Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu Kufuatia Kuuawa Shahidi Kamanda Husain Hamedani Chapa
10/10/2015
Supreme Leader's Message on the Martyrdom of Sardar Hussein HamedaniAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kufuatia kuuawa shahidi kamanda aliyejaa fakhari, shahid Husain Hamedani kwa ajili ya kutoa mkono wa pongezi na mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi mwanamapambano huyo shujaa. Matini ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Ninapenda kutumia fursa hii kutoa mkono wa baraka na mkono wa pole kwa familia, wafiwa, marafiki na wanamapambano pamoja na majimui yote iliyojaa fakhari ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kufuatia kuuawa shahidi kamanda wa kujivunia, shahid Husain Hamedani. Mwanamapambano huyo mkongwe, mcheshi na mwenye bidii kubwa, alipitisha ujana wake wote uliojaa usafi na ibada, katika medani za heshima na utukufu, katika kulindia nchi yake ya Kiislamu na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu; na sehemu ya mwisho wa maisha yake yaliyojaa baraka na sura yake iliyojaa nuru, ameipitisha katika kulinda Haram ya Ahlul Bayt Alayhimus Salaam na katika kupambana na uafiriti wa kitakfiri ulio dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu na amefanikiwa kutimiza ndoto zake kubwa na za muda mrefu, za kupoteza maisha kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, na akiwa katika kupigana jihadi katika njia ya Allah, na hivyo kufanikiwa kupata rehema na baraka nyingi za Mwenyezi Mungu.
Safu imara iliyonyooka ya watu wenye hamu ya kupata heshima hiyo, na wale walioko mstari wa mbele katika njia ya jihadi na kuwa tayari kufa shahidi katika njia ya Allah, ni safu ndefu sana na ni jengo madhubuti mno ndani ya Iran ya Kiislamu na katika jeshi la Sepah na kwenye vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu: Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwishakufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo. (al Ahzab:23)
Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya shahid Hamedani na ziwe juu ya watu wote wanaopigana jihadi katika njia ya Allah.

Sayyid Ali Khamenei,
18 Mehr 1394
(10 Oktoba 2015).

 
< Nyuma   Mbele >

^