Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi MuadhamuAonana na Makamanda, Wafanyakazi wa Kikosi cha Wanamaji cha Sepah na Familia Zaoa Chapa
07/10/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na makamanda na wafanyakazi wa kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah na majimui ya familia zao na vile vile familia za mashahidi wa kikosi hicho na huku akiashiria nafasi ya vijana wanamapinduzi katika kikosi cha wanamaji cha Sepah na vijana mashujaa wa Kusini mwa Iran katika kudhamini na kulinda usalama wa baharini na kumtia woga na hofu adui amesisitiza kuwa: Wanachopigania maadui ni kubadilisha mahesabu ya viongozi nchini na kubadilisha fikra za wananchi wa Iran na hususan vijana, hivyo watu wote wanapaswa kuwa macho na makini mno katika kukabiliana na njama za maadui.
Katika mkutano huo Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amegusia umuhimu wa suala la usalama wa baharini na kusema kuwa, uimara na kuwa tayari wakati wote vikosi vya ulinzi nchini Iran kunapaswa kuwa kwa namna ambayo kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu, kuweze kutia woga na hofu kubwa ndani ya nyonyo za maadui ili maadui hao wasithubutu kabisa kufikiria kuivamia Iran kwani kama ngome itakuwa na nafasi ya kuweza kupenya, basi adui lazima atapenya.
Ameongeza kuwa, hivi sasa kutokana na baraka za kuundwa kambi ya kimapinduzi ya kusini mwa Iran ambayo inaundwa na vikosi vya wanamaji vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah na vijana mashujaa wa kusini mwa Iran, kumeweza kutekelezwa kivitendo mafundisho na amri ya Qur'ani Tukufu ya kuzusha hofu na woga mkubwa katika nyoyo za maadui.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amesisitiza kwa mara nyengine tena kuwa, kamwe Iran si nchi inayoweza kuanzisha vita dhidi ya wengine na wakati huo huo lakini ameongeza kuwa: Amma ni jambo lililo wazi kwamba daima adui ana mawazo ya kufanya uchokozi na kujipenyeza kwenye nchi nyingine, hivyo Iran inapaswa wakati wote kuongeza uwezo na nguvu zake za kielimu na kisilaha kupitia ubunifu wa kila namna na wa kila leo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kujiimarisha na kujistawisha zaidi na zaidi kikosi cha wanamaji cha Sepah na kikosi cha majini cha Jeshi la Iran kuwa ni jambo la dharura mno na kusisitizia ulazima wa kuzibakisha hai kumbukumbu na utajo wa vijana wanamapinduzi na wenye imani thabiti ya kidini kama vile Shahid Nader Mahdavi na wenzake ambao walikabiliana kwa ushujaa mkubwa na manuwari ya Wamarekani na kuwapa Wamarekani somo ambalo hawawezi kamwe kulisahau. Ameongeza kuwa: Maadui wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamekumbwa na ushujaa kama huu na kusimama kidete namna hii kwa wanamapambano shujaa wa Iran na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si mfumo ambao mtu anaweza kuufanyia lolote analopenda.
Vile vile Ayatullah Udhma Khamenei amezishukuru familia hususan familia za makamanda na wafanyakazi wa kikosi hicho cha wanamaji kwa kushirikiana vizuri na vilivyo na wapendwa wao kwenye maeneo ya kusini mwa Iran.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran ameendelea na hotuba yake kwa kugusia njama hatari za madola ya kibeberu na kiistikabari dhidi ya eneo la Mashariki ya Kati na huku akisisitiza kuwa, madola hayo hayasiti hata chembe kutumia silaha hatari mno na mbinu zisizo za kibinadamu kabisa katika kuua watu wasio na hatia ameongeza kuwa: Madai ya mabeberu ya kwamba eti yanapigania na kulinda haki za binadamu na haki za raia yanakinzana kikamilifu ya ukweli wa mambo na kwa hakika ni chapwa na ni madai ya kipuuzi kikamilifu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja shambulio la Marekani katika hospitali moja huko Afghanistan na kuuliwa wananchi wa Syria, Iraq, Yemen, Palestina na Bahrain kuwa ni mifano ya waazi ya maafa yanayofanywa na madola ya kiistikbari yasiyo na chembe ya huruma kwa kushirikiana na vitimbakwiri wao na kuongeza kuwa, hatari kubwa zaidi inayoukabili ulimwengu hivi sasa ni unafiki, riya, kujionesha na uongo wa wale wanaodai kutetea haki za binadamu duniani.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia nafasi muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazingira ya hivi sasa liliyomo ndani yake eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa: Katika mazingira kama haya, Jamhuri ya Kiislamu kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, mbali na kufanikiwa kuzuia ushawishi na kujipenyeza adui ndani ya nchi, imefanikiwa pia kuvunja na kufelisha njama na mipango ya adui katika eneo hilo kwenye masuala mengi sana.
Aidha amesisitiza kuwa, kufeli na kushindwa njama za adui ndani ya Iran na kwenye eneo la Mashariki ya Kati kumetokana na baraka za kuwa macho, kuwa tayari wakati wote na kuwa na nia ya kweli vijana wanamapinduzi pamoja na nguvu za Jamhuri ya Kiislamu katika eneo hili na kusisitiza kuwa: Ni kwa sababu hiyo ndio maana njama kubwa zaidi na mipango mingi ya madola ya kiistikbari ya kuufanyia uadui mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na madai ya Marekani na kutaka kufanya mazungumzo na Iran yakapaswa kutiwa kwenye fungu hilo hilo na kuhesabiwa kwenye fremu hiyo hiyo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewalaumu wale watu ambao wanafanya uzembe na ambao ni wavivu wa kufikiri ndani ya Iran ambao wanashindwa kuuona ukubwa na uzito wa hatari za njama hizo za Marekani na kuongeza kuwa: Mbali na kuwepo watu hao walio wavivu wa kufikiri, kuna watu wengine katika jamii ambao hawajali kabisa maslahi na manufaa ya nchi na ya taifa lao.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia maswali kadhaa yanayoulizwa na watu wasioona mbali, wasiojali maslahi ya nchi na ya taifa lao na walio wavivu wa kufikiri kuhusiana na kufanya mazungumzo na Marekani na kusema kuwa: Watu hao wanatoa hoja kuwa, mbona Imam Ali Alayhis Salaam na Imam Husain Alayhis Salaam walifanya mazungumzo na maadui wao, itakuwaje sisi leo hii tunapinga kufanya mazungumzo na Marekani?
Amewajibu watu wenye mawazo kama hayo akisema: Mtu anayetoa hoja na uchambuzi wa namna hiyo kuhusu masuala ya historia ya Uislamu na kuyafananisha na masuala yalivyo hivi sasa nchini, ni mtu mwenye mawazo finyu kupindukia kwani Imam Ali Alayhis Salaam hakufanya mazungumzo na Zubair na wala Imam Husain Alayhis Salaam hakufanya mazungumzo na Umar Saad kwa namna ya mazungumzo yalivyo leo hii ya kujiuza na kujikabidhi kwenye mikono ya adui, bali watukufu hao wawili walifumbia macho kila kitu na kuamua kuzungumza na watu wawili hao kwa ajili ya kuwanasihi na kuwakumbusha wajibu wa kuogopa hasira za Mwenyezi Mungu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Ni jambo la kusikitisha kuona kuwa kuna baadhi ya watu wanaojaribu kulazimisha kufanyika mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na shetani mkubwa Marekani na kujaribu kuhalalisha jambo hilo kwa kutoa hoja za kimaamuma zisizoangalia mbali na kusema kuwa, watu hao wanasema mambo hayo kupitia magazeti, kwenye hotuba zao na kwenye mitandao ya Intaneti, jambo ambalo kwa kweli ni makosa kikamilifu.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza pia kuwa, Iran kamwe haijawahi na haitowahi kupinga asili ya kufanya mazungumzo na nchi nyingine, ni sawa tu mazungumzo hayo yatafanyika baina yake na nchi za Ulaya au zisizo za Ulaya lakini wakati huo huo amesisitiza kuwa: Amma kuhusiana na Marekani, suala hapo ni tofauti kabisa, kwani msimamo wa Wamarekani na mtazamo wao kuhusiana na mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran una maana ya kuwapa fursa ya kujipenyeza na kufungua njia kwa ajili ya kulibebesha taifa la Iran ubeberu wao.
Aidha ameashiria namna Marekani inavyoshirikiana na mrengo wa Kizayuni kufanya mambo yanayokwenda kinyume kabisa na ubinadamu na kusisitiza kuwa: Kufanya mazungumzo na Marekani kuna maana ya kufungua njia ya kujipenyeza Wamarekani kwenye masuala ya kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kiusalama ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia mazungumzo ya hivi karibuni ya nyuklia na kusema: Katika mazungumzo hayo, upande wa pili wa mazungumzo ulifanya njama ya kutumia kila fursa iliyojitokeza ili kujipenyeza nchini na kufanya mambo yaliyo kinyume na maslahi ya nchi na ya taifa la Iran, lakini timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran ilikuwa macho, ingawa katika baadhi ya sehemu Wamarekani walipata baadhi ya fursa hiyo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema: Ni marufuku kufanya mazungumzo na Marekani kwani mazungumzo hayo kwanza hayana faida yoyote, bali pili, yana madhara makubwa mno.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kipindi cha hivi sasa ni kipindi muhimu mno hasa kwa kuzingatia mazingira yaliyopo hivi sasa na kwa kutilia maanani njama zinazoendela kufanywa na maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ambao tab'an Iran ina taarifa kamili kuhusiana na njama zao.
Amesema, wanachotaka maadui ni kubadilisha mahesabu ya viongozi wa Iran na kubadilisha fikra za wananchi wa Iran hususan masuala yanayohusiana na Mapinduzi ya Kiislamu, masuala ya kidini na mambo yanayohusiana na maslahi ya nchi na ya taifa.
Amesisitiza kuwa, katika suala la kubadilisha fikra za wananchi wa Iran, shabaha kuu ya maadui ni kubadilisha fikra za vijana wa taifa hili, hivyo vijana nchini Iran wanapaswa kuzidi kuwa macho kwa kadiri inavyowezekana.
Ameongeza kuwa: Tab'an kwa taufiki na uwezo wa Mwenyezi Mungu, vijana wetu katika Vyuo Vikuu na vile vile katika vikosi vya ulinzi wako macho na wanachapa kazi vizuri, nami sina wasiwasi wowote katika upande huo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia kumbukumbu na maadhimisho ya siku ya Mubahala na namna Mtume Muhammad Swallallahu Alayhi Waalihi Wasallam na Aal zake watoharifu walivyosimama kidete kukabiliana na mrengo wa ukafiri na amewakhutubu vijana wanamapinduzi nchini Iran akiwaambia kwa kusisitiza kuwa: Kama ilivyojiri katika kadhia ya Mubahala mwanzoni mwa Uislamu, imani yote ilisimama kukabiliana na ukafiri, leo hii pia ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imani yote imesimama kukabiliana na ukafiri na kama ambavyo katika zama hizo za mwanzoni mwa Uislamu, kwa unyofu wa kimaanawi wa Bwana Mtume Swallallahu Alayhi Waalihi Wasallam na Aal zake watukufu hao walifanikiwa kumshinda na kumlazimisha adui kukimbia medani ya mapambano, leo hii pia taifa la Iran kwa kutumia nguvu na uwezo wake wa kimaanawi, litafanikiwa kumfurusha adui na kumtoa nje ya medani ya mapambano.
Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Kama tutakuwa tayari kuinusu dini ya Mwenyezi Mungu na kuipigania inavyotakiwa, bila ya shaka yoyote ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwanusuru na kuwasaidia wanaoinusuru na kuipigania vilivyo dini Yake, itatimia; na wote wanaoutakia mabaya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran watafeli na kushindwa tu katika njama na mipango yao ya kiusalama, kijeshi, kiuchumi na kiutamaduni.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Admirali Fadavi, Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah ametoa hotuba fupi na sambamba na kuashiria ushujaa wa jeshi la Sepah katika kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu (vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa wakati huo wa Iraq dhidi ya utawala mchanga wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran) na kumwambia Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran kwamba: Wanajeshi wako wako tayari wakati wote na wanasubiri tu amri yao ili waweze kutoa funzo kubwa na la kihistoria kwa shetani mkubwa na kwa vibaraka wake wote wanaokera na kufanya usumbufu na ambao wanaua raia na watoto wadogo katika eneo hili la Mashariki ya Kati bila ya sababu na bila ya kuwa na hatia yoyote.
Kamanda Fadavi amesisitiza pia kuwa, kikosi cha majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Sepah kiko imara mno hivi sasa na kuongeza kuwa: Hatua ya kikosi cha wanamaji cha Sepah ya kuonyesha sehemu ndogo tu ya uwezo wake wa kijeshi na uimara wake, imewalazimisha maadui waanze kuzungumzia suala la kubadilisha mikakati na stratijia zao baharini wakati ambapo mambo ambayo wanayajua maadui kuhusu uwezo wa kijeshi wa Iran ni machache mno na hayawezi kukisiwa kamwe na yale wasiyoyajua kuhusu nguvu na uwezo huo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
 
< Nyuma   Mbele >

^