Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Turkmenistan Chapa
22/11/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo jioni (Jumapili) ameonana na Rais Gurbanguly Berdimuhamedow wa Turkmenistan na huku akiashiria uhusiano wa karibu na wa kidugu uliopo baina ya Iran na Turkmenistan na nafasi kubwa na pana ya kupanua ushirikiano wa pande mbili na kukabiliana na machafuko mengi yaliyopo katika eneo hili amesisitiza kuwa: Njia ya kupambana na ugaidi na kumaliza kabisa chokochoko za makundi hayo, ni kuwafungulia njia wananchi; ya kufanya harakati sahihi za Kiislamu na kuzitia nguvu fikra za kweli za Uislamu ambazo ni za misimamo ya kimantiki na ya wastani (iliyo mbali na uchupaji mipaka).
Katika mazungumzo hayo, Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa mataifa mawili ya Iran na Turkmenistan ni majirani walio sawa na jamaa na ndugu wa karibu na huku akisisisitizia udharura wa kutumiwa nafasi nyingi zilizopo kwa ajili ya kustawisha ushirikiano wa pande mbili ameongeza kuwa: Kuna wajibu wa kuchuliwa hatua za kweli na za kivitendo na kupewa uzito mkubwa suala la utekelezaji wa makubaliano yanayofikiwa ili kwa njia hiyo iwezekane kushatawishwa vilivyo ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, usalama, ustawi na maendeleo ya majirani wa Iran na nchi za Kiislamu kiujumla ni kwa manufaa ya Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Mipaka ya Iran na Turkmenistan ni mipaka salama na yenye amani na utulivu suala ambalo linazipa utulivu pande zote mbili na hiyo ni fursa nzuri sana kwa Turkmenistan ya kuweza kutumia njia ya Iran kwa ajili ya kuyafikia maji ya Ghuba ya Uajemi (na ulimwengu mpana wa nje).
Amegusia usalama ulipo katika nchi za Iran na Turkmenistan licha ya kuweko machafuko mengi kwenye eneo hili na kusema kuwa, ni jambo la dharura kuzidi kushirikiana pande mbili ili kuhakikisha hali hiyo inandelea kuwepo.
Ameongeza kuwa: Njia ya kuweza kukabiliana na unyama na ugadi wa kikatili wa Daesh na magenge ya kitakfiri kama hilo yanayotumia vibaya Uislamu kutenda jinai hizo, ni kuwafungulia njia wananchi ya kufanya harakati sahihi za Kiislamu na njia bora kabisa ya kufanikisha suala hilo na kuvunja chokochoko za magenge hayo ya kigaidi ni kutiliwa nguvu fikra ya Kiislamu ya misimamo ya wastani na ya kimantiki.
Ayatullah Udhma Khamenei amezitaja jinai za kutisha za magenge ya kigaidi za kuwakata watu vichwa na kuwachoma watu wakiwa hai kwamba ni ithbati kamili kuwa magenge hayo hayana uhusiano wowote na Uislamu.
Amesisitiza kuwa: Uislamu ni dini ya udugu, ni dini ya kupendana, ni dini ya kuwapendelea watu wengine mema na mazuri na kwamba jinai zinazofanywa na magenge hayo hazina uhusiano hata chembe na Uislamu.
Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa pia na Bw. Jahangiri, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; Rais Gurbanguly Berdimuhamedow wa Turkmenistan ameelezea kufurahishwa kwake na kupata fursa ya kutembelea tena Tehran na amesema, ni fakhari kwake kupata fursa ya kuonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa: Siku zote hizi Iran na Turkmenistan zimekuwa na uhusiano mzuri wa kihistoria na zimekuwa pamoja kwa shinda na raha na kwamba matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kwamba Iran na Turkmenistan si majirani tu bali ni jamaa wa karibu, yamezidi kuipa moyo na kuifurahisha serikali na wananchi wa Turkmenistan.
Rais wa Turkmenistan amekumbushia pia nasaha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika safari zake za huko nyuma nchini Iran na kumueleza Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei kuwa: Matamshi yako ukiwa kiongozi mwenye muono mpana na mwanafikra unayeangalia mbali yana thamani kubwa kwetu na nasaha zako zimetuletea matunda mazuri baada ya kuzifanyia kazi.
Vile vile ameashiria nafasi kubwa na nyingi zilizopo kwa ajili ya kupanua uhusiano wa pande mbili hususan katika sekta za gesi, usafiri na usafirishaji pamoja na ujenzi wa barabara na kusema: Utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ya kiuchumi ya nchi mbili za Iran na Turkmenistan una manufaa kwa eneo hili zima.
Vile vile Rais wa Turkmenistan amekumbushia historia kongwe pamoja na umuhimu mkubwa wa "Njia ya Hariri" na kuongeza kuwa: Baadhi ya nchi zinapenda kuunganishwa na njia huru za baharini (za Ghuba ya Uajemi) kupitia Iran na Turkmenistan.
Vile vile amesema kuwa, hali ya kisiasa katika eneo hili si nzuri na huku akiashiria jinai za genge la kigaidi la Daesh amesema: Daesh na magenge mengine kama hilo hayajui chochote kuhusu Uislamu na hayana uhusiano wowote na dini hiyo ya Mwenyezi Mungu lakini inasikitisha kuona kuwa kuna baadhi ya madola yanayasaidia na kuyaunga mkono kwa kila hali magenge hayo.
 
< Nyuma   Mbele >

^