Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mnasaba wa Wiki ya Kujihami Kutakatifu Chapa
24/09/2015
Ayatullah Udhma Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Alkhamisi) ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kuanza maadhimisho ya wiki ya kujihami kutakatifu na siku ya kuwaenzi mashahidi na watu wanaojitolea kwenye njia ya Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa: Shahidi na kuuawa shahidi katika utamaduni wa Kiislamu ni dhihirisho la uhai na ustawi na kwamba kupita kwa muda hakujaweza na hakutaweza kupunguza heshima, hadhi na kumbukumbu za mashahidi azizi.
Matini kamili ya ujumbe huo uliotolewa sambamba na kuanza zoezi la kupangusa mavumbi na kuyanyunyizia marashi maziara ya mashahidi kote nchini Iran na ambao umesomwa na Hujjatul Islam Walmuslimin Shahid Mahallati, mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) katika Taasisi za Mashahidi na Masuala ya Watu Wanaojitolea katika Njia ya Haki katika maziara ya Behesht Zahra, kusini mwa Tehran, ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Kupita kwa muda hakujaweza na hakutaweza - Inshaallah - kupunguza haiba, jina na kumbukumbu za mashahidi. Shahidi na kuuawa shahidi katika utamaduni wa Kiislamu ni dhihirisho la uhai, kuwepo daima, kunawiri na kuwa na harakati zinazong'ara; na kwa hakika ni sisi ambao ndio tunapaswa kujifungamanisha na kujiunganisha na maana hiyo kubwa na ya milele kwa faida yetu wenyewe, kwa jamii na kwa nchi yetu ili tuweze kujiletea heshima na kuwa na athari za kubakia milele. Kuteuliwa siku moja na kuitwa Wiki ya Kujihami Kutakatifu, ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu linalotakiwa katika uwanja huo.
Amani ya Allah iwe juu ya roho safi za mashahidi na familia zao vumilivu.
Sayyid Ali Khamenei
2 Mehr 1394 (Hijria Shamsia)
24 Septemba 2015.

 
< Nyuma   Mbele >

^