Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Awasilisha Siasa Kuu za Mazingira Chapa
02/12/2015
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaandikia barua wakuu wa Mihimili Mitatu Mikuu wa dola (Serikali, Bunge, Mahakama) na kuwakabidhi siasa kuu za masuala ya mazingira, ikiwa ni katika kutekeleza kipengee cha kwanza cha kifungu cha 110 cha Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kuanzisha mfumo mmoja ulioshikamana barabara wa kitaifa kuhusiana na mazingira, kuweko uratibu mzuri wa pamoja wa kusimamia vyanzo muhimu vya taifa, kuhesabiwa kuwa ni uhalifu kuharibu mazingira, umuhimu wa kuandaliwa mfumo wa ikolojia ya Atlasi (Atlas ecosystem), kutilia nguvu udiplomasia wa kulinda mazingira, kustawisha "uchumi kijani" pamoja na kuweka misingi madhubuti ya utamaduni na maadili ya kulinda na kuhifadhi mazingira, ni miongoni mwa maudhui kuu zilizomo kwenye siasa kuu za masuala ya mazingira zilizowasilishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa wakuu wa mihimili mitatu mikuu ya dola nchini.
Matini kamili ya siasa hizo kuu za masuala ya mazingira ambazo zimetolewa baada ya kushauriana na Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kama ifuatavyo:
 

Bismillahir Rahmanir Rahim
Siasa Kuu za Mazingira

1 - Usimamiaji wa pande zote, wenye uratibu wa pamoja na wenye mpangilio mzuri wa vyanzo muhimu mno vya mazingira (kama vile hewa, maji, udongo na anuwai zote za mazingira) kwa kuzingatia uwezo endelevu wa ikolojia hususan kupitia kuongeza uwezo unaofaa wa kisheria na kimuundo sambamba na kuwa na mtazamo wa kuwashirika vilivyo wananchi katika ufanikishaji wa suala hilo.
2 - Kuanzisha mfumo mmoja ulioshikamana vilivyo wa kitaifa kuhusu mazingira.
3 - Kufanyia marekebisho hali ya mazingira kwa lengo la kuwa na muundo uliokusanya mambo yote yanayohusiana na mazingira salama na kuchunga uadilifu na haki za vizazi vyote.
4 - Kuweka kinga na kuzuia kuenea anuwai kwa anuwai za uchafuzi uliopigwa marufuku na kuhesabiwa kuwa ni uhalifu kuharibu mazingira na kutolewa adhabu yenye taathira na itakayozuia vitendo vya wachafuaji na waharibufu wa mazingira na kuwalazimisha wafidie hasara waliyoyasababishia mazingira.
5 - Kuweko ufuatiliaji endelevu na kudhibitiwa vizuri vyanzo na sababu zinazopelekea kuchafuliwa hewa, maji, udongo pamoja na uchafuzi wa mbali mbali wa sauti, mawimbi haribifu na mabadiliko yasiyo mazuri ya ikolojia, na ulazima wa kuchungwa viwango na vielelezo vya mazingira katika sheria na maamuzi ya nchi sambamba na kuweko mipango maalumu ya ustawi na kutumiwa vizuri ardhi.
6 - Kuandaa mfumo maalumu wa "Ikolojia ya Atlasi" ya nchi na kulinda, kuhuisha na kutumia vizuri na kustawisha maliasili jadidika kama vile bahari, maziwa, mito, mabwawa, madimbwi, vyanzo vya chini ya ardhi vya maji, misitu, udongo, maeneo ya malisho ya wanyama na anuwai kwa anuwai za maliasili hususan zinazohusiana na maisha ya wanyama pori na kuweka mipaka ya kisheria katika matumizi ya vyanzo hivyo kulingana na uwezo wa kiikolojia (uwezo unaoweza kubeba matumizi hayo na kujijadidisha) kulingana na vigezo na vielelezo endelevu, kusimamia vizuri mfumo wa maeneo nyeti na yenye thamani kubwa ya kiikolojia kama vile mabustani ya taifa na athari za kimaumbile za taifa na kulindwa vyanzo vya kijenetiki na kuhakikisha vinakwea daraja hadi kufikia viwango vya kimataifa.
7 - Kusimamia vizuri mabadiliko ya tabianchi na kukabiliana na mambo yanayotishia usalama wa mazingira kama vile kupambana na kuenea jangwa, hali ya hewa ya vumbi na hususan ukame na vitu vinavyopelekea kuenea vijidudu maradhi na vinururishi na kupanua wigo wa kuangalia mustakbali na kuelewa vizuri mambo mapya yanayozuka ndani ya mazingira na kuyadhibiti.
8 - Kustawisha uchumi kijani kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
8 - 1 - Kuwa na viwanda vinavyozalisha kaboni chache, kutumia nishati safi, mazao salama ya kilimo na ya kibayotiki na kusimamia vizuri matumizi ya mbolea na udhibiti wa majitaka kwa kutumia nafasi na uwezo wa kiuchumi, kijamii, kimaumbile na kimazingira.
8 - 2 - Kufanyia marekebisho vigezo vya uzalishaji katika sekta tofauti za kiuchumi, kijamii na kutumia vizuri kigezo cha matumizi ya maji, chemchemu, chakula bidhaa nyinginezo na nishati hususan kulipa nguvu suala la kueneza matumizi ya mada za nishati zinazolinda mazingira.
8 - 3 - Kustawisha sekta ya usafirishaji na uchukuzi kijani wa uma na usiotumia mada za fosili ikiwa ni kulipa kipaumbele suala la kutumia umeme na kuongeza vyombo vya usafiri vinavyobeba watu wengi hususan katika miji mikubwa.
9 - Kuweko mlingano sawa wa kisekta na kulindwa ubora wa maji ya chini ya ardhi kupitia utekelezaji wa operesheni za kuvuna maji ya mvua, kusambaza maji, kusimamia mambo yanayopelekea kupungua matumizi ya maji ya chini ya ardhi, kuchemsha na kudhibiti uingiaji wa uchafu katika maji hayo.
10 - Kuandaa mfumo wa ukaguzi wa mazingira nchini kwa kuzingatia thamani na gharama za mazingira (uharibifu, uchafu na uhuishaji) katika hesabu za taifa.
11 - Kuunga mkono na kuhamasisha uwekezaji na teknolojia zinazolinda mazingira kwa kutumia njia zinazofaa kama vile ushuru na kodi kijani.
12 - Kubuni hati ya kimaadili ya mazingira na kueneza kiumakini na kwa njia madhubuti utamaduni na maadili ya kulinda mazingira kupitia thamani na vigezo bora vya Iran - Kiislamu.
13 - Kunyanyua kiwango cha utafiti na uhakiki wa kielimu na kutumia vizuri teknolojia za kisasa za kulinda mazingira na uzoefu mzuri wa kijadi katika suala zima la kulinda mlingano wa mazingira ya jadi na kuzuia kuchafuliwa na kuharibiwa mazingira.
14 - Kunyanyua kiwango cha welewa, elimu na maarifa kuhusu mazingira katika jamii na kutia nguvu utamaduni na maarifa ya kidini ya kushiriki na kubeba majukumu ya kijamii hususan katika suala la kuamrishana mema na kukatazana mabaya kwa ajili ya kulinda mazingira na kuenezwa welewa na maarifa hayo kati ya watu wa matabaka na viwango vyote vya jamii.
15 - Kutia nguvu udiplomasia wa mazingira kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
15 - 1 - Kufanya jitihada za kubuni na kutia nguvu taasisi za kieneo kwa ajili ya kukabiliana na hali ya hewa ya vumbi na uchafuzi wa maji.
15 - 2 - Kustawisha uhusiano na kuvutia watu kushiriki katika miradi mbali mbali na kuleta ushirikiano wenye malengo maalumu na wenye taathira nzuri wa pande mbili, wa pande kadhaa, wa kieneo na wa kimataifa katika suala zima la kulinda mazingira.
15 - 3 - Kutumia kwa njia sahihi na kwenye taathira nzuri - fursa na vihamasishaji vya kimataifa - katika harakati ya kuelekea kwenye uchumi unaozalisha kaboni chache na kusahilisha ugurishaji na ustawi wa teknolojia na ubunifu wa kisasa unaohusiana na suala hilo.

 
< Nyuma   Mbele >

^