Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Makamanda wa Jeshi Mjini Nowshahr Chapa
01/10/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Alkhamisi), ameonana na makamanda wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na sambamba na kusisitiza kwamba, sababu hasa ya kuweko uadui wa kila namna dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni kusimama kidete taifa la Iran na kutokubali kuburuzwa na kupigishwa magoti na madola ya kibeberu na kuongeza kuwa: Vikosi vya ulinzi nchini Iran vinapaswa kuongeza kasi yake katika maendeleo na kujiimarisha na kujiweka tayari wakati wote na viwe na nguvu kiasi kwamba maadui hata wasithubutu kufikiria tu katika akili zao kutaka kuivamia Iran.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kuweka mipango ya kuifanya Iran ya Kiislamu kuwa na mustakbali bora na kupiga hatua kubwa zaidi za kimaendeleo katika nyuga zote kuwa ni jambo la dharura na ameongeza kwamba: Mustakbali wa Iran umo mikononi mwa vijana, na vijana wanapaswa kujua thamani ya jambo hilo na kuna wajibu wa kukifanya kizazi kijacho cha Iran kuwa imara zaidi, kuwa na nguvu zaidi, kuwa kizazi kilichoelimika zaidi na kilicho shujaa zaidi kwa ajili ya kujenga mustakbali wenye nguvu kubwa zaidi na wenye umadhubuti mkubwa zaidi wa kuifaya Iran iwe na kauli thabiti na ya wazi zaidi katika eneo hili na duniani kwa ujumla.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria namna Iran ilivyokuwa imebaki nyuma kiajabu na kihistoria kutokana na watawala na vibaraka wa madola ya kibeberu hususan katika kipindi cha wafalme wa Kipahlavi na kuongeza kuwa: Maendeleo makubwa viliyopiga leo hii vikosi vya kijeshi vya Iran katika nyuga na nyanja tofauti yana thamani kubwa, lakini kutokana na jinsi Iran ilivyokuwa imebakishwa nyuma na tawala za kitaghuti huko nyuma, kuna wajibu wa kuongeza kasi katika harakati hiyo ili Iran iweze kuwa na nguvu kwa namna ambayo maadui hawatathubutu hata kufikiria tu ndani ya akili zao kufanya uchokozi kwenye mipaka ya nchi hii.
Vile vile ameutaja muqawama na kusimama kidete taifa la Iran katika kipindi cha miaka minane ya kujihami kutakatifu (wakati wa vita ilivyolazimishwa Iran kupigana baada ya kuvamiwa na utawala wa wakati huo wa Iraq) kuwa ni uzoefu muhimu unaoonekana wazi mbele ya walimwengu wote na kusisitiza kuwa: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni mfumo ulio huru na tangu mwanzoni mwa Mapinduzi ya Kiislamu umekuwa ukitangaza na kufuatilia kwa uwazi kabisa siasa zake na haina woga wala hofu yoyote mbele ya makeke ya dola lolote lile linalopinga siasa zake hizo.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia uadui mkubwa na mzito wa maadui dhidi ya harakati huru na ya maajabu ya taifa la Iran na kusema kuwa: Adui anataka kuuona mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unasalimu amri na kupiga magoti mbele ya adui huyo na kwamba kumlegezea kamba kwa aina yoyote adui hakutamaliza uadui wake wa kila namna dhidi ya taifa hili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kuchomoza taifa huru lililosimama imara kukabiliana na ubeberu wa madola ya kiistikbari, si jambo linaloweza kuvumiliwa hata kidogo na mfumo wa kibeberu duniani, hivyo lazima mfumo huo wa kiistikbari utalifanyia uadui taifa hilo na kwamba si sahihi hata chembe kudhani na kuwa na mawazo kwamba kama mtu fulani ametoa matamshi fulani basi na sisi tusifanye lolote na tusimwangalie kwa jicho la adui, na tukifanya hivyo kutapunguza uadui wa maadui hao dhidi yetu.
Aidha ameashiria namna mataifa mengine duniani pamoja na baadhi ya tawala zisizo vibaraka wa mabeberu zinavyounga mkono harakati huru ya Iran na kuongeza kuwa: Mataifa ya dunia yanavutiwa mno yanapoona maendeleo na namna taifa la Iran lilivyosimama imara kujihami na kulinda manufaa yake mbele ya madola ya kibeberu na kwamba katika safari za nje ya nchi za viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu pia kwenye nchi na mahala popote ambapo tawala za nchi husika zinawaruhusu wananchi kuonesha mapenzi yao kwa Iran na uungaji mkono wao kwa misimamo yake isiyotetereka, basi utaona wimbi kubwa la watu linajitokeza kuunga mkono misimamo hiyo.
Katika sehemu nyengine ya hotuba yake, Ayatullah Udhma Khamenei amezungumzia umuhimu wa kufanya utafiti na kuleta maendeleo katika sekta hiyo ndani ya vikosi vya ulinzi vya Iran na kuongeza kuwa: Vyuo Vikuu na vituo vya utafiti nchini Iran vina uwezo na nafasi kubwa ya kuweza kuleta maendeleo hayo, hivyo kuna wajibu wa kutiwa nguvu mahusiano ya kielimu baina ya Vyuo Vikuu na vituo hivyo vya utafiti kwa upande mmoja na vikosi vya ulinzi kwa upande mwengine.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia pia umuhimu wa kuingia kwenye nyuga mpya zisizojulikana za kijeshi na kufanya ubunifu mpya na amma kuhusiana na mafunzo na mazoezi ya kijeshi amesema: Maandalizi ya ratiba za mazoezi ya kijeshi yanapaswa yazingatie kuwa mazoezi hayo ya kijeshi yanakaribia mno hali ya vita vya kweli katika medani ya vita, na inabidi zitabiriwe nguvu na suhula zote za kijeshi za adui na kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana nazo.
Mwanzoni mwa mkutano huo, Admeri Habibullah Sayyari, Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ametoa ripoti fupi kuhusiana na kazi na operesheni za Jeshi la Majini la Iran katika nyuga za kujiimarisha kivifaa na kizana, kwa ataarifa, operesheni na kujistawisha kielimu na kimaarifa, kwa teknolojia ya mawasiliano pamoja na kudhamini usalama wa njia za mawasiliano na ustawi wa masuala ya baharini ya Iran.
 
< Nyuma   Mbele >

^