Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiisdlamu Aonana na Mkuu na Wakurugenzi wa IRIB Chapa
12/10/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na mkuu na wakurugenzi wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB pamoja na wajumbe wa baraza la kusimamia na kutathmini kazi za shirika hilo na kubainisha malengo ya vita laini vilivyopangiliwa vyema, vikubwa na vya pande zote vya mfumo wa kibeberu duniani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, kubadilisha imani na itikadi za wananchi ni miongoni mwa malengo makuu vya vita hivyo tata. Amesisitiza kwamba, Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB lina nafasi ya kipekee katika kupambana na mashambulizi hayo makali na kulitaja suala la kuwa na mipangilio mizuri ya kiutalaamu kwa ajili ya kufanikisha majukumu ya kihabari na kitaifa kuwa ni jambo la dharura kwa shirika hilo.
Mwanzoni mwa hotuba yake, Ayatullah Udhma Khamenei amezungumzia suala la umuhimu wa shirika hilo la utangazaji la taifa katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na huku akiashiria harakati adhimu ya upashaji habari na msaada wa vyombo vipya vya habari vilivyochomoza hivi karibu amesema kuwa: Shirika la utangazaji la taifa IRIB bila ya kutaka limelazimika kutumbukia katika medani ya mapambano ya ajabu na makubwa, nayo ndiyo hiyo medani tata na nzito mno ya vita laini.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mwito kwa wanafikra, wasomi, watu wenye uchungu na taifa lao na wenye hamu ya kufanya mambo, wasomne na kutalii kwa kina vitu vipya na kufanyia utafiti wa kina na kutoa tathmini nzuri juu ya vipenge mbali mbali vya vita laini na kuongeza kuwa: Katika vita laini kunafuatiliwa malengo yale yale ya vita vya wazi na vya dhahiri vya kutumia silaha, na tofauti yake ni kuwa katika vita laini, malengo yake yanafuatiliwa kwa ukubwa na kwa kina na kwa upana zaidi.
Vile vile amegusia baadhi ya utata mkubwa na hatari nyingi zaidi za vita laini ikilinganishwa na vita vya kutumia zana za kivita na kuongeza kuwa: Vita laini - tofauti na vita vya kutumia silaha na zana za wazi za kivita - madhara yake hayaonekani na kueleweka na hata katika baadhi ya masuala, upande wa pili unaendelea na mashambulizi yake, lakini jamii inayolengwa na mashambulizi hayo utaiona imelala usingizi fofofo na haihisi wala haishughulishwi na mashambulizi hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Vita vya moja kwa moja vya kutumia silaha kwa kawaida huzusha hasira za wananchi na kuleta umoja na mshikamano pamoja na kuungana vilivyo watu wa taifa linaloshambuliwa wakati ambapo katika vita laini, msukumo wa kupambana na vita hivyo hupotea na badala yake huandaliwa uwanja wa kuzuka hitilafu na mizozo ndani ya taifa linaloshambuliwa.
Baada ya kubainisha hatari kubwa mno na zenye kutia wasiwasi mkubwa za vita laini, ikilinganishwa na vita vya wazi vya moja kwa moja vya kutumia silaha, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa: Vita laini haviihusu Iran peke yake lakini kuhusiana na Iran, lengo kuu la vita hivyo vilivyopangiliwa vizuri mno ni kuiyeyusha Jamhuri ya Kiislamu yza Iran na kuisambaratisha ndani kwa ndani kupitia kuharibu sira na batini yake na kuiacha ibakie jina tu bila ya kuwa na taathira yoyote.
Amesisitiza kuwa, kuvuruga batini na sira kuna maana ya kuvuruga msukumo, kaulimbiu, nara, vitu vikuu na vya kimsingi vya Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na malengo yake makuu. Ameongeza kuwa: Ndani ya mipaka ya malengo ya vita laini vya adui, kuendelea kuwepo jina la Jamhuri ya Kiislamu na hata kuwepo mtu mwenye kuvaa kilemba katika nafasi ya juu kabisa ya utawala nchini, si muhimu kwa adui, lililo muhimu kwake ni kuifanya Iran idhamini malengo ya Marekani, ya Uzayuni na ya kanali ya madola ya kibeberu duniani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, viongozi na wananchi ndio walengwa wakuu wa vita hivyo laini na kusisitiza kuwa: Amma kuhusiana na mipango iliyomo ndani ya vita laini kuhusu viongozi nchini Iran ni kwamba nimeshazungumza na viongozi na nitaendelea kuzungumza nao juu ya jambo hilo, lakini walengwa wakuu wa vita laini ni wananchi hususan watu wenye vipaji, watu wa Vyuo Vikuu, wanachuo, vijana na wanaharakati walio mstari wa mbele katika jamii ya Iran.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Wanacholenga maadui ni kuwaathiri wananchi wa Iran na kubadilisha sehemu kubwa na pana ya itikadi zao hususan vijana na watu wenye vipaji na ushawishi katika jamii ya Iran. Amesema: Miongoni mwa itikadi zinazolengwa na maadui hao ni itikadi za kidini, kisiasa na kiutamaduni za wananchi wa Iran.
Ameongeza kuwa: Wananchi wetu wana itikadi zao maalumu kuhusu dini, familia, suala la wanawake na wanaume, uhuru, kupambana na mabeberu, demokrsia ya Kiislamu na masuala mengine mbali mbali ya kiutamaduni na kwamba upande wa pili hivi sasa unafanya njama za kubadilisha na kuvuruga itikadi hizo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kubadilisha itikadi na kuzifanya zilizopitwa na wakati na kurejesha itikadi za zamani kwamba ni lengo na shabaha nyengine ya vita laini na kusisitiza kuwa: Wananchi wetu wana itikadi zao maalumu kuhusiana na utawala fasidi na wa kidikteta uliopita nchini, lakini kinachofanyika kwenye vita laini, ni kujaribu kuyafanya mambo maovu, machafu na chapwa ya huko nyuma nchini Iran yaonekane mazuri na yenye kukubalika nchini.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Wanachofanya maadui ni kujaribu kufuta itikadi za hivi sasa na kurejesha itikadi za zamani na kuwafanya wananchi wa Iran waamini kuwa hakukuwa na haja wala ulazima wa kutokea Mapinduzi ya Kiislamu yaliyokuja kuangamiza maovu ya huko nyuma.
Amesema, kuzibadilisha itikadi za wananchi wa Iran kwa kuzingatia mustakbali na hali ya hivi sasa ni shabaha nyengine ya vita laini na kuongeza kuwa: Maadui wanafanya njama za kuwaonesha vijana wa leo nchini Iran kuwa, hali iliyo nayo nchi yao hivi sasa inatia aibu na haiwezekani kabisa kupata maendeleo katika siku za usoni kupitia mfumo uliopo wa utawala, ili kwa njia hiyo wawakatishe tamaa vijana na kuwapokonya nguvu za kufanya harakati, kujielimisha na kufanya kazi kwa bidii.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezitaja njama za kujaribu kuleta itikadi zisizo za kweli ndani ya vijana wa Iran kuhusu masuala ya dunia na hususan Marekani na Ulaya na kujaribu kuonesha kuwa huko ndiko kwenye maisha bora na kwamba nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo zinaishi kwa raha, kwa amani na bila ya matatizo yoyote, kuwa ni lengo jengine la vita laini. Hapo hapo ametoa muhtasari wa hotuba yake kuhusu maudhui hiyo akisema: Lengo kuu na la juu kabisa la vita laini ni kuiyeyusha na kuisambaratisha ndani kwa ndani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia kuharibu itikadi za watu na kudhoofisha imani zao hususan vijana.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia uwezo wa vifaa na zana za kuendeshea vita laini alizo nazo adui na kuongeza kuwa: Maendeleo yote yanayostawi kila leo katika mitandao ya Intaneti yanalenga kwenye kufanikisha malengo na shabaha za vita laini, lakini lililo muhimu zaidi ni kuwa, suhula na maendeleo hayo ni sawa na jeshi kubwa linalofanya mashambulizi dhidi ya watu muhimu na wenye vipawa vya kifikra, kisiasa, kisarufi, kijamii na wanaharakati wakubwa katika vyombo vya mawasiliano, na kada mbali mbali za sanaa vitu ambavyo vina athari na nguvu kubwa sana za kuweza kufanikisha malengo ya vita laini.
Vile vile ameitaja mipango kabambe na kufanya kazi kwa bidii na bila ya kutosha; kwa uratibu na mpangilio mmoja kuwa ni katika sifa maalumu za wapangaji na waendeshaji wa vita laini na kuongeza kuwa: Katika kazi zote za uzalishaji vitu mbali mbali yakiwemo mazalisho ya sauti, taswira na maandishi ya upande unaolikabili taifa la Iran, yote yana malengo ya kufanikisha vita baridi, tab'an mambo hayo yanafuatiliwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja, lakini kwa sura ya kudumu, ya mtawalia na ya kubebesha mambo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kueneza tabia ya kutekeleza mafundisho ya dini kwa kiwango cha chini sana na kuipa umuhimu na kipaumbele dini ya kisekula ambayo inatanguliza mbele vitendo vya watu binafsi na vya kijamii kabla ya mafundisho ya dini, kuwa ni miongoni mwa malengo ya siri ya mipango mikuu ya kijamii yanayopiganiwa kufanikishwa na vyombo vya habari vya madola ya kibeberu na kuongeza kuwa: Maadui wana mipango kabambe na madhubuti ya kufuatilia malengo yao hayo tata mno, lakini sisi tuko nyuma katika uwanja huo.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amezitaja bidii za chombo cha umma cha utangazaji IRIB kuwa ni nzuri sana na wakati huo huo ameongeza kuwa: Inabidi bidii na jitihada hizo ziendelee na zifanyike kwa njia bora kabisa kwa ajili ya kufanikisha malengo yaliyokusudiwa, bila ya ria wala majivuno na kujiona bora na kwa kuzingatia uwezo wa vipindi na ratiba zote za shirika hilo la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili viweze kuwavutia walengwa na kuwafanya wavikubali.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kazi muhimu zaidi ya kufanya kwa ajili ya kufanikisha kwa uwazi malengo ya chombo hicho cha utangazaji za taifa katika kukabilana na kupambana na vita laini vya maadui, ni kuwa na utafiti na tathmini ya kina, ya kimsingi, sahihi na ya kuyaangalia katika uhalisia wake mazingira yaliyopo hivi sasa nchini na hali ya kieneo na ya kimataifa kwa maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Tathmini na utafiti huo utaziunganisha akili na misimamo ya viongozi na wakuu wa daraja mbali mbali ndani ya shirika hilo na ndio msingi wa harakati zote za shirika hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei amekutaja kujiweka mbali na suala la kuongeza chumbi na kuchupa mipaka katika kutumia uwezo uliopo, kuzingatia matatizo yaliyopo, kutokubali kuathiriwa na propaganda potofu za madola ya kigeni, kujiepusha na suala la kuangalia mambo kwa mtazamo finyu na kuzingatia uwezo wa hivi sasa na wa dhati uliopo wa kuwezesha kufanyika utafiti na tathmini ya kimsingi ndani ya Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mambo ya lazima na ya dharura na yenye taathira kubwa na kuongeza kuwa: Kulinganisha kwa njia sahihi hali ya hivi sasa ya Iran na kuipima na hali yaliyokuwa nayo mapinduzi makubwa duniani katika kipindi cha miaka kama hiyo ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kunaweza kutoa picha sahihi na inayozingatia uhalisia wa mambo kuhusiana na hali ya Iran sasa hivi.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia kuwepo matatizo mengi, vita vya ndani vya umwagaji damu na hata kurejea baadhi ya mapinduzi ya zama hizi kwenye tawala zilizopinduliwa na mapinduzi hayo na kuongeza kwamba: Inabidi hali iliyo nayo Iran hivi sasa ipimwe na hali iliyokuwa nayo Marekani miaka karibu arubaini iliyopita baada ya kutolewa azimio muhimu la uhuru wa nchi hiyo, na ikisiwe na hali iliyokuwa nayo Ufaransa baada ya miongo minne ya Mapinduzi Makubwa ya Ufaransa, kwani ni kwa njia hiyo ndipo utaweza kupatikana ukweli wa mambo na ndipo utakapodhihirika uhakika wa maendeleo makubwa iliyopata Iran katika kipindi cha miongo takriban minne ya tangu yalipopata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu nchini.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kubainisha udharura wa kupatikana tathmini ya kimsingi na ya pande zote ndani ya Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB kwa kusema: Inabidi uzingatiwe pia upotoshaji wa vyombo vya habari vya madola ya kibeberu ambavyo vinapindua kikamilifu ukweli kuhusu Iran mbele ya walimwengu na hata kati ya Wairani wenyewe kwa ajili ya kufanikisha shabaha na malengo ya vita vyao laini. Amesema, taswira inayooneshwa na vyombo hivyo duniani kuhusiana na Iran ni potofu kikamilifu.
Ayatullah Udhma Khamenei amewapendekezea wakuu na wakurugenzi wa shirika hilo la utangazaji la taifa kwamba wawe na tathmini ya kina na ya kuzingatia uhalisia wa mambo kuhusiana na hali ya Jamhuri ya Kiislamu ikilinganishwa na hali ya baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati ambazo zimekuwa zikiishi chini ya kivuli cha Marekani katika kipindi cha miongo minne iliyopita.
Vile vile amesema: Ulinganishaji huo utathibitisha kuwa, kusalimu amri na kukubali kuburuzwa kuna madhara kiasi gani na kusimama kidete kukabiliana na ubeberu wa Marekani kuna kheri na manufaa kiwango gani na kunaweza kuiletea nchi maendeleo ya kiasi gani.
Baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu udharura wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa na tathmini ya kimsingi na ya kina ukiwa ndio msingi wa vipindi na ratiba zote za shirika hilo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kazi ya pili ya chombo hicho cha utangazaji cha taifa akisema, ni jambo la dharura kwa chombo hicho kutekeleza kwa namna na kwa njia bora zaidi majukumu yake kupitia kuainisha na kubuni fikra za kimsingi na za kiusuli za kufanikisha majukumu hayo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria stratijia na mikakati aliyoiwasilisha kwa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB tangu alipochukua uongozi Bw. Sarafraz na kusisitiza kuwa: Inabidi mikakati hiyo yote ipewe umuhimu mkubwa na kuwekwe ratiba na mipangilio mizuri ya kuitekeleza kiutaalamu ambapo tab'an kumefanyika kazi nzuri katika baadhi ya mambo kuhusu mikakati hiyo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema kwa kusisitiza kuwa, ni jambo la lazima na la dharura kuwa na ratiba na mipangilio mizuri ya kufanikisha mikakati iliyowasilishwa kwa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB kwa ajili ya ufanikishaji wa stratijia na mikakati yote ya Jamhuri ya Kiislamu.
Amesema, chombo hicho cha utangazaji cha taifa ni chombo cha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, ni chombo cha nchi na ni chombo cha Mapinduzi ya Kiislamu. Amesisitiza kuwa: Shirika la IRIB ni kambi iliyoko mstari wa mbele, na ni kambi amilifu katika kupambana na vita laini na kwamba viongozi na wafanyakazi wa chombo hicho cha utangazaji cha taifa, ni makamanda na ni wanajeshi kwenye vita hivyo.
Vile vile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa shukrani zake kutokana na jitihada na bidii kubwa zinazofanywa na wafanyakazi wa shirika hilo la utangazaji la taifa hususan Bw. Sarafraz, mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB na kusema kuwa, Bw. Sarafraz ni mtu mchapa kazi, mwenye bidii kubwa, mwenye hima, anayefanya kazi zake kwa utaratibu na mpangilio mzuri, asiyependa makuu na aliyejiweka mbali na masuala ya anasa, msafi na mwenye uchungu na ‘baytul maal,' shujaa, mwenye uthubutu wa kuchukua maamuzi mazito, mbunifu, mwenye mawazo mapana na anayekwenda na wakati.
Ameongeza kuwa: Sifa hizo zenye thamani kubwa zinastahiki kupongezwa na inabidi kuhakikisha zinaendelea kuwepo na ni jambo la dharura kwa shirika kama la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB ambalo ni shirika lenye nafasi na umuhimu mkubwa sana ikilinganishwa na taasisi nyenginezo nchini.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Bw. Sarafraz, Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB ametoa ripoti fupi kuhusu mipango na hatua mbali mbali zilizochukuliwa na shirika hilo.
Mkuu wa Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB amegusia changamoto na matatizo mbali mbali linayokumbana nayo shirika hilo la utangazaji la taifa na kusema: Kufanyia marekebisho muundo wa kiidara na vile vile kufanyia marekebisho ajenda na sheria za shirika hilo, kuandaa utangulizi wa kuanzishwa mfumo unaokubalika wa upashaji habari, kuweka mipango kwa ajili ya kutia nguvu nafasi ya IRIB katika mitandao ya Intaneti na mitandao ya kijamii ya simu za mkononi na kuongeza ubora wa vipindi vya chombo hicho cha utangazaji ni miongoni mwa harakati na mikakati muhimu zaidi ya Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ameongeza kuwa: Kufuatilia masuala muhimu na ya kimsing kama vile kueneza fikra za Mapinduzi ya Kiislamu, uchumi wa kimuqawama na wa kusimama kidete, mtindo wa maisha ya Kiirani Kiislamu na ustawi wa kielimu, kuasisiwa kituo maalumu cha kupanua uandikaji wa miswada ya filamu, kupangiliwa upya na kuanzishwa kanali ya televisheni ya watoto, kuanzishwa kundi la ‘elimu jamali' na ‘elimu maarifa' kutumiwa nguvu kazi kijana na za waumini katika uongozi wa vitengo mbali mbali vya shirika hilo, kuongeza idadi ya walengwa na vipindi vya shirika hilo la utangazaji la taifa na kuongeza taathira na ushawishi wa kanali za televisheni za al Alam na Press TV, kuanzisha Shirika la Habari la IRIB, kufanywa ya kisasa na ya kiutaalamu zaidi Kanali ya Habari, kusisitizia mno suala la kufayiwa uchambuzi na kutolewa ufafanuzi matukio mbali mbali, kuanzishwa kanali za televisheni za lugha za Azari, Kikurdi na Kiurdu ndani ya Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo cha Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, kuzalishwa upya vyanzo mbali mbali vilivyohifadhiwa katika kitengo cha kuhifadhi vitu tofauti, kuupa umuhimu mkubwa muziki wa kidini na wa kimapinduzi, kuzingatia umuhimu wa kuvutia imani ya wananchi na kuwafanya wahisi kwamba wanaishi katika usalama, ni mipango na hatua nyingine za shirika hilo la utangazaji la taifa.
 
< Nyuma   Mbele >

^