Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Kiongozi Muadhamu Aonana na Waendeshaji wa Kongamano la Taifa la Fikihi ya Sanaa Chapa
13/01/2016
 Miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa wakati alipoonana na waendeshaji na wasimamiaji wa Kongamano la Taifa la Fikihi ya Sanaa, mkutano ambao ulifanyika Januari 11, 2016, imesambazwa leo katika kituo cha makongamano cha Ghadir cha ofisi ya Tablighi ya Kiislamu ya Hawza (Chuo Kikuu cha kidini) ya Qum.
Katika mkutano huo, Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei aligusia umuhimu wa suala la sanaa na kuelezea kufurahishwa kwake na kuona kuwa chuo kikuu cha kidini kimeingia katika uga wa fikihi ya sanaa na kuongeza kuwa, sanaa, ni kitu kilichobarikiwa cha kibinadamu na ni matunda ya kuwa na tafakuri pana, hisia na dhuku kali na ni sehemu ya maisha ya mwandamu. Amesema, kati ya wanavyuoni na mafakihi wa hawza (vyuo vikuu vya kidini) kumejaa watu waliobobea katika sanaa na ambao ni majimbi katika bahari za tungo na fasihi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesema ni jambo la dharura na lenye baraka nyingi la kufanya uhakiki, kupiga mbizi na kubainisha vizuri fikihi ya sanaa katika jamii. Ameongeza kuwa, fikihi ndiyo inayosimamia mambo yote katika maisha ya mwandamu na sanaa ni moja na mambo hayo ambayo fikihi inapaswa kuyashughulikia.
Amesema, kazi ya kuchunguza, kuhakiki, kufanya utafiti na hatimaye kutoa hukumu na nadharia za kifikihi kuhusiana na sanaa ni kazi ambayo inahitajia kuwa na utambuzi wa kina kuhusiana na sanaa, mipaka na hududi zake.
Amesema, Uislamu si tu kwamba unakubaliana na sanaa, bali hata unashajiisha kufanya kazi za sanaa, na mifano mingi ya sanaa katika historia ya Uislamu ni uthibitisho wa namna dini hiyo ya Mwenyezi Mungu inavyolipa umuhimu suala la sanaa na kuhamasisha kufanyiwa kazi.
Ayatullah Udhma Khamenei ameashiria namna sanaa ilivyojikita vilivyo katika jamii za mwanadamu leo hii na athari zake za moja kwa moja katika fikra, roho na mtindo wa maisha ya watu na kuongeza kwa kusema: Amma kuhusiana na baadhi ya fatwa maarufu kuhusu masuala ya sanaa ni kwamba inawezekana kuja na fatwa mpya kwa kupiga mbizi na kuzama zaidi katika fikihi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuhusu mambo ya lazima ya kuja na vitu vipya katika fikihi ya sanaa kwamba: Inabidi usuli na misingi ya fikihi ichungwe kikamilifu katika suala hilo na inabidi hukumu na fatwa zitolewe kwa kutumia usuli na msingi wa kutoa fatwa wa wanavyuoni wa Kishia na kwa kutegemea Qur'ani na Sunna, bila ya kuathiriwa na wimbi na anga inayotawala katika jamii.
Aidha amesifu hatua ya kuanzisha sunna nzuri ya kuiingiza fikihi katika sanaa na kuitisha kongamano la fikihi ya sanaa na amewasisitizia waendeshaji na wasimamiaji wa kongamano hilo kwa kuwaambia: Kazi hii ilipaswa ianze zamani sana na kwa vile hivi sasa imeshaanza, inabidi iendelee bila ya kusita.
 
< Nyuma   Mbele >

^