Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais wa Bolivia Chapa
24/11/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni (Jumanne) ameonana na Rais Evo Morales wa Bolivia na huku akiipongeza Bolivia na baadhi ya nchi za Amerika ya Latini kwa misimamo yao imara, ya kishujaa na ya kuvutia katika kukabiliana na ubeberu wa kambi ya kiistikbari, ametahadharisha kuhusiana na siasa hatari mno za Marekani duniani na katika eneo la Amerika ya Latini za kutaka kubadilisha utambulisho wa vijana wa nchi za eneo hilo na kusisitiza kuwa: Inabidi zitiwe nguvu irada na utashi na kuongezwe mawasiliano na ushirikiano (baina ya nchi huru duniani) kwa ajili ya kukabiliana na siasa hizo za kibeberu.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kusimama imara katika kukabiliana na siasa za kibeberu na za kupenda kujikumbizia kila kitu za Marekani kuwa ni fursa muhimu zaidi kuliko hata mafanikio iliyopata Bolivia na Rais Morales ya kuyafanya mafuta ya nchi hiyo kuwa mali ya taifa na kuongeza kwamba: Iran ilikuwa nchi ya kwanza kabisa duniani ambayo ilifanikiwa kutoka kikamilifu katika udhibiti wa Marekani kutokana na harakati huru na ya wananchi ya Imam Khomeini (Rahmatullahi Alayh) na kufanikiwa kusimama imara mbele ya upinzani na mashinikizo ya kijeshi, kiusalama na kiuchumi ya madola ya kibeberu na kambi mbili kuu za Mashariki na Magharibi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kuzungumzia nukta hiyo akisisitiza kwa kusema: Ni kwa msingi huo ndio maana Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikawa inamuunga mkono mtu yeyote katika sehemu yoyote ile duniani ambaye amesimama kukabiliana na ubeberu na uistikbari.
Vile vile ameashiria suhula na vipaji vingi vya wananchi wa Bolivia na kuongeza kuwa: Fursa hizo na vile vile uhusiano wa nchi mbili pamoja nyuga nyingi za ushirikiano ni mambo ambayo yanaweza kutumikia vizuri kwa ajili ya kulinda manufaa ya mataifa ya dunia na kuyawezesha kusimama kidete kukabiliana na mabeberu.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema, maendeleo ya kiuchumi ni jambo la lazima kwa Bolivia kwa ajili ya kujidhaminia uhuru wake wa kisiasa na kiuchumi na kuongeza kuwa: Mbali na maendeleo hayo ya nje na ya dhahiri, inabidi yaweko pia maendeleo ya batini na ya ndani ya nyoyo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezitaja siasa za Marekani duniani na vile vile katika eneo la Amerika ya Latini kuwa ni kubadilisha utambulisho wa wenyeji na vijana wa nchi hizo kwa kutumia mbinu mpya za mawasiliano na kutahadharisha kuwa: Kama Wamarekani watafanikiwa kwenye siasa zao hizo na iwapo wataweza kuzibadilisha fikra za vijana kuwa fikra za Kimarekani, wakati huo wataweza kuzidhibiti kirahisi sana nchini nyingine na hawatahitajia tena kufanya mapinduzi ya kijeshi na wala kuchukua hatua nzito zenye mashaka.
Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kutiwa nguvu utambulisho wa asili wa mataifa ya dunia na kuelimishwa vizuri vijana wa mataifa hayo utambulisho wao wa kweli, ni miongoni mwa njia nzuri za kukabiliana na siasa hizo za kibeberu za Marekani na kusisitiza kuwa: Ni jambo linalowezekana kupata ushindi kwenye vita hivyo kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kwa kutia nguvu irada na utashi wa mataifa.
Katika mazungumzo hayo, Rais Evo Morales wa Bolivia ameelezea kufurahishwa kwake na kupata fursa ya kuonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na amemwambia: Sisi tunakuhesabu kuwa wewe ni baba wa mapinduzi yote huru hususan mapinduzi ya eneo la Amerika ya Latini na tunajifunza mengi kutokana na matamshi yako yenye thamani kubwa, yanayotupa ilhamu na matumaini makubwa.
Bw. Morales ameutaja uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya mataifa mengine kuwa ni tatizo kubwa na kuongeza kuwa: Tangu mwanzoni kabisa mwa kuchukua kwangu madaraka niliwasisitizia Wamarekani walipotuonya kuhusu uhusiano wetu na Iran kuwa, sisi ni nchi huru na hatuombi ruhusa ya mtu yeyote katika kuweka uhusiano wetu na watu wengine.
Rais wa Bolivia amesisitiza pia kuwa nchi yake haitosalimu amri kamwe mbele ya mashinikizo ya Wamarekani na kuongeza kuwa: Sisi tumethibitisha kivitendo kuwa ni nchi huru baada ya kuyatangaza mafuta kuwa ni mali ya taifa na kwa hatua hiyo tumeweza kumaliza miaka ya udhibiti na uporaji wa Magharibi nchini mwetu.
Rais Morales ameongeza kuwa, kiwango cha maendeleo na huduma zinazotolewa kwa wananchi katika kipindi cha uhuru wa Bolivia kimepindukia mno kiwango cha kipindi ambacho nchi hiyo ilikuwa kibaraka wa Magharibi na huku akisisitizia udharura wa kupatikana uhuru wa kiuchumi chini ya kivuli cha uhuru wa kisiasa amesema: Leo hii uzalishaji ghafi wa kitaifa wa Bolivia umeongezeka mno na kufikia zaidi ya dola bilioni 36 ambalo ni ongezeko la mara nne zaidi ikilinganishwa na wakati Bolivia ilipokuwa mikononi mwa Magharibi.
Vile vile Rais wa Bolivia amezungumzia uzoefu na uwezo mkubwa wa Iran katika nyuga tofauti za kielimu na kiteknolojia na kuongeza kuwa: Iran ni Bolivia ni waitifaki wawili wa kihistoria, kiutamaduni na kiwananchi na ni matumaini yangu husiano wa nchi hizi mbili utastawishwa zaidi katika nyanja tofauti.
Rais Morales amesema: Bolivia daima imekuwa ikifurahishwa na kuishukuru misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu na tuna uhakika kuwa Iran itaendelea kuwa hivi hivi na utulivu wake.
Rais Evo Morales ameongeza kuwa: Bolivia nayo ni nchi yenye nguvu, yenye utulivu na iliyo imara chini ya kivuli cha kustawisha ushirikiano na uhusiano wake na nchi za kimapinduzi na za muqawama kama Iran.
 
< Nyuma   Mbele >

^