Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Matamshi ya Kiongozi Muadhamu Kuhusu Kuuawa Shahidi Alimu Muumini na Madhlumu, Sheikh Nimr Chapa
03/01/2016
 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi katika darsa yake ya "Khariji" ya fikihi (darsa ya daraja la juu kabisa ya fikihi) amekilaani kitendo cha Saudi Arabia cha kumuua shahidi alimu muumini na madhlumu Sheikh Nimr Baqir al Nimr na huku akisisitizia ulazima wa mataifa ya dunia kutekeleza vizuri majukumu yao kuhusiana na jinai hiyo pamoja na jinai nyingine kama hizo zinazofanywa na Saudia katika nchi za Yemen na Bahrain amesema: Ni jambo lisilo na shaka kuwa, damu iliyomwagwa kidhulma ya shahid huyo madhlumu itatoa athari zake haraka sana na kisasi cha Mwenyezi Mungu kitawakumba wanasiasa wa Saudia.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amesema: Alimu huyo madhulumu si kwamba aliwachochea watu wabebe silaha na wala hakufanya njama zozote, bali kitu pekee alichofanya ni kulaumu hadharani na kutekeleza wajibu wake wa kuamrisha mema na kukataza maovu kutokana na ghera zake za kidini.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekutaja kuuliwa shahidi Sheikh Nimr na kumwagwa damu yake kidhulma kuwa ni kosa kubwa la serikali ya Saudia na kuongeza kuwa: Mwenyezi Mungu Mtukufu haachi damu ya mtu asiye na hatia imwagwe kidhulma vivi hivi, hivyo athari za dhulma hiyo zitawakumba haraka mno wanasiasa na waendeshaji wa utawala huo wa Saudia.
Aidha amelaumu vikali kimya cha wanaodai kutetea uhuru, demokrasia na haki za binadamu na uungaji mkono wao kwa utawala wa Saudia ambao umemwaga ya mtu asiye na hatia ambaye kitu pekee alichofanya ni kukosoa kwa maneno yao utendaji wa utawala huo na kusisitiza kuwa: Ulimwengu wa Kiislamu na dunia yote watekeleze vizuri majukumu yao kuhusiana na suala hilo.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la kuwatesa na kuwakandamiza wananchi wa Bahrain kunakofanywa na wanajeshi wa Saudia pamoja na kuharibiwa misikiti na nyumba za wananchi hao na vile vile mashambulizi ya zaidi ya miezi kumi sasa ya Saudia dhidi ya wananchi wa Yemen kuwa ni mfano mwingine wa jinai zinazofanywa na utawala wa Saudi Arabia.
Amesisitiza kuwa: Watu ambao wana mapenzi ya kweli ya mustakbali mwema wa mwanadamu na haki za binadamu na uadilifu, wanapaswa kuyafuatilia vizuri masuala hayo na wasiyanyamazie kimya mambo hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema: Ni jambo la yakini kwamba shahid Sheikh Nimr atapata radhi na fadhila za Mwenyezi Mungu na bila ya shaka yoyote, kisasi cha Mwenyezi Mungu kitawakumba madhalimu ambao wameidhulumu roho yake na hilo ni jambo la kutia faraja sana.
 
< Nyuma   Mbele >

^