mapinduzi ya Kiislamu na matunda na mafanikio yake limekwisha, bali hadi leo hii wanaendelea kujitokea kishujaa katika medani tofauti na kutekeleza majukumu yao kwa nia safi na kwa msimamo usiotetereka.
 
< Nyuma   Mbele >

^