Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Matamshi ya Kiongozi Muadhamu katika Darsa ya "Khariji" ya Fikihi kuhusu Maafa ya Mina Chapa
27/09/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumapili) na kabla ya kuanza kutoa darsa yake ya "Khariji" ya fikihi (darsa ya daraja la juu kabisa la fikihi) ametoa hotuba fupi na huku akiashiria maafa makubwa ya Mina huko Saudi Arabia amesisitiza kwamba: Ulimwengu wa Kiislamu unajiuliza maswali mengi kuhusu maafa hayo na kwamba viongozi wa Saudi Arabia badala ya kukwepa, wanapaswa kuuomba radhi umma wa Kiislamu na familia zilizopata majonzi kutokana na maafa hayo, na wabebe dhima ya tukio hilo zito na jukumu la kila kinachohusiana na maafa hayo.
Ayatullah Udhma Khamenei amekumbushia tukio chungu la Mina na kugeuka sikukuu ya Eidul Adh'ha kuwa majonzi na huzuni kwa umma wa Kiislamu badala ya furaha na kusisitiza kuwa: Mtu hawezi kuacha kufikiria maafa hayo hata kwa sekunde moja na kwamba huzuni hizo zitaendelea kwa muda kuwa jambo zito linaloziumiza nyoyo zetu na za Waislamu wote.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekitaja kitendo cha viongozi wa Saudi Arabia cha kujaribu kukwepa majukumu yao kuhusiana na maafa hayo kwamba si jambo sahihi na ni kitendo tasa kisicho na taathira yoyote. Amesema: Ulimwengu wa Kiislamu unajiuliza maswali mengi hivi sasa na hatua ya kupoteza maisha zaidi ya watu elfu moja kwenye tukio hilo si suala dogo hata chembe, hivyo ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kukaa na kulitafakari vyema jambo hilo.
Vile vile amesisitiza kuwa: Suala hili halitosahauliwa kamwe, na kwamba mataifa ya Waislamu yataendelea kulipa uzito mkubwa suala la kulifuatilia jambo hilo, na Wasaudia nao - badala ya kujaribu kukwepa na kuwabebesha wengine lawama za maafa hayo - wanapaswa kukubali kubeba dhima ya tukio hilo na kuuomba radhi umma wa Kiislamu na familia zilizojaa majonzi kwenye maafa hayo.
 
< Nyuma   Mbele >

^