Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kufuatia maafa ya kusikitisha katika ardhi ya Mina Chapa
24/09/2015
http://english.khamenei.ir//images/stories/20120913_smpl.jpgKiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran ametoa ujumbe maalumu kufuatia kutokea maafa ya kusikitisha yaliyopelekea kufariki dunia mahujaji wengi wa Baytullahil Haram huko Mina nchini Saudi Arabia. Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Kwa hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwa hakika Kwake Yeye tutarejea.
Maafa mabaya ya kusikitisha yaliyotokea leo huko Mina na kupelekea kufariki dunia idadi kubwa ya wageni wa Mwingi wa rehema na waumini waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kutoka nchi mbali mbali duniani, ni msiba mkubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu na yameitumbukiza kwenye huzuni na majonzi sikuu ya Waislamu (ya Idul Adh'ha). Katika nchi yetu azizi (Iran), makumi ya familia ambazo zilikuwa zinawasubiri kwa hamu kubwa wapendwa wao warejee nyumbani kutoka kwenye ibada ya Hija, hivi sasa wametumbukia kwenye msiba na majonzi.
Nikiwa na majonzi na huzuni kubwa moyoni, ninatumia fursa hii kutoa mkono wa pole kwa watu wote waliokumbwa na tukio hilo la kusikitisha, kwanza kwa roho toharifu ya Bwana Mtume Muhammad SAW, pia kwa Imam wa Zama, Imam Mahdi AS ambaye yeye hasa ndiye mwenye msiba huu na kwa jamaa wote na wafiwa wote katika kona zote za ulimwengu wa Kiislamu na hususan ndani ya Iran azizi na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu na Mwingi wa shukrani awape ahueni ya haraka wageni Wake hao watukufu waliojeruhiwa na ninapenda hapa kukumbushia mambo kadhaa ambayo ni:
1 - Maafisa wa ofisi zangu pamoja na taasisi ya Hija nchini, wafanye juhudi maradufu na bila ya kuchoka kuwatambua na kuwatibu mahujaji waliojeruhiwa na kuwarejesha nchini na kutoa habari na taarifa za haraka kuhusu suala hilo na kama ambavyo leo kutwa nzima wamekuwa wakishughulikia jambo hilo, waendelee vivyo hivyo na kila mwenye uwezo awasaidie.
2 - Watekeleze majukumu na wajibu wao wa Kiislamu kwa ndugu zao Waislamu kwa kutoa msaada wowote utakaohitijiwa na mahujaji wa nchi nyenginezo.
3 - Ni wajibu kwa serikali ya Saudia kubeba jukumu zito la tukio hilo chungu na itekeleze majukumu yake kwa haki na kiuadilifu. Hatupaswi kusahau kuwa usimamiaji mbovu na hatua zisizo sahihi zilizochukuliwa na wasimamiaji wa amali hiyo huko Saudi Arabia ndiyo sababu iliyopelekea kutokea maafa hayo.
4 - Mahujaji waliopoteza maisha yao kwenye tukio hilo Inshaallah waingie kwenye maneno haya yaliyojaa nuru ya Qur'ani Tukufu kwenye aya inayosema:

وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ
 
Na anayetoka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. (Suratun Nisaa - 4:100).
Hiyo kwa kweli ni faraja kubwa kwa wafiwa. Mahujaji hao wamekwenda mbele ya Haki baada ya kutufu, kwenda Safa na Marwa na baada ya kupitisha masaa yaliyojaa baraka ya Arafa na Mash'ar na walikuwa katika utekelezaji wa amali za Hija. Inshaallah Mwenyezi Mungu atawamiminia rehema na neema Zake maalumu. Ninaitumia fursa hii kutoa mkono wa pole kwa mara nyengine tena na ninatangaza siku tatu za maombolezo ya umma nchini (Iran).
Na amani iwe juu ya waja wa Mwenyezi Mungu walio wema.
Sayyid Ali Khamenei
2 Mehr 1394 (Hijria Shamsia)
(10 Mfunguo Tatu Dhulhijja 1436)
(24 Septemba 2015).
 
< Nyuma   Mbele >

^