Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Nasaha za Kiongozi Muadhamu Kuhusiana na Ziara ya Arubaini ya Imam Husain AS Chapa
30/11/2015
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatatu) katika darsa yake ya "Khariji" ya fikihi (darsa ya daraja la juu kabisa ya fikihi) amelitaja tukio lisilo na kifani la harakati adhimu na iliyojaa maana ya maandamano ya Arubaini ya Imam Husain Alayhis Salaam kuwa ni jambo jema la kubakia milele na kuongeza kuwa: Kuweza kukusanya pamoja "huba na imani" na "akili na hisia" ni katika sifa za kipekee za madhehebu ya Ahlul Bait Alayhimus Salaam na kwamba harakati iliyojaa mapenzi na kushiriki wimbi kubwa la wananchi wenye imani thabiti kutoka nchi tofauti duniani katika tukio hilo lisilo na kifani la Arubaini ya Imam Husain AS, bila ya shaka yoyote ni katika "sha'air" na alama za Mwenyezi Mungu.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia ukarimu na mapenzi makubwa ya wananchi wa Iraq wanaowapokea na kuwahudumia vizuri wafanya ziara ya Arubaini ya Imam Husain AS na hapo hapo ametoa nasaha kwa watu waliopata taufiki ya kushiriki kwenye harakati hiyo adhimu yenye utukufu mkubwa kwamba waitumie vizuri fursa hiyo ya Arubaini ya Imam Husain AS, na kusema, sisi tunaoangalia tukiwa mbali harakati hiyo adhimu tunatamani laiti tungelikuwa pamoja nanyi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kupata fursa ya kuwa na mawasiliano ya kimaanawi na ya kimapenzi makubwa na Watu wa Nyumba ya Bwana Mtume Muhammad (Swallallahu Alayhi Waalihi Wasallah) na kuwasuru watu hao wakubwa, bora, wenye nuru na waliojaa umaanawi ni katika mambo bora yanayoipambanua tafakuri ya madhehebu ya Kishia na madhehebu mengineyo ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Harakati adhimu ya wananchi kutoka Iran na nchi zote duniani na kushiriki katika maandamano makubwa ya Arubaini ya Imam Husain AS ni dhihirisho la sifa kubwa za kipekee za madhehebu ya Ahlul Bait Alayhimus Salaam kutokana na kwamba katika harakati hiyo kumejaa imani, itikadi thabiti ya ndani ya moyo na mafundisho sahihi kama ambavyo imejikita vilivyo pia huba na mapenzi makubwa ndani ya harakati hiyo.
Vile vile amewataka wafanya ziara ya Arubaini ya Imam Husain AS kuheshimu sheria na kanuni zilizowekwa na kusisitiza kuwa: Serikali imeweka sheria maalumu kwa ajili ya watu wanasafiri nje ya nchi na inabidi sheria hizo ziheshimiwe na si ruhusa kwa mtu yeyote yule kudharau sheria hizo.
 
< Nyuma   Mbele >

^