Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Wajumbe wa Kamati ya Kongamano la Mashahidi wa Chaharmahal va Bakhtiari Chapa
07/10/2015
 Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na wajumbe wa kamati ya kongamano la mashahidi wa mkoa wa Chaharmahal va Bakhtiari tarehe 5 Oktoba 2015, imesambazwa leo kwenye Msikiti Mkuu wa Imam Khomeini (quddisa sirruh) katika mji Shahrekord, makao makuu ya mkoa huo.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei aliashiria kwenye mkutano huo, juu ya njama na mashambulizi ya kila upande ya kiutamaduni na ya kiitikadi na ya kisiasa ya adui ambaye anatumia silaha na zana zote katika mashambulizi yake hayo dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Kuzidhoofisha itikadi za kidini na kisiasa na kufanya njama za kuwashawishi na kuwavuta vijana amilifu na wenye taathira kwenye jamii na kuwaingia kwenye mkondo huo ni miongoni mwa mipango ya uadui wa kisiasa na kiutamaduni wa adui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, juhudi zinazofanyika hivi sasa pamoja na harakati mbali mbali za vijana waumini na vijana "mahizbullah" na viongozi wenye itikadi thabiti katika kukabiliana na mashambulizi ya adui ni mambo muhimu na ya lazima na kuongeza kuwa: Kufanya kazi za kueneza na kutia nguvu mafundisho muhimu ya Uislamu kama vile jihadi, itikadi ya kufa shahidi na kuwa tayari kulinda itikadi hiyo kwa kuwa tayari kufa shahidi na kusubiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa kazi muhimu ambazo zinaweza kuzishinda njama zote za adui.
Amesema jambo la lazima la kuwezesha kufanyika kazi kubwa na ya kina katika kueneza mafundisho hayo muhimu na ya kimsingi, ni kuzikinaisha nyoyo za walengwa na kutumia mbinu za kisanii na kitablighi katika kufanikisha jukumu hilo muhimu na kuongeza kuwa: Watu wa kutoa fikra na nadharia pamoja na watu wa sanaa wanapaswa kushirikiana katika kuzalisha vitu vyenye taathira kubwa na nzuri na kwamba jambo hilo ni jukumu pia la viongozi wa serikali na wasio wa serikali kama ambavyo ni jukumu pia la watu wote waumini na wenye imani thabiti ya dini.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia kuweko msukumo, ikhlasi na kujitokeza kwa wingi wananchi wa mkoa wa Chaharmahal va Bakhtiari katika nyuga na medani mbali mbali za Mapinduzi ya Kiislamu na za kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu na amewashukuru sana wananchi wa mkoa huo kwa uungwana wao.
 
< Nyuma   Mbele >

^