Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Atembelea Nyumbani kwa Kamanda Shahid Hamedani Chapa
19/10/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo usiku (Jumapili) amekwenda nyumbani kwa kamanda shahid Hussein Hamedani na sambamba na kuonana na familia ya mwanamapambano huyo, ametoa mkono wa baraka na mkono wa pole kwa familia hiyo kufuatia kuuawa shahidi mwanamapambano huyo shujaa (wakati alipokuwa analinda Haram ya Bibi Zaynab SA nchini Syria na kutoa ushauri wa kijeshi kwa taifa hilo).
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia ikhlasi, jihadi na jitihada kubwa alizofanya kamanda shahid Hamedani katika medani mbali mbali za hatari na kusema kuwa, kuuawa shahidi na kupata mwisho mwema kama huo unaosubiriwa kwa hamasa kubwa, ni matumaini ya muda mrefu na ya ndani kabisa ya nyoyo za watu wote wanaopigana jihadi katika njia ya haki. Amesema, Mwenyezi Mungu amewafungulia mlango wa kufa shahidi waja Wake wenye ikhlasi na ni jambo la kusikitisha iwapo watu wanaopigana jihadi katika njia ya haki kama vile shahid Hamedani, wataondoka duniani kwa namna isiyokuwa ya kufa shahidi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kujitokeza kwa wingi mno watu katika maziko ya shahid Hamedani mjini Tehran na kushiriki kwa wingi ambao ni mara chache umewahi kushuhudiwa, wananchi wa Hamedan kwenye maziko hayo ni dhihirisho la malipo mema ya Mwenyezi LMungu kwa shahid huyo mtukufu kutokana na ikhlasi aliyo kuwa nayo. Ameongeza kuwa: Kujitokeza watu kwa wingi huo wa kustaajabisha kwenye maziko hayo kunatokana na mvuto na ikhlasi ya shahidi huyo na kwa hakika alikuwa ni neema na fursa ya Mwenyezi Mungu kwa wananchi wa Hamedan ili kwa mara nyengine tena waweze kuitumia fursa hiyo kuonesha hisia zao za kimapinduzi na kuwa kwao tayari kufa shahidi katika njia ya haki.
Vile vile amempongeza mke na watu wengine wa familia ya shahid Hamedani kutokana na subira yao ya kupigiwa mfano na huku akiashiria namna familia za mashahidi zilivyo na fungu katika malipo mema ya Mwenyezi Mungu amesisitiza kuwa: Kuendelea silisila ya watu wanaokufa shahidi katika njia ya Allah na kuzidi kustawi na kunawiri neema hiyo adhimu ya Mwenyezi Mungu katika jamii, kunatokana na subira hiyo ya kupigiwa mfano ya familia za mashahidi. Amesema: Namuomba Mwenyezi Mungu amfufue shahidi huyu azizi pamoja na Mtume Mtukufu Swallallahu Alayhi Waalih na pamoja na mawalii Wake na aijaalie familia yake kuwa miongoni mwa wanaomiminiwa rehema na baraka Zake nyingi.
 
< Nyuma   Mbele >

^