Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Afanya Khitma ya Mahujaji Waliokufa kwenye Maafa ya Mina Chapa
04/10/2015
 Khitma na "majlis" ya kuwaenzi na kuwaombea dua mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina nchini Saudi Arabia imefanywa leo (Jumapili) na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Husainia ya Imam Khomeini (quddisa sirruhu), mjini Tehran.
Mbali na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, majlis hiyo imehudhuriwa pia na baadhi ya watu wa familia za mahujaji waliopoteza maisha yao katika maafa ya Mina, wakuu wa Mihimili Mitatu Mikuu ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama), maulamaa na wanavyuoni wa kidini pamoja na shakhsia na wakuu wa nchi na wa vikosi vya ulinzi na matabaka mbali mbali ya wananchi. Maqarii wa Qur'ani Tukufu wamesoma Qur'ani Tukufu na baada ya hapo wasoma kasida za Ahlul Bayt Alayhimus Salaam wamesoma kasida mbali mbali za kuomboleza vifo vya mahujaji hao madhlumu katika maafa ya Mina na kukumbushia pia msiba wa Imam Husain AS.
Katika majlis hiyo, Hujjatul Islam Walmuslimin Siddiqi, ametoa hotuba fupi na kubainisha kwamba maafa ya Mina yamezijeruhi na kuzitia majonzi makubwa nyoyo za Waislamu na kuongeza kuwa, ukoo wa Aal Saud ndio unaopaswa kulaumiwa na kubeba dhima ya kumwagika damu za wageni hao watukufu wa Mwenyezi Mungu.
Vile vile majlis kama hizo za kuwaenzi, kuwasomea Faatiha na dua mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina, zimefanyika kwa wakati mmoja katika Haram ya Bibi Maasuma Salamullahi Alayha mjini Qum na katika makao makuu ya mikoa yote ya Iran kwa niaba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei.
 
< Nyuma   Mbele >

^