Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Nigeria Chapa
23/11/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na kulitaja suala la kuongeza ushirikiano baina ya nchi za Kiislamu katika kulinda utambulisho wa Uislamu na Waislamu kuwa ni udharura wa kimsingi na kusisitiza kuwa: Muungano wa kimataifa unaodai kupambana na magenge ya kigaidi hauaminiki hata kidogo kwani nyuma ya pazia la kuanzishwa na kuungwa mkono magaidi hao kama vile Daesh wako hao hao wanaounda muungano wa kupambana na magenge ya kigaidi hususan Marekani.
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, "maadui wa wazi wa Uislamu" na "maadui wanaoupiga vita Uislamu kwa jina la Uislamu" ni pande mbili za makali ya mkasi na kuongeza kuwa: Nchi za Kiislamu zinapaswa kuongeza ushirikiano wao katika kupambana na maadui hao hatari mno na kwa ajili ya kulinda utambulisho na manufaa yao.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, si sahihi kuwa na matumaini na misaada ya Marekani na nchi za Magharibi katika kupambana na magenge ya kigaidi kama vile Daesh na Boko Haram na kuongeza kuwa: Kwa mujibu wa taarifa sahihi na za kina, Wamarekani na baadhi ya nchi butu zenye fikra finyu za eneo hili, zinalisaidia moja kwa moja kundi la Daesh huko nchini Iraq na kuchangia katika uharibifu unaofanywa na kundi hilo.
Amelitaja suala la kuimarishwa uhusiano baina ya nchi za Kiislamu kuwa hakuna maana ya kukataa na kufunga njia za uhusiano wa nchi nyingine na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ina uhusiano mzuri na nchi zote ukitoa Marekani na utawala wa Kizayuni, lakini tunaamini kuwa nchi za Kiislamu zinapaswa kuwa na uhusiano mpana zaidi na kuwa karibu zaidi baina yao.
Vile vile Ayatullah Udhma Khamenei ameelezea kufurahishwa kwake na kuchaguliwa Muhammad Buhari - akiwa Muislamu mwenye imani thabiti na aliyeshikamana vizuri na dini yake - kuwa rais wa nchi muhimu sana ya Nigeria na kusema kwamba, kuna nafasi kubwa na nyingi za kushirikiana nchi mbili za Iran na Nigeria. Amesisitiza pia kuwa: Inabidi kufanyike juhudi za makusudi za kugundua uwezo huo na kutumiwa vizuri.
Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na Bw. Jahangiri, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameutaja uhusiano wa nchi mbili za Iran na Nigeria kuwa ni mkongwe na ni madhubuti na kuongeza kuwa: Iran ni nchi kubwa iliyopiga hatua nzuri za kimaendeleo na ina uwezo mwingi na nafasi pana ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano na nchi nyingine.
Rais wa Nigeria ameishukuru Iran kwa kumwalika kushiriki katika kikao cha nchi zinazosafirisha gesi kwa wingi na kuongeza kuwa: Leo nimejifunza mambo mengi wakati nilipoonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na ninashukuru kupata fursa hiyo na kujifunza mambo mengi katika mazungumzo yetu.
 
< Nyuma   Mbele >

^