Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Waendeshaji wa Ibada ya Hija Chapa
19/10/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, adhuhuri ya leo (Jumatatu) ameonana na maafisa wa kusimamia ibada ya Hija wa nchini Iran na kuyataja maafa machungu mno na ya kusikitisha sana ya Mina kuwa ni miongoni mwa mitihani ya Mwenyezi Mungu na huku akizilaumu tawala za nchi mbali mbali na hususan tawala za nchi za Magharibi na mashirika yanayodai kutetea haki za binadamu kwa kunyamazia kimya msiba huo mkubwa amesisitiza kuwa: Tukio hilo halipaswi kusahauliwa hata mara moja na kwamba chombo cha diplomasia na Taasisi ya Hija ya Iran zina wajibu wa kulifuatilia kwa uzito wa hali ya juu sana suala hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria pia dhima na jukumu linalopaswa kubebwa na utawala unaopokea mahujaji kuhusiana na mahujaji elfu saba waliopoteza maisha yao kwenye maafa ya Mina na kuongeza kuwa: Ilitegemewa kuwa ulimwengu wa Kiislamu ungelisimama kwa sauti moja kutangaza hasira na malalamiko yao baada ya kutokea maafa hayo, lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuwa, ukitoa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hakuna sauti nyengine yoyote ya kulalamikia maafa hayo iliyotolewa kiasi kwamba hata tawala za nchi ambazo raia wake wamepoteza maisha kwenye maafa hayo, hazikuonesha malalamiko makubwa kuhusu suala hilo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kufanyika mazungumzo na tawala za nchi mbali mbali kuhusiana na uzito wa maafa hayo na kutafutwa njia za kuzuia kujitokeza tena jambo hilo kuwa ni jukumu muhimu kwa viongozi wa Iran hususan chombo cha diplomasia nchini na kuongeza kuwa: Dhahiri ya tukio hilo inaonesha kuwa, maafa hayo yametokana na uzembe wa utawala unaopokea mahujaji lakini vyovyote iwavyo, kadhia hiyo si suala la kisiasa bali mjadala hapa ni kwamba maelfu ya Waislamu wamepoteza maisha yao wakati wa kutekeleza ibada na amali za Hija wakiwa katika vazi la Ihram, hivyo suala la kuifuatilia kadhia hiyo inabidi lipewe uzito wa hali ya juu sana.
Vile vile amesema kuwa, upande mwengine unaopaswa kufuatiliwa vizuri ni kimya cha wazi kabisa na kuchupa mipaka cha mashirika na taasisi zinazodai kutetea haki za binadamu za barani Ulaya na Marekani na kuongeza kuwa: Mashirika kidhabu na ya kinafiki yanayodai kutetea haki za binadamu na vile vile tawala za nchi za barani Ulaya ambazo baadhi ya wakati utaziona zinazusha makelele mengi mno duniani kwa kuuawa mtu mmoja, zimenyamazia kimya kabisa uzembe uliopelekea kupoteza maisha maelfu ya watu huko Mina.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Watu hao wanaojinadi kuwa ni watetezi wa haki za binadamu, kama ni wakweli katika madai yao hayo, basi wanapaswa wawatake waliosababisha maafa ya Mina wabebe dhima ya maafa hayo, wawatake wafidie hasara zake na watoe dhamana kuwa maafa kama hayo hayatatokea tena.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kuendelea kulifuatilia na kulibakisha hai suala hilo muhimu kuwa ni jukumu la Taasisi ya Hija na Ziara ya nchini na kusisitiza kuwa: Suala hili halipaswi kunyamaziwa kimya na wala kuliacha lisahauliwe na inabidi liendelee kuzungumziwa kwa miaka mingi ijayo na mawimbi ya harakati hiyo yaelekewe kwa tawala za nchi za Magharibi na kwa taasisi na mashirika yanayodai kutetea haki za binadamu duniani.
Vile vile amewashukuru kwa udhati wa moyo wake maafisa na wasiamiaji wote wa ibada ya Hija nchini Iran na hasa Hujjatul Islam Qadhi Asgar kutokana na ufuatiliaji wake wa karibu na kwa moyo na misimamo yake isiyotetereka na pia kutokana na harakati za kila upande na kuwa tayari kujibu maswali wakati wote na kutekeleza vizuri jukumu lake Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran, Bw. Saeed Ouhadi na ameongeza kuwa: Ujira na malipo mema ya Mwenyezi Mungu yako kwa ajili ya wahusika wote wa masuala ya Hija kutokana na jitihada zao kubwa na subira yao ya kupigiwa mfano na kwamba jitihada hizo kubwa katika njia ya Mwenyezi Mungu ndizo ambazo Bibi Zainab Salamullahi Alayha aliziita kuwa ujamali na uzuri baada ya kukumbwa na masaibu yote yale yaliyotokea kwenye jangwa la Karbala.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Qadhi Asgar, mwakilishi wa Fakihi Mtawala (Waliyyul Faqih) na msimamiaji wa mahujaji wa Iran ametoa ripoti fupi kuhusu kazi zilizofanyika katika Hija ya mwaka huu na vile vile ametoa ufafanuzi kuhusu hatua zilizochukuliwa kuhusiana na tukio la kuporomoka winchi ndani ya Masjidul Haram na maafa machungu ya Mina na kuongeza kuwa: Maafa ya Mina yametokea kutokana na usimamiaji mbovu na ukosefu wa tadibiri wa viongozi wa Saudi Arabia na kwamba suala hilo litaendelea kufuatiliwa kwa karibu na vyombo husika, na kutawekwa kumbukumbu nzuri kuhusiana na matukio na maafa hayo.
Kwa upande wake, Bw. saeed Ouhadi, Mkuu wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran amesema kuhusiana na kurejeshwa nchini Iran mahujaji waliofariki dunia kidhulma katika maafa ya Mina na kuwahudumia watu waliojeruhiwa kwenye maafa hayo kwamba, ufuatiliaji wa kina wa kujua hali ya mahujaji waliobakia wa Kiirani waliopotoeza maisha huko Mina zinaendelezwa kwa nguvu kubwa na vyombo vyote husika.
Mkuu wa huyo wa Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran ametoa ripoti pia kuhusu kazi zilizofanyika kwenye ibada ya Hija mwaka huu.
 
< Nyuma   Mbele >

^