Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Venezuela Chapa
23/11/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na Rais Nicolás Maduro wa Venezuela na huku akiipongeza nchi hiyo kutokana na muqawama na harakati yake yenye kutoa ilhamu nzuri kwa wengine katika kukabiliana na siasa za kiistikbari na kusisitiza kuwa: Leo hii siasa za kiistikbari ni balaa kubwa kwa wanadamu na njia pekee ya kuweza nchi huru duniani kupata ushindi na maendeleo, ni kusimama kidete na kutegemea nguvu za wananchi wao katika vita vya irada na utashi.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia namna Marekani inavyoliangalia kwa tamaa kubwa eneo la Amerika ya Latini na kuongeza kuwa: Marekani inalihesabu eneo hilo kuwa ni sehemu yake ya kujifaragua, lakini harakati isiyo na mbadala na isiyo na mfano ya Venezuela imefanikiwa kuligeuza eneo hilo kuwa nukta huru yenye utambulisho wake.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, lengo la Marekani la kuiwekea mashinikizo Venezuela ni kujaribu kuangamiza muqawama wenye kutoa ilhamu kwa mataifa mengine wa serikali na taifa la Venezuela na kuongeza kuwa: Vita vinavyoendelea hivi sasa duniani kwa kweli ni vita vya irada na utashi, na bila ya shaka yoyote mtaweza kuyashinda matatizo yenu yote kwa kusimama imara kwenye irada na utashi wenu na kwa kutumia vizuri uwezo mkubwa wa nchi yenu.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia namna Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran yalivyo kigezo kizuri kutokana na kufanikiwa kwake kuupindua utawala kibaraka wa Kipahlavi uliokuwa umejizatiti kwa silaha za kisasa na kuongeza kuwa: Imam Khomeini (Rahmatullahi Alayhi) aliingia kwenye medani ya mapambano akiwa mikono mitupu na kufanikiwa kuuangusha utawala uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani na Ulaya kwa kutegemea matabaka yote ya wananchi na hivyo akafungua njia ya ushindi na kuendelea tawala huru duniani kupata mafanikio kwa kutumia kigezo hicho hicho.
Amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kupata maendeleo makubwa na ya kustaajabisha ya kielimu na kiteknolojia licha ya kuweko wimbi kubwa la mashinikizo na vikwazo vya maaduni na huo ni uzoefu muhimu sana. Ameongeza kuwa, uzoefu huo umepatikana kwa kutegemea nguvu za wananchi na kwamba ufunguo wa kutatulia matatizo yanayojitokeza ni kuzivutia nyoyo za wananchi kupitia kuwatumikia wananchi hao na kuwafanyia kazi zao kiukweli na kwa uaminifu.
Vile vile Ayatullah Udhma Khamenei amesisitizia haja ya kustawishwa ushirikiano wa pande mbili za Iran na Venezuela katika nyuga zote na kusisitiza kuwa: Iran na Venezuela ni marafiki wa kweli wenye uhusiano mzuri usioyumba.
Kwa upande wake, Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amegusia heshima na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo hayati Hugo Chaves, rais wa zamani wa nchi hiyo kwa Iran na kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Mimi pia nimejifunza mambo mengi kutokana na kuonana na wewe na matamshi na nasaha zako zimekuwa na taathira kubwa kwangu.
Rais wa Venezuela amesisitizia udharura wa kusimama imara katika kulinda uhuru wa taifa na kuongeza kuwa: Madola ya kibeberu yanazusha machafuko na vurugu duniani na kudunisha utambulisho wa nchi nyingine kwa shabaha ya kuangamiza uhuru wa mataifa hayo.
Rais Maduro ameashiria pia namna serikali na wananchi wa Venezuela walivyojiandaa vilivyo kwa ajili ya kukabiliana na njama za Marekani na kusema: Kama ulivyosisitiza, inabidi tupambana vilivyo katika vita vya irada na utashi kwa kutegemea nguvu za wananchi ili tuweze kuwashinda maadui.
Rais wa Venezuela amesisitizia pia umuhimu wa kikao cha nchi zinazosafirisha gesi kwa wingi duniani na wajibu wa kuangaliwa upya jumuiya ya OPEC na kuongeza kuwa: Tuna wajibu wa kuwa na mipango mipya kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ushirikiano wa pande mbili na utekelezaji wa miradi ya pamoja ili kwa njia hiyo tuweze kunyanua na kulinda heshima na hadhi zetu kama huko nyuma.
 
< Nyuma   Mbele >

^