Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Makamanda na Maafisa wa Jeshi la Majini Chapa
29/11/2015
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo (Jumapili) ameonana na makamanda na maafisa wa Jeshi la Majini la Iran na huku akiashiria umuhimu wa bahari na maendeleo makubwa ya jeshi la baharini katika kutumia fursa nyingi za baharini, amesisitizia haja ya kuendelea Jeshi la Majini kujiletea maendeleo na kujiimarisha zaidi na kuongeza kuwa: Nguvu kazi salama, inayoonesha radiamalai ya haraka na yenye fikra na usiamiaji sahihi sambamba na kusimama kidete, kuwa na nia isiyotetereka, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kuwa na matumaini mema na mustakbali ndiyo mambo bora kabisa ya kuweza kuifikisha Iran ya Kiislamu katika nafasi kubwa na ya kihistoria inayostahiki kuwa nayo.
Katika mkutano huo uliofanyika kwa mnasaba wa maashimisho ya siku ya Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Udhma Khamenei ambaye ndiye Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amesema kuwa, maendeleo ya miaka ya hivi karibuni ya jeshi hilo yanaonekana kwa uwazi kabisa na kuongeza kuwa: Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, ulikuwa ukidharauliwa umuhimu mkubwa na adhama ya masuala ya baharini, lakini leo hii Jeshi la Majini limepiga hatua kubwa sana za maendeleo ingawa tab'an bado tuko mbali na nukta tuliyokusudia kuifikia.
Kiongozi Muadhamu wa Maipnduzi ya Kiislamu ameitaja bahari kuwa ni medani ya kupambana kishujaa na kiume na maadui na wakati huo huo kufanya harakati zenye taathira na kushirikiana vizuri na marafiki.
Ameongeza kuwa: Kuyafikia maji ya bahari kuu, kujiunganisha na pembe zote nne za dunia kupitia bahari na kuweza kuilinda nchi kutokea baharini ni miongoni mwa baraka za bahari ambazo inabidi wananchi na viongozi nchini wazizingatie na kujua thamani yake.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran amegusia pia umuhimu wa Bahari ya Oman na fukwe za Makran na kusema: Eneo hilo ni nukta ya kimsingi ya kutekelezea majukumu ya Jeshi la Majini. Aidha ametoa maagizo kadhaa ya lazima kwa serikali kwa ajili ya kulihuisha eneo hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema jambo la lazima la kuweza kulifanya Jeshi la Majini lifanikishe vizuri jukumu lake hilo ni kujijenga vilivyo hususan katika upande wa nguvu kazi inayofaa, salama na yenye radiamali ya haraka na kusisitiza kuwa: Uongozi na nguvu kazi nzuri hufanya miujiza kama ambavyo tumeshuhudia katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita ambapo nchi yetu ilikumbwa na matatizo ya kifedha na ya kibajeti na hadi hivi sasa matatizo hayo yapo lakini uzoefu unaonesha kuwa, inawezekana kuvuuka kwenye matatizo mengi kwa kuwa na uongozi mzuri hata kama kutakuwa na mapungufu, vizuizi bali hata kwa kuwa mikono mitupu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa uongozi wa Imam Khomeini (quddisa sirruh) kuwa ni dhihirisho la miujiza ya nguvu kazi na kuongeza kuwa: Imam wetu mtukufu, alitegemea nguvu za Mwenyezi Mungu na uwezo na ushawishi wake wa kipekee kuandaa mawimbi makubwa katika mkondo wa bahari ya wananchi na kufanikiwa kuuangusha mfumo kibaraka wa kisiasa licha ya mfumo huo kuwa na suhula na zana nyingi kupindukia.
Ameutaja ushindi wa kustaajabisha wa taifa la Iran katika vita vya kujihami kutakatifu na kufanikiwa taifa hili kumshinda adui aliyekuwa na zana na silaha za kisasa na ambaye alikuwa akiungwa mkono kila upande kisiasa na kijeshi, kuwa ni muujiza mwengine wa nguvu kazi na kusema: Leo hii uwezo na maendeleo ya taifa la Iran pamoja na vikosi vya ulinzi umeongezeka maradufu na inawezekana kufikia mustakbali unaong'ara zaidi taifa la Iran kwa kusimama kidete kuwa na irada na azma ya kweli pamoja na kuwa na matumaini mazuri kuhusu mustakbali na kutawakali kwa Mwenyezi Mungu.
Kabla ya hotuba ya Amirijeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu, Admeri Habibullah Sayyari, Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa ripoti fupi kuhusiana na kazi za jeshi hilo na kusema kuwa, leo hii Jeshi la Majini linapiga hatua mbele kwa uimara zaidi, kwa shauku na hamasa kubwa zaidi na hima ya hali ya juu ili liweze kuwa katika taraja na hadhi ya kuwa jeshi la taifa la Iran.
 
< Nyuma   Mbele >

^